4. Maono na matukio aliyopewa Raymond Aguilera, July 1990.

Ni Julai 13, 1993, Nakwenda kurekodi Maono na Matukio yaliyotokea miaka mitatu iliyopita kutoka kwenye kumbukumbu yangu ya kichwani kwa kuwa sikuwa nimeinasa kwenye kanda ya kurekodia. Asubuhi yote Bwana amenikumbusha kuwa niiandike kwenye kitabu cha unabii (nimeamua kufunga na kuomba wakati huu ninapoandika matukio/maono haya kwani mapambano ya kiroho yanayoambatana na matukio haya ni ya ajabu mno)

Maono na Matukio:

Siku moja mchana wakati nikomba kitandani mwangu, niliona maono ya Kristu akiwa amechukua msalaba akitelemka kweye mtaa wa fulani na mtu moja akiwa ana mchapa mjeledi kwa ukali sana.

Kisha nikamsikia mtu Fulani akisema "Ukiendelea kumchapa namna hiyo utamuua kabla hajasulubiwa".

Nilikuwa namwona Yesu akiwa ameanguka chini na akiwa na maumivu makali sana na mara mtu moja analazimishwa kutoka kwenye kundi la watu achukue msalaba wake. Kufika tuu kwenye sehemu ya kusulubishwa mara nikaona watu kadhaa wakimshika Yesu wakati mtu mmoja wa miraba minne akimpigilia msumari mkono wake wa kushoto kwenye msalaba. Huyo mtu wa miraba minne alikuwa na mikono mikubwa na alivaa kitambaa kwenye uso wak,e, alinyanyua nyundo ya mti na kisha akampigilia msumari kwenye mkono au kiganja cha mkono wa Kristu. Nilikuwa naona uchungu Kristu aliokuwa nao wakati mwili wake uliponyanyuka juu kwa kishindo cha nyundo kwenye msumari. Kwa jinsi fulani nilikuwa naona nyundo hiyo ikija chini kwa Yesu kutoka ardhini kanakwamba inanijia mimi.

Nakumbuka nikiwa nimeshutushwa sana kuona mambo yanayotendeka katika ulimwengu wa roho. Kwa jinsi hiyo tena niliona aidha mkono wake wa kulia ukipigiliwa msalabani kwa namna ile ya kwanza. Nilikuwa naona nguvu aliyekuwa akitumia yule mtu wa miraba mine kwenye nyundo yake hiyo. Baada ya mikono yake miwili kupigiliwa msalabani miguu yake pia ilipigiliwa hali Yesu akijaribu kuyanasua bila mafanikio. Nilikuwa naona watu hao wakinyanyua msalaba huo na Yesu nakuusimika kwenye shimo iliyotayarishwa kwenye ardhi. Maumivu ya Yesu yalikuwa dhahiri wakati msalaba uliponyanyuliwa juu. Kisha naamini mambo zilipigiliwa chini ya msalaba kuufanya usimame.

Naona kama jambo la ajabu kwa mimi kukumbuka kinagana picha ya yule mtu wa miraba minne na ile nyundo yake ya mbao baada ya miaka hii yote iliyopita. Nakumbuka nilikuwa nimelala kitandani nikiyawaza mambo hayo niloyoyaona katika ulimwenguwa roho. Kisha bila onyo mkono wangu wa kushoto ulianza pole pole kuondoka kutoka mwilini mwangu Niljaribu kuuzuia bila mafanikio. Nikiwa na mkono ulionyooshwa mtu yule yule mnene niliyemwona hapo mwanzo kwenye maono ya Kristu alinyanyua nyundo ile yambao hewani. Nakumbuka nilijaribu kuondoa mkono wangu bila mafanikio wakati nyundo ikiendea juu na kuja chini kwa nguvu kubwa juu ya msumari katika ulimwengu wa roho. Nilianza kulia kwa nguvu kuweweseka nikapiga mateke, nikaanza kupiga yowe nikijaribu kujinasua bila mafanikio. Nilikuwa nalia nakupiga kelele nikitumia nguvu zangu zote kujinasua. Hapakuwa na maumivu ya kweli, ila mshtuko wakutokuweza kujinasua na huku nikona nyunda ikija chini.

Kisha mtu yule alionekana kwa mara nyingine tena na mkono wangu wakulia ukaanza kusogea kutoka mwilini mwangu, nikajaribu kupiga ili usinyooke kama ule wa kwanza bila mafanikio nao pia ukapigiliwa msumari. Nikajikuta mikono yangu yote miwili imenyoshwa juu ya kitanda changu na kupigiliwa misumari nikajiona kuwa sina njia ya kuyanasua. Kisha miguu yangu ikaanza kujisogeza pamoja. Nilijaribu kuyazuia bila mafanikio. Nilijaribu kujinasua kwa nguvu zangu zote bila mafanikio kwa mtu yule tena akajitokeza akafanya kama alivyofanya kwa mikono. Kisha, msalaba pamoja na mwili wangu juu yake ukasimamamishwa nakuwekwa imara juu ya ardhi. Nikajiona mimi niko pamoja na maelfu na maelfu ya watu waliokuwa wame sulubishwa misalabani. Milima hii ilikuwa nikama yote imejaa misalaba na watu juu yao, watu wengine walikuwa wamenyongwa na wengine wameteswa. Wingi walikuwa wamesulubiwa lakini wengine walikuwa wamenyongwa na wengine wameteswa. Ilkuwa kama sehemu kubwa sana ya makaburi ya Misalaba. Ghafla nikaona nyota nyeupe ikijitokeza kutoka ndani ya mwanga mweupe ulioko juu ya mlima, nami nikatambua kuwa ni Yesu. Nilimuliza Yesu kuhusu kilicho kuwa kina tokea na sikapokea jibu. Kisha nikahisi na kuona kitu kinacho onekana ni utupu mweusi ambao hauendi popote kushotoni mwangu, ila nyuma yangu. Nikaanza mara mmoja kumwambia Yesu kuwa hapa siyo mahala pangu. Nakumbuka kumwambia kuwa hapa siyo mahala pangu ila mahala pangu nipamoja na ile misalaba mingine upande ule mbali kidogo na ule utupu Lakini Kristu hakusema neno lolote. Alibaki tu juu ya mlima huu na kuniangalia. Nikamlilia na kumlilia asikie ombi lake bila mafanikio. Yeye alibaki juu ya mlima huu katika ukimya mkubwa.

Kisha baada ya kitu kama dakika ishirini hivi kupita, Kristu akasema, "Watu walioko kwenye misalaba ni waliokuwa wamesulubishwa kwa ajili Yangu misalaba ni watu waliosulubishwa kwa ajili Yangu Kwa miaka mingi ya hadi sasa."

Tukio hili lilikuwa la kuchosha. Nilingoja nakungoja kisha baada ya kitu kama dakika ishirini kupita maono mengine yalianza kupita Mbele ya macho yangu. (Sintaandika hayo maono niliyo yaona kwa sababu Bwana hakuniruhusu niyaandike. Hivyo nitaishia hapo kuhusu maono na matokeo hayo.)

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.