44. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 4 Mai 1992 saa 1:29 asubuhi. Katika ndimi, Kiingereza, Kihispania, na lugha isiyoeleweka.
Kihispania:
Oo ni aibu ilioje, Oo ni aibu ilioje, vitu vilivyopo vitakuwa, ni aibu gani, ni aibu gani.
Kiingereza:
Ndiyo, ndiyo, Raymond, vitu vya Mbinguni vitakuwapo kwa wakati uliopangwa. Tazameni, sikilizeni, kutakuwapo na boti. Hiyo boti itakuja kusafiri kwa kupitia mlango wa bandari uitwa "the Golden Gate". Mnisikilize, hiyo boti itakuja kusafiri kupitia mlango wa bandari uitwao "the Golden Gate" (ulioko Kalifonia Amerika), Wakati na saa umekwisha wekwa. (Lugha isiyoeleweka?)
Kiingereza:
Nitawatuma watu wafaao wakati utakapo fika. Watawasiliana na wenyeji wa Mbinguni, kwani saa na wakati umewadia. Ujumbe niliokuwa nikinena kwa maelfu ya miaka, hautasimamishwa. Hakuna chochote katika ulimwengu kinaweza kuzuia ninachosema, kwani zana kwa ajili ya uwanja wa mapambano ziko tayari, zana za adui ziko tayari na matayarisho ya zana za wenyeji wa Mbinguni yapo tayari.
Ni wale tu walio na masikio na macho yakuona ndio watakao ona. Tatizo ni kuwa ninyi hamna tafakari ya ukweli wa ulimwengu wa Kiroho. Ninyi hamnayo njia ya kidunia ya kupima hali halisi ya ulimwengu wa kiroho bila kusoma Biblia, na kisha inakuwa vigumu kutafakari. Lakini hata hivyo hali halisi bado ni halisi sana, na wakati siku ya Mekka itakapofika, dunia itakuja kustushwa. Kwani mlionywa, nakuonywa, na kuonywa, lakini yote mnayofanya nikufunika macho yenu, nakufunika masikio yenu.
Ninyi mawe, mnaua, mnawadhulumu, Manabii Wangu, kwa hiyo huruma inafikia kikomo. Siku ya kuitwa, siku ya kutoa hesabu, siku ya hukumu imefika. Kwa hiyo ninyi hamna visingizio, kwa hiyo ninyi hamna visingizio, na hamwezi kupata njia ya kukwepa hatia siku ile ya hukumu. Kwani najua kilichoko mioyoni mwenu: Udanganyifu, Uwongo, machukizo, kwa Bwana Mwokozi wenu.
Mwokozi wenu Yesu Kristo atakuja kuleta Jeshi la Mbinguni, wakati na saa msiyo tarajia. Na mtakuja kujua kuwa Mimi ndimi Baba wa kila kitu. Na kwenda kuweka kila kitu sawa kwa sababu mambo yameenda kwa muda mrefu wa kutosha. Nimeweka siku na saa, na wewe na Watu Wangu hamtakuwa na udhuru. Ninyi Wakristo, Ninyi msio Wakristu, Ninyi Watu wa Baali, ninyi watu wote mtafahamu kuwa Bwana wa Mabwana, Mfalme wa Wafalme, na hakuna hata mmoja na hakuna hata mmoja ataepuka Upanga wa hasira Yangu.
Kwani siku imefika, jua linaanza kuchomoza, mwezi unatumbukia na mtaona. Mtaona utukufu wa Baba, wa Mwana na Roho Mtakatifu. Watu wenye kumbukumbu/akili ndogo hukumbuka/huona vitu vidogo, lakini Nguvu na Utukufu wa Mungu siyo kitu ambacho wewe unaweza kukitania, au kucheza nacho, au kuipa jina la kufaa theologia yako. Watu, Wanatheologia, ambao wanadhania kuwa wanafahamu yote, watakuja kushangaa sana. Kwani wanafuata, wengi wao, njia za Wayahudi katika siku za zamani, lakini na iwe hivyo. Niliwaonya, Niliwapenda, Niliwaponya, na walikuwa vipofu, na viziwi.
Kwani siku ya Mekka itakuwa siku ya furaha ya Milele Mbinguni. Kwani Malaika wa Mbinguni wamekuwa wakiingojea siku hiyo, wako tayari, wamekwisha jitayarisha kwa siku hiyo tukufu ya mwisho katika ulimwengu huu, siku ambayo nitawaleta Watoto Wangu nyumbani. Wananingoja kwa hamu. Wanaingojea kwa hamu saa ya tarumbeta, lakini bado kidogo kuna muda, bado unanafas. Kwa hiyo sikiliza Manabii, msikilizeni Roho Mtakatifu kwa Moyo, Moyo wa Nafsi yako, na wala siyo kwa Akili yako, kwani akili yako inaweza kukuhadaa.
Huyu ni Baba yako. Baba wa Mbingu na Dunia, wa kila kitu kilichokuwapo, kilichoko na kitakacho kuwapo. Pamoja na upendo midomoni Mwangu, Nawataka mikononi Mwangu. Nawataka kuwapakata. Nataka kuwabusu, Nataka kuwalinda. Nataka kuwapenda lakini inabidi mje Kwangu kwa hiari yenu. Lazima mje kwa hiari yenu. Ni uamuzi ambao itawabidi kujifanyia wenyewe. Sintawa washurutisha ninyi. Sintafanya chochote, ila kuwa onyeni na kuwapendeni mpaka siku ile niliyoiandaa, laiti tu mungelifahamu, laiti kama mngweweza kuitafakari, kinachotendeka katika Milki za Mbingu. Shetani yule adui wenu mkuu, ameogopa kabisa. Anajua kinachokuja, lakini anahasira. Anahasira. Kwa sababu anajua hatima yake. Na atajaribu kwa kadri ya uwezo wake wote muende chini pamoja naye. Kwa hiyo sikilizeni, Kwahiyo ombeni, kwa hiyo muone kilicho cha haki na mjutie dhambi zetu. Huyu ni Baba yenu na ujumbe wa Upende. Kwa hiyo naiwe hivyo. Naiwe hivyo.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )