6. Matukio aliyopewa Raymond tarehe 6 Augusti 1990 kama saa 9:00 usiku. (Kutoka kumbukumbu ya fahamu na mkanda wa kunasia sauti.)
Nilipatwa na tukio lisilokuwa la kawaida usiku huu, na ilinisumbua. Rafiki yangu alinipigia simu na tukazungumza naye hadi saa 8 za usiku, lakini baada ya kukata simu na kwenda kulala kitu fulani kiliniamsha. Sielewi kilikuwa ni kitu gani. Siwezi kuielezea, lakini nilikisikia na nilikihisi kuwa kilikuwa ni kitu kilicho kuwa kikipanda ngazi kuja kwenye chumba changu cha kulala na ndicho kitu hicho kilichoni amsha.
Ni mmoja wa ule msisimko wa mwili unaokupata wakati unadhani mtu au kitu fulani kipo ndani ya chumba chako lakini hukioni wala hukisikii, ila unahisi kuwa kipo. Sikukiona kilipokuwa kinakuja kwenye ngazi kwani mlango wangu wa chumba; ulikuwa umerudishwa na kufungwa kwa ufunguo, lakini nilipotazama kwenye mlango wangu wa chumba niliona hivi vivuli viwili vyeusi vikiingia kupitia mlango wangu huo ambao umefungwa.
Mmoja kilikuwa na umbile la mwanaume na kingine kilikuwa na umbile la mnyama mdogo. Mimi niliamua niendelee kulala hapo na kuangalia hivyo vifuli viwili vyeusi vikienda hadi kwenye miguu ya kitanda changu. Kilicho kuwa cha ajabu ni kuwa, vilikuwa vivuli vyeusi na wala si watu na chumba changu kilikuwa kwenye giza nene lakini bado nilikuwa naviona. Nashindwa jinsi ya kueleza ni kwavipi naviona vivuli hivyo vyeusi kwenye chumba changu cha giza. Lakini nilikuwa naweza kuviona.
Kisha baada ya kivuli cha mwanaume kusimama pale na kuangalia kile kivuli kidogo kikaanza kutambaa chini ya matandiko yangu na kujiviringisha kwenye miguu yangu na kisha kikaendelea kutambaa ndani ya blanketi kikielekea kwenye uso wangu karibu na mwili wangu. Mwanzoni nilidhania labda ni mwanangu Stefano kwenye miguu ya kitanda changu kwani wakati fulani huwa anaingia na kuchukua nguo zake au taulo.
Lakini nilipokuwa nimelala pale nikiangalia blanketi langu likawa linaenda juu chini juu chini na kusogea kuja usoni mwangu, nikadhani labda ni mbwa wetu Leroy, na kwa kuwa sikupenda nipatwe na viroboto kwenye kitanda changu; nikasema kwa sauti ya ukali "Leroy umefika fikaje hapa juu?" lakini kwa kuwa bado kinaendelea kunyata kuja kwenye kichwa changu nikasema tena "ulifika fikeje hapa?" nikageuka ilinimguse, lakini hapa kuwa na kitu na badala yake blanketi iliyokuwa imenyanyuka ilianguka utupu.
Sikujua la kufanya. Hivyo niligeuka nikanyanyua Bibilia yangu kilichokuwa karibu na kitanda changu na kukiweka mahala pale ambako kile kitu kilipotelea chini ya blanketi langu. Lakini kile kivuli kilicho kuwa na sura ya binadamu kilisimama pale kwenye miguu ya kitanda changu kimetulia kikiangalia, na kisha kikapotea baada ya kile kivuli kidogo kama mnyama kupotea. Labda nilikuwa mjinga au nilikuwa nimeshtuka sana kwani baada ya kuweka Biblia juu ya kitanda, niliendelea kulala. Nashindwa kujieleza ila ninachojua ni kuwa nilijisikia ni salama na amani baada ya kukiweka Biblia ile juu ya mahala pale patupu ambako kile kivuli cha mnyama kilikuwepo. Hayo ndiyo niliyotaka kuyaeleza.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )