Sauti 56

Sehemu hii ya sauti 56 imehaririwa (kufupishwa) na kuwa ya kama dakika 5:56 au (714 KB) kutoka kwenye habari yenyewe ya kwenye mkanda wangu mdogo wa kurekodia Kwanza fanya majaribio kutoka: sound.htm kuona kama mitambo yako ya kutoa sauti inafanya kazi sawasawa. Kuna sauti ya kukwaruza kwenye kanda au faili hii. Unabii huu uko katika lugha ya Kiingereza, Kihispania na lugha isiyoeleweka. Soma ujumbe wa hapa chini wakati unaposikiliza mkanda huu wote ili uweze kupata matokeo mazuri.

Ili kusikiliza mkanda huu unahitajika uwe na Kadi ya sauti, na Modamu ya 14.4 au 28.8 kwenye komputa yako. Ili kupata "the RealAudio Player" ya kusikilizia mkanda huu kama haipo kwenye komputa yako, bonyeza kwenye kitufe hiki.
 

56. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 19 Mei 1992 saa 7:15 mchana Jumanne katika lugha, Kiingereza,na lugha isiyoeleweka.

Safina! Safina! Safina! (lugha isiyoeleweka.)

Kiingereza:

Ee Bwana Wangu. Ee Bwana Wangu. Ee Bwana Wangu.

Mimi Ndimi, Mimi Ndimi, Mimi Ndimi.

Maana Kondoo Dume, Beberu, na Kahaba, watakuja pamoja. Beberu atakuwa mnyama ambaye atakuwa sababu ya kuanguka kwa adui. Kwani Beberu atajisikia yuko salama kwa wakati kisha ataanguka.

Kahaba atawatia utumwani, atateka mioyo ya watu wasio na hatia. Kahaba atakuja wa mwisho. Kwa maana atawashawishi wenye nguvu, wenye uwezo watu halali kwani yeye ni chukizo kwa Wateule. Kwa maana atawalaghai Viongozi wa Mataifa. Atawadanganya Viongozi wa Dunia. Atawaleta chini kwenye shimo la Jehanamu, na pale atatupwa yeye pamoja na wafuasi wake wote.

Kwa maana yeye ni mchawi wa siri apotoshaye, na aelekezaye vibaya mtu yeyote na kwa wakati wowote na kwa sababu yeyote. Yeye ni mchawi mpweke, apendaye kusifiwa na apendaye kuheshimiwa, lakini wale wamfuatao watatupwa katika shimo la Jehanamu. Kwa siku zote zilizoko Mbinguni, jihadharini, jihadharini na mchawi ambaye atawategeni kwa hila kwa milele yote.

Kutakuwa na jeshi litakalo gawanyika katika vifungu vitatu ambayo litaivamia nchi Takatifu kutoka Mashariki, Kaskazini na kutoka Kusini. Uvamizi utafanyika wakati utawala wa Mbwa Mwitu, kwa maana Mbwa Mwitu ni mnyama mjanja. Jitayarisheni, jitayarisheni, muwe tayari kwa maana Mbwa mwitu na Mwanakondoo watakutana kwa wakati uluopangwa.

Lini na kwa namna gani ni Mimi tu ndio ninayefahamu, Kwa maana Yehova anajua yote, kwani Yehova atawaonya kabla tarumbela haijalia kutoka Mbinguni na Duniani. Kwa maana ninyi ni Watoto Wangu na Ninawapenda.

Jihadhari na Jeshi lililogawanyika katika vifungu Vitatu. Kila kikundi kina uwezo wa kuchoma kama ng’e, kila kikundi kinaweza kutafuna kama simba, kila kikundi kinaweza kuharibu kwa uharibifu ambao dunia haijawahi kuufahamu kabla. Muwe imara, Muwe imara, Muwe Waaminifu, Muwe na imani, mtafuteni Yesu, kwa maana Yeye haonekani, lakini kwa wakati wowote na kwa mahali popote Yeye atakuwa pale na kwa saa hiyo hiyo niliyo chagua, kwa kimbilio, kwa ajili ya wale wanaomtafuta.

Usicheke wala usikenulie Jina la Yesu, kwa maana unakuja wakati ambako utakula maneno yako hayo. Kwa maana njia ya kwenda kwenye usalama, njia ya kuja Kwangu inapita kwenye Jina hilo la Yesu wa Nazareti, Jina lililo Takatifu sana katika Ulimwengu. Kumbukeni hayo. Kumbukeni hayo! Kwa maana kwa wale wanao simama pale na kukenulia Jina hilo itawabidi mfanye zaidi ya kula viburi, majigambo na ubinafsi wenu. Kwa maana itakapowajieni mtakuwa mmechelewa sana.

Msijiamini wenyewe, kwa maana kujiamini kwenu wenyewe kutawapatia shimo la Jehanamu, huo ni uhakika. Mimi Yehova nawahakikishieni, lakini mkimwamini Mtu na Mungu, ambaye ni Mwanangu aliyesulubiwa kwa ajili yenu, mtapata utulivu na amani mnayohitaji wakati huo wa dhiki Kuu. Wengine wenu mnaosoma, au kusikia au kuona ujumbe huu, utaingia kwenye akili yenu lakini utatoka nje kwenye hewa, bila kuacha aina yeyote ya maarifa ndani ya miili yenu. Hao ndio wale ambao machozi Yangu yanatoka. Kwa sababu hao wamepotea na watakula majigambo yao na majivuno yao milele. Na kwa wakati huu ninyi hamjui ukweli wa milele ni nini. Hivyo mjifurahishe, baada ya muda mfupi namba yenu itakuwa imetimia. Kumbukeni hilo, lakini pamoja na hayo bado Mimi nawapenda ninyi.

Huyu ni Yehova, na Mwanangu Yesu Kristu, na Roho Mtakatifu. Tunafungua mikono Yetu, Tunawakaribisheni, lakini inawabidi mfanye uamuzi ninyi wenyewe. Kwa vyovyote vile nilichokiweka kwenye mwendo hakiwezi kuzuilika. Kwa maana Huyu ni Mungu wenu, Mtengenezaji, Muumbaji, wa Ulimwengu, Yehova. Fikiri! Fikiri! Watoto Wangu fikirini kuhusu nini mnafanya. Tubuni! Tubuni! Nami nitawaokoeni, lakini ni lazima mfanye wenyewe. Safina inaendelea kujengwa sekunde hii.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.