8. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 3 Desemba 1990, kwa lugha ya Kihispania.

Ndiyo, una hali gani?

Ndiyo, una hali gani?

Nakupenda sana, kwa Moyo Wangu wote,

Upendo Wangu, Upendo Wangu, Upendo Wangu,

Unakupenda sana.

Watu wote wa dunia

ni kama Moyo Wangu, Ni kama Moyo Wangu.

Moyo wa dunia,

Ah, ulivyopendeza, ulivyo mzuri,

Nawapenda, Nawapenda sana.

Oh, Warembo Wangu,

Warembo Wangu

kwa Damu nyekundu ya Yesu,

kwa Damu nyekundu ya Yesu

Mwanangu, Mwanangu wa Pekee,

Nampenda sana,

aliyekufa kwa ajili yenu, kwa sababu

Nawapenda sana.

Nawapenda sana.

 

Wakati umewadia, wakati umewadia.

Tazama dunia inakuja.

Dunia itakuja kuisha.

Shetani,

Shetani hatakuwapo,

Shetani hatakuwepo kwa sababu

Muda wa shetani,

Muda wa shetani umeisha.

Muda wa shetani umeisha.

Nami, Mungu wa dunia yote,

wa Mbinguni, wa kila kilichokuwepo, kilichopo, na kitakacho kuwapo,

Nawaambia kuwa muda umewadia.

 

Imeanza.

Parapanda,

Parapanda ya Mbinguni

Parapanda ya Mbinguni ililia jana,

 

katika sehemu zote za dunia, sehemu zile tisa.

Ni zangu, ni zangu tena,

 

na shetani hana mahali tena pa kulaza kichwa chake.

Sasa yeye ni shetani wa angani kwa sababu

 

Nimeipokonya ardhi

Ile niliyompa miaka mingi iliyopita.

Nimempokonya ardhi yake.

Kwa sababu dunia, dunia itakuja kuisha.

Nataka Wanangu na Mabinti Zangu,

Wanangu na Mabinti Zangu, walio na macho ya kuona,

na walio na masikio ya kusikia.

Sikieni Maneno yangu!

Wakati umeanza. Wakati umeanza.

Watu wa dunia

fungueni macho yenu, na masikio yenu.

Lazima msikie Maneno

ya Watakatifu watakao kuja kuwaambia.

Watakuja kuwaambia ukweli,

na ukweli utakuja kutimia.

Kwa sababu shetani wa angani hawezi kuzuia mazungumzo.

Neno haliwezi kuzuiwa kwa sababu

Siku imefika ambayo nimewaambia miaka mingi iliyopita

Ilikamilishwa jana

Jumapili, jana, Desemba 2,

jana.

Sikieni Maneno Yangu Watoto Wangu.

Sikieni Maneno Yangu Watoto Wangu.

Sikieni Maneno Yangu Watoto Wangu, kwa sababu

wakati tayari umekwisha fika,

Lakini Ukweli, Ukweli Watoto Wangu

hauwezi kuzuiwa.

Shetani hawezi kuzuia Neno la Ukweli,

Kwa sababu Mimi Ndimi Ukweli.

Mimi ndiye niliye uunda Ukweli

Shetani atawala ninyi.

Shetani atawala ninyi.

Na iwapo hamsikii Maneno yangu,

mtakwenda kuishi na shetani

kwa siku zote ambazo ziko,

kwa siku zote ambazo ziko Mbinguni,

kwani una nafasi moja tu

Sikieni! Sikieni!

Wanangu na Mabinti zangu sikieni,

Sikieni Wanangu na Mabinti zangu,

wakati umefika.

 

Sikia neno la Haki,

mazungumzo, Neno, Maneno ya Haki.

kwa sababu nawapenda sana kwa Moyo Wangu wote.

Nawapenda kwa Moyo wangu wote.

Nataka kila mmoja anisikie Mimi kwa sababu

Mimi ni Mungu wenu,

Mimi ni Mungu wenu,

Mimi ni Mungu wenu.

Mimi ni Baba,

Baba wa vyote,

wa kila kilichokuwapo, kuwapo, kuwapo,

na kilichopo, na kilichopo,

namtafahamu

kwamba nitakuwapo milele

hapa, hapa, hapa.

Nyakati zote

pamoja na Mwanangu Yesu,

pamoja na Mwanangu Yesu,

pamoja na Roho Mtakatifu.

Pamoja na Roho Mtakatifu,

Atakwenda kuwaonyesheni ninyi

 

Atawafundisha ninyi

Yote mnayohitaji kujua.

Fungueni macho yenu,

Fungueni macho yenu na masikio yenu,

Kwani zitakuwepo

Ishara nyingi angani,

duniani, ndani ya vichwa vyenu, ndani ya akili zenu.

Kutakuwa na ishara nyingi,

na mtakuja kujua

Kwamba Mimi Ndimi Baba yenu.

Baba yenu anawaambia ukweli kwa sababu

Kila kilicho cha haki ni cha ukweli na Mimi Ndimi huo Ukweli.

Wekeni masikio yenu ardhini,

wekeni masikio yenu ardhini

na Umsikie Roho Mtakatifu,

kwani Miguu ya Roho Mtakatifu

itaanza kutoa kishindo cha sauti

sauti ambayo dunia nzima itakuja kuisikia.

Kwani kutatokea vita angani, angani.

Tazama angani, kutakuwa na vita.

 

Shetani, shetani anaogopa

kwani anajua kuwa wakati umefika.

Imeanza. Ni sherehe!

Ni sherehe ya Mbingu na Dunia.

 

Ni sherehe Wanangu, na Mabinti zangu.

Ni sherehe, Malaika wote wana furaha kubwa,

Wanafuraha sana kwa sababu imeanza.

Kimeanza, nilicho kisema

miaka mingi iliyopita, miaka iliyo pita,

kwenye sheria, kwenye sheria,

ile niliyoinena kwa Wanangu, baba zenu wa miaka mingi, iliyo pita.

Kwani niliwaambia Ukweli,

na Ukweli utakuja kutimia.

Hakuna! Hakuna!

Kitakacho zuia Ukweli

Kwani Mimi Ndimi Ukweli,

na Ukweli ni Mungu

pamoja na Mwana na Roho Mtakatifu.

Nisikieni Mimi! Nisikieni Mimi!

Kwa masikio yenu, kwani nafasi

mliyonayo ni ya mara moja tu,

ni ya mara moja tu; Wanangu na

Mimi nawapenda sana,

Ninawapenda sana,

Ebu njoni tu kwangu Wanangu,

mniambie dhambi zenu,

mniambie dhambi zenu,

kwa mioyo yenu yote,

kwa mioyo yenu yote,

na kama mtaniambia dhambi zenu

mnaweza kuja na Mimi.

Hiyo pekee inatosha. Ni rahisi tu.

Iko hapo tu mbele ya pua zenu,

mbele ya pua zenu Watoto Wangu.

Tazama! Tazama!

Nipo hapa mbele yenu

Mikono Yangu ikiwa imeinuliwa juu

na Mikono yangu pale.

Nataka niwaguse ninyi,

Nataka niwaguse

kwa mikono yangu,

iko pale,

iko pale mikono yangu,

mniguse, Mniguse Mimi

Lakini nataka muwe Wasafi.

Nataka muwe Wasafi Wanangu.

kwani hamwezi kuja pamoja nami kama ni wachafu.

Hamwezi kuja kwa sababu

ya milango ya Mbinguni,

kwani kila kilichopo Mbinguni ni kisafi,

ni kisafi, ni kisafi

na hakuna aliyemchafu

atakayeweza kuja, anatakayeweza kuja.

Mnisikilize Mimi Wanangu

Hakuna awezaye kuja kama ni mchafu.

Niambieni dhambi zenu,

niambieni dhambi zenu kwa Moyo Msafi,

Nami nitawasikiliza, Nitawasikiliza ninyi.

Haijalishi ulichokifanya,

haijalishi ulichokinena,

au ulichokifanya,

kwani cha maana ni kuwa, Moyo wako ni Msafi,

pamoja na akili yako,

na roho yako ikiongea na Mimi,na akili yako, kuhusu kilicho cha Haki.

Mnisikie! Mnisikie!

Huyu ni Baba.

Baba wa yote Yaliyoko na Yatakayo kuwapo.

Ninyi mlio na Roho Mtakatifu ,

Mlio Wasafi,

mtakuwa pamoja nami Mbinguni

Kwa sababu Mimi ni Mungu wenu,

nanyi ni Wanangu.

Mnisike! Mnisikie!

Safisheni masikio yenu, Safisheni masikio yenu

kwa sababu mtakuja kuona,

mtakuja kutishika

na mtakuwa mmechelewa sana.

 

Mtakuwa mmechelewa

na Mimi ninataka ninyi nyote mje pamoja Nami.

 

Kwa sababu Mimi ni Baba wa wote,

Mimi ni Baba wa wote pamoja na Mwanangu,

na Roho Mtakatifu.

Mimi ni Baba wa wote,

Mimi ni Baba wa yote.

 

Mwanangu ana Sheria,

Mwanangu ana Sheria.

Nataka nyote Mpemdeni Yeye, kwa Mioyo yenu yote,

kwa sababu kilicho Changu ni Chake,

na kilicho Chake ni Changu.

Yeyote ampendaye Yeye, anipenda Mimi.

Mnisikie! Mnisikie!

Roho Mtakatifu atakuja kuwafundisha ninyi

yote mnayopaswa kufahamu,

kwani Nawapenda sana.

Machozi yangu, Machozi yangu ni kwa wale

ambao hawaji pamoja Nami,

Kwani walikuwa na nafasi,

Walikuwa na nafasi,

Lakini hawakuona wala kusikia.

 

Kama hawasikii au kuona,

hawatakuwa pamoja Nami.

Kwani shetani atakuwa amewachukua kwa ridhaa yao.

Lakini Moyo Wangu unaumia endapo nitampoteza hata mmoja.

kama nitampoteza mmoja itaumiza Moyo Wangu,

Lakini Sheria,

Sheria ya Mwanangu lazima itimizwe,

Lazima itekelezwe.

Kwani vita vimekwishaanza.

Parapanda, Parapanda ya Mbinguni,

Na ya duniani imekwisha anza.

Imeanza, Watoto Wangu.

Tazama mawinguni,

Tazama mawinguni,

Kwani imekwisha anza.

Nisikieni!

Huyu ni Baba yenu akitokwa na Machozi,

Na Machozi Machoni Mwangu.

Mnisikie! Mnisikie!

Wakati karibu umetimia

Ogopeni, ogopeni,

kwani wakati unakuja.

Ogopeni, kwa mioyo yenu yote,

kwa sababu Mimi sitaweza kuwasaidia,

kama hamtafungua macho yenu na masikio yenu.

Nawapenda sana.

Nawapenda sana.

(kumb. iliyotolewa)

 

Ufunuo Sura ya 2

Ezekieli Sura ya 35

Isaya sura 13, 14, 18, 48

Kitabu cha Yona


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.