60. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 25 Mai 1992 saa 5:31 asubuhi katika lugha ya Kiingereza.
Kulitokea hasa nini katika miaka mingi iliyopita? Kulikuwa na wakati, ambao hali ya mioyo ya watu wa dunia ilikuwa ya upendo na inayopendeza, lakini shetani alikuja akaibadilisha. Na sasa hali ya miyo ya watu imekuwa ya wendawazimu, katili na ambayo haitawaliki kabisa kabisa. Lazima muelewe kuwa inabidi mambo ya fanyike katika mpangilio unaotakiwa. Vitu lazima vitokee katika mpangilio, vingine vitangulie kabla vingine havija tokea, katika mpangilio ulioagizwa na vitekelezwe na vitimie. Ni mipango niliyoweka, katika dunia haijawa, kabla haijaundwa kwa Neno langu niliolisema. Na Neno Langu nililolinena liliumba kila kitu.
Kwahiyo ili uelewe vitu fulani fulani jinsi vilivyo tokea inabidi muelewe kuhusu Neno Langu Nililonena. Kwahiyo kama unahitaji kuelewa fomula ya jinsi ulimwengu ulivyo umbwa, inabidi, msome Neno Langu lililonenwa. Kwahiyo mnisikilize na mjifunze, kwani Ninalonena ni yaliyonyooka, na ni Ukweli. Kwani inakuja wakati ambako mtahitaji huo Ukweli, na huo Ukweli ni Neno la Mungu, na Neno la Mungu ni Yehova, pamoja na Mwana na Roho Mtakatifu. Bila hilo Neno, mtakuwa mmepotea milele na milele yote.
Kwa hiyo inabidi mjue, msikilize, muangalie, mtambue, mpime kwa njia ya kudhamanisha isiyo ya kidunia. Njia ya udhamanisho itokayo katika Mdomo wa Mungu, Njia ya udhamanisho ambayo ni Mungu, Yehova. Yehova amekuwapo siku zote. Yehova ni Mungu wa kila kitu. Yehova ni Mumbaji wa kila kitu, lakini inabidi mlielewe Neno, na Neno ni Mungu. Inakubidi uone, na kusoma Biblia. Soma Biblia. Ni Neno Langu nililolinena. Ni ukweli kabisa. Ni ukweli unaoongoza mbegu, mbegu ilienda njia ambayo ni kinyume na Neno Langu, Yehova.
Kwa hiyo, ili mbegu iweze kuokoka na kuendelea kuwako, inabidi irudi kwenye njia ya Neno. Hakuna njia nyingine ya mbegu kuendelea kuishi. Kwani bila Neno mbegu itakuwa imepotea milele. Amani na utulivu, kwa wote wanaosikia Neno la Mungu. Kwani Neno la Mungu ni Ukweli na uadilifu. Amani na iwe Duniani. Amani na iwe nanyi. Kwani Neno langu haliterudi tupu. Kwani Mimi ni ukweli, uadilifu, na ni Mungu wenu.
Kwahiyo sikilizeni viziri, na mtii, kwani muda umefika ule niliosema katika Neno langu. Dunia, Ulimwengu, kila kitu kilichokuja katika uwepo kwa njia ya Neno langu kitasahihishwa hadi kiwe sawa na njia ile iliyonenwa.
Kwa hiyo sikilizeni, Msikie Maneno Yangu kwani wakati umefika wa Mimi kutekeleza yale niliyonena kabla ninyi hamjazaliwa. Kwa maana muda huo umefika! Na ni lazima Msikilize, kwani kama hamtasikiliza mtakuwa sehemu kubwa ya ardhi haribifu itakayo undwa baada ya hapo, kwa ajili vitu visivyofaa, visivyo adilifu, na vilivyovichafu machoni mwa Yehova. Kwa hiyo mjihadhari, muwe wasafi, waadilifu, wema waaminifu, wakweli na mjitenge na uovu. Kwani ubaya utatawala ardhi ya uharibifu mara mmoja na daima. Mahali ambako humtaweza kamwe kupawazia. Kwa kweli nawapendani ninyi.
Kwa hiyo sikilizeni na mjihadhari na nabii wa uwongo ambaye atawajia hivi karibuni. Pimeni, tambueni kwani atawadanganya wengi walio waadilifu na wasio waadilifu wa Watoto wa Mungu. Kwani Nabii wa Uwongo atakwenda kufanya kilicho elezwa katika Biblia kabla ninyi hamjazaliwa. Kwahiyo sikilizeni, msikilizeni Baba yenu wa Mbinguni kwa maana muda umefika, saa imechaguliwa, siku na mwezi inakuja kwa kasi kubwa. Kwa hiyo Watoto Wangu mmeambiwa, mmeonywa, msifanye kama dunia inavyofanya. Kwa maana mtapata ardhi ya uharibifu kwa milele yote kama mtafanya kama dunia ifanyavyo. Kwa maana Baba yenu anawapenda ninyi, na anataka kuwaongoza kwenye Amani na utulivu milele, lakini inabidi mfanye ninyi kwa hiari yenu wenyewe. Kwa maana nitawakubali wale tu wanaotaka kuwa wazuri na wanyofu, wao wenyewe na kwa hiari yao. Kwa maana Mimi siyo Mungu ambaye atawalazimisha kuja Kwangu, kwani upendo haulazimishi, upendo haudai, upendo ni kutoa upendo.
Kwa hiyo Watoto Wangu mjihadhari, sikilizeni maneno yangu. Ombeni. Mwombeni Mwanangu, Yesu kristu wa Nazareti, Atawaonyesheeni njia, Atawaongoza, Yeye ni Mfalme wenu, Yeye ni Mwokozi wenu, Yeye ni Mwanangu, Yeye ni Mkurugenzi, Yeye ni Mtendaji, Yeye ni Msimamiza wa utekelezaji wa Neno langu. Kwa hiyo tegeni masikio na msikilize, kwani wakati umefika, saa inakaribia kwa kasi kubwa.
Kwa maana huyu ni Baba yenu, Baba yenu wa Mbinguni, Yehova Mungu wenu. Mungu wenu wa leo, wa jana na wa kesho. Amani na iwe kwenu Watoto Wangu Wapendwa, kwa maana muda umefika.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )