5. Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 29 Julai 1990 na kuandikwa tarehe 6 Augusti 1990.
Vema, leo ni August 6, 1990. Nadhani inanibidi kuandika tukio fulani katika kitabu changu cha kumbukumbu ambacho kilitokea muda uliopita.
Kurudi kidogo nyuma nadhani ilikuwa Julai 29, siku ya Jumapili jioni. Nilitembelewa na rafiki yangu. Tulikaa naye hadi saa 9 usiku hivi tukiongea kuhusu Ukristu. Rafiki yangu huyo alifika muda wa saa 4 usiku; hivyo tuliongea kwa muda kama wa masaa matano hivi. Baada ya rafiki yangu huyo kuondoka nilienda kitandani nikalala usingizi wa fofofo, kisha kwa ghafla kitu kikavuta mkono wangu wa kulia kwa nguvu kubwa sana na kuelekea juu angani, lakini kwa vile nilivyo kuwa nimechoka sana sikupenda upumbavu wowote kutoka katika ulimwengu wa kiroho. Hivyo niliuvuta mkono wangu ndani ya matandiko kwa nguvu kubwa kupinga nguvu za hicho kitu. Kisha nikasema, "Shetani niachia mara moja! Sina wakati wa kustahimili upumbavu wako," kisha nikaviringika na kuendelea kulala.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )