Sauti 68

Sehemu hii ya sauti 68 imehaririwa (kufupishwa) na kuwa ya dakika 10:13 (1.2 MB) kutoka dakika 20 ya kwenye habari yenyewe ya kwenye mkanda wangu mdogo wa kurekodia. Kwanza fanya majaribio kutoka: sound.htm kuona kama mitambo yako ya kutoa sauti inafanya kazi sawasawa. Kuna sauti ya kukwaruza kwenye kanda au faili hii. Unabii huu uko katika lugha ya Kiingereza, Kihispania na Lugha isiyoeleweka. Soma ujumbe wa hapa nchini wakati unaposikiliza mkanda huu wote iliuweze kupata matokeo mazuri.

Ilikusikiliza mkanda huu unahitajika uwe na Kadi ya sauti, na Modamu ya 14.4 au 28.8 kwenye komputa yako. Ili kupata "the RealAudio Player" ya kusikilizia mkanda huu kama haipo kwenye komputa yako, bonyeza kwenye kitufe hiki.
 

 

68. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 28 Mei 1992 Alhamisi saa 8:15 usiku katika lugha, Kihispania, Kiingereza, lugha isiyoeleweka.

Kihispania:

Mbegu, mbegu...

Lugha isiyoeleweka?

Kihispania:

Mbegu, mbegu..

Lugha isiyoeleweka?

Yesu.

Kiingereza:

Nataka ninyi msikilize, mchunguze, mhukumu, mchunguze na mchambue kila Unabii. Kuchambua na kuchunguza kila Unabii, kwa maana Neno la Mungu Yehova ni Ukweli, ni hakika bila mawaa. Nini Neno la Mungu. Unabii siyo kitu cha kuchezea, kwa ajili ya kujifurahisha, kwa ajili ya kujisikia. Siyo cha nyakati mpya. Siyo cha kuangalia nyakati katika jiwe kama kioo. Siyo cha kutatua matatizo ya Binadamu kwa kusoma na kujifunza elimu ya kufikiria mambo mazuri, tabia ya Binadamu.

Haya yote ni mbinu ndogo ya kupindisha ukweli na ukweli pekee, ambao ni Neno la Mungu Yehova. Kwa maana mashirika au vikundi hivi vya shule za kufikiria juu ya nini kilicho sawa na nini kisicho sawa na kuhusu maneno na maana ya maneno yote ni vya uchoyo na ulafi. Kwa maana siku ile itakapofika ambayo iko mbele yenu na bila kujua kuwa iko mbele yenu, siku ya hukumu ndipo mtakapojua kuwa mlikuwa mnamtegemea mungu wa uwongo. Kwa maana Mungu wa Ulimwengu, Mungu wa kila kitu kilichopo na kitakacho kuwapo ni Yehova na Mwanawe Yesu Kristu wa Nazareti na Roho Mtakatifu.

Kumbuka mambo hayo kufikiri kuwa mambo ni shwari (positive thinking) itawapeleka Jehanamu. Kumbukeni Neno hilo, kwa maana nawaambia mara mtakapopapata mahali hapo kila kitu kuhusu kufikiri kuwa mambo yataenda sawa (positive thinking), mawazo (theory) kuhusu maisha ya kisasa yote yamefungwa katika neno mmoja tu iitwayo Jehanamu. Hamtapata amani. Hamtapata chochote ila tu kuguna na kusaga meno kwa milele yote.

Kwa hiyo, hili ni onyo kutoka kwa Mungu Jehova, Muumbaji wa Ulimwengu, Muumbaji wa Binadamu. Kama utamruhusu Shetani akudanganye, utakuwa unastahili uishi naye. Kwa maana nimewaonya ninyi niliwapendeni, na ninyi badala yake mlinigeuzia kisogo; na mkaondoka nakuwaendea vijimiungu yenu; kwa miungu ya mawe; kwa miungu ya maneno ya uwongo, kwa miungu ya manabii wa uwongo; kwa miungu ya kila kitu kilicho chukizo kwa Jina la Yehova. Kwa maana Yehova hata ruhusu Jina lake linajisiwe kwa njia na hali namna yeyote ile. Kwa maana kila kilicho chema, kilicho cha haki kilichokuwepo, kilichopo, na kitakachokuwepo daima ni Mungu wako, Yesu, Roho Mtakatifu na Mimi Baba.

Kwani wakati mnapocheza na Shetani mnaishi na shetani. Sitakuwa na huruma ya aina yoyote kwa wale watakaokuwa na Mhuri wa Mnyama. Sitakuwa na huruma na ninyi mnaoangalia nyota, au kupiga ramli na wale wanao angali mambo ya baadaye kwa njia ya elimu ya angani, ninyi Manajimu. Angalieni kama hizo alama za angani, jinsi Mwezi ulivyokaa au jua zitawaokoa na hasira zangu.

Naongea nanyi kwa ukali kama Baba kwa maana ninachosema kitatimia, kwa maana hakuna mtu wala mtaalam wa unajimu, wala mtaalamu wa kupiga ramli au wa elimu ya kufikiria kuwa mambo ni shwari (positive thinkers) au wataalamu wa elimu ya kutumia tufe au chochote ambacho mnakiamini na kukiabudi iwe ni gari yako au boti, au nyumba, au kazi, au mke wako, au mwanao, hakuna chochote kati ya hayo kitawaokoa. Wokovu pekee unapatikana kutoka kwa Yesu Kristu wa Nazareti, Mwanangu wa pekee.

Ana mamlaka, Mamlaka kamili juu ya Wanadamu wote. Kila goti, kila ulimu utapigwa na kukiri na kuungama kuwa Yesu Kristu wa Nazareti ni Mfalme wa Wafalme, Bwana wa Mabwana, na hicho ndicho pekee kilichopo. Hakuna cha labda, hakuna cha sikujua, hakuna cha nasikitika nisamehe, kwa maana siku ile na wakati ule utakwenda pale ambako Mwanangu anataka uende.

Kwa hiyo chochote kimkufurucho Baba, kinamkufuru Mwana na Roho Mtakatifu hicho hakitaruhusiwa kwa hali yeyote au njia yeyote au kwa sura yeyote. Ninyi watenda maovu mtapata Uovu kwa Uovu na haitajalisha cheo chako cha kazi, elimu yako, wadhifa wako wa kuzaliwa, rangi ya ngozi yako, yoyote hayajalishwi ila kilichoko moyoni mwako. Na mwenendo wako ulikuaje wakati wa kumwabudu Mungu wa kweli, Yesu Kristu, Roho Mtakatifu, na Mimi Baba yako.

Sitakuambia kwa uzuri. Sitakwambia Maneno mazuri. Sitakwambia ya kuwa kila kitu kitakuwa kama wewe unavyotaka kusikia kwa sababu unataka kama unavyotaka. Kwa sababu itakuwa Kama Ninavyotaka, na huo ndio ukweli, yaani ukweli wote. Kwa maana Mungu Wenu ni ukweli. Yeye ni Upendo, Yeye ni Haki. Kama utatubu na unamaanisha kabisa hiyo toba na kama utatubu kwa Nafsi yako yote na akili yako yote na kunigeukia Mimi sasa hivi sekunde hii, Mimi nitasamehe yote na kila kitu ambacho umewahi kufanya kuanzia siku ile ulipotungwa mimba.

Kwa maana nataka utiifu kamili kwa Mwanangu, Upendo kamili. Sifa zote na Utukufu wote zimwendee Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Miungu yenu haina faida yoyote zaidi ya kuwapatieni bonde la Kifo la Milele, Shimoni. (Lugha isiyo eleweka?)

Kwa hiyo kumbukeni nilichosema ninyi mliowarefu, ninyi mliowafupi, ninyi mliowanene, ninyi mlio wakondefu, ninyi wanaume, na wanawake. Nawaangalia kwa makini, kila sekunde ya kila siku Macho Yangu yako pale kwa Upendo na Huruma. Lakini msidanganywe na macho hayo ya Upendo na Huruma kwa maana Hasira ya Mungu siyo kitu cha kucheza nacho.

Muwasikilize wale Manabii wanaowaambia kuwa mgeukieni Yesu, mgeukieni Yehova, mgeukieni Roho Mtakatifu, hao ni Manabii niliwatuma kuwajulisheni, Ukweli na Haki. Kwani wao ni jibu ya hiyo dini yenu ya nyakati mpya "new age Religion". Kwa maana dini yenu hiyo ya Nyakati mpya siyo chochote, ni kanisa la Shetani. Na Shetani yuko karibu kufungwa na kutupwa Jehanamu. Kama unataka kuwa pamoja na marafiki, basi usitubu uungane na marafiki zako pamoja na Viongozi wa kanisa lako Jehanamu. Jehanamu ni mahali pa mateso ya Milele, lakini kumbuka japo nasikika kuwa mkali, na bahili lakini una nafasi Kwangu.

Tubuni na wapendeni jirani zenu, toeni Utukufu na Sifa kwa Yehova, Yesu Kristu, na Roho Mtakatifu. Nirahisi sana, lakini Mimi nasoma Mioyo na siyo midomo yenu, kwani midomo itawapatia shimo. Kwa maana wale wanaoongea kwa ndimi zilizogawanyika watapata Shimo kwa maana huwezi kumdanganya Mungu, Yehova. Huwezi kujificha kutoka kwa Yehova.

Kwa maana hakuna katika Ulimwengu ambacho kimeumbwa bila Neno Langu Nililolinena. Ni vigumu kwa ninyi kuelewa hayo, lakini ni ukweli, kama ninyi mlio na bahati mtafika Mbinguni, tutazungumzia hayo nanyi pale. Na tutaimba na kucheza pale na kwa kweli pale tutafahamiana vizuri zaidi, lakini uamuzi ni wako, ni juu yako kufanya wewe mwenyewe. Mimi sitakushawishi uende kushoto au kulia. Nitakuonya tuu, Nitawatuma Manabii Wangu na nitangoja, uamuzi ni wako. Kwa maana Mimi ni Mungu wa Maisha ya milele, pamoja na Mwanangu, Yesu Kristu na Roho Mtakatifu. Na amani na upendo wa Jirani yako ikue ndani ya mioyo yenu milele. Watoto Wangu nasema haya yote kwa upendo na huba kwa maana najua mioyo yenu. Kwaherini Wakristu Wangu wapya. Nawapenda.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.