Sehemu hii ya sauti 69 imehaririwa (kufupishwa) na kuwa ya dakika 30 (3.7 MB) kutoka kwenye habari yenyewe ya kwenye mkanda wangu mdogo wa kurekodia. Kwanza fanya majaribio kutoka: sound.htm kuona kama mitambo yako ya kutoa sauti inafanya kazi sawasawa. Kuna sauti ya kukwaruza kwenye kanda au faili hii. Unabii huu uko katika lugha ya Kiingereza. Soma ujumbe wa hapa nchini wakati unaposikiliza mkanda huu wote iliuweze kupata matokeo mazuri.
Ilikusikiliza mkanda huu unahitajika uwe na Kadi ya sauti, na Modamu ya 14.4
au 28.8 kwenye komputa yako. Ili kupata "the RealAudio Player" ya kusikilizia
mkanda huu kama haipo kwenye komputa yako, bonyeza kwenye kitufe hiki.
69. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 29 Mei 1992 saa 5:11 asubuhi siku ya Ijumaa katika lugha ya Kiingereza.
Nakupenda, mambo yanakwenda vizuri sasa hivi, kumbuka kutakuwa na wakati wa taabu, majaribu kiasi ambacho hutaweza kuelewa, lakini kumbuka, siku inakaribia ambayo kila kitu kitafikia ukomo wake. Sheria ile iliyoelezwa kwenye Biblia, kuhusu nyakati za mwisho itakuja kutimizwa kama ilivyoandikwa katika Biblia.
Kwani saa na siku inakaribia kwa kasi kubwa. Kutambua kuwa dunia yenu itakuja kubadilika itawachanganya wengi wenu kwani mmezama katika shughuli zenu za kila siku, lakini yote hayo yanakuja kukoma.
Vita vikuu vya mwisho vitatokea katika nyakati za maisha yenu. Kwa hiyo mjitayarishe, muwe imara fanyeni mazoezi ya kutekeleza Neno la Mungu katika maisha yenu ya kila siku. Fanyeni mazoezi ya kufuata Sheria na taratibu ambazo zimeelezwa katika Biblia. Mwangalieni Yesu Kristu wa Nazareti, Mwangalieni Roho Mtakatifu ili kupata Mwongozo, Niangalieni Mimi kwa kusikiliza Maombi yenu kwani siku za Mnyama zimewadia.
Siku za kutawalishwa kwake itaanza wakati ule Nyigu na kombamwiko/mende watakapopambana. Matokeo ya mapambano yao hayo yataweka mamlaka na nguvu za Mnyama ambazo zitaanza mwanzo wa mwisho. Wengi watachanganyikiwa kwa maana vitaanza ghafla sana. Wale watakaookolewa ni wale tu watakao Wasikiliza Manabii, na Maneno maadilifu ya Yesu Kristu, Yehova na Roho Mtakatifu.
Kwa maana mtakachokiona katika siku za hivi karibuni ni mwanzo wa mwisho. Mwisho wa wale ambao siyo Wakristu na wasiomwamini Mwanangu ya kuwa alifia Msalabani kwa ajili yao. Lakini kwa wale wanaoamini itakuwa mwanzo wa maisha ya amani na furaha ya Milele Mbinguni. Najua kuwa haya maneno kwenu yanasikika kama ahadi isiyo ya ukweli, Maneno yasiyo na Mamlaka, lakini huo ni Ukweli.
Kwa hiyo kumbukeni kuwa mwisho huo utakapofika kila mtu aliyewahi kuishi duniani itabidi atoe hesabu ya maisha yake yote. Yakuhusu aliishije na Mungu wake na Ndugu zake wa Kiume na wa Kike kwa maana hakuna kilichoumbwa kwa ajili uovu. Lakini shetani aliiharibu ile Mbegu.
Sasa siku ya Hukumu imewadia, iko karibu kabisa kiasi cha kuwa sawa na ratiba ya Maisha yenu. Kwa maana wengine wenu watamfuata Shetani hadi mwisho, mpaka mahali alipotayarishiwa. Wale wanaolikufuru Jina Langu, Jina la Mwanangu na la Roho Mtakatifu. Na kwa wale wengine wanaomfuata Mwanangu na ambao wamekufa na walioteswa hadi kifo, na wale walioshurutishwa kufa kwa njaa kwa ajili ya Mwanangu, na walioteswa kwa miaka mingi hii iliyopita kwa njia ya magonjwa, kwa njia ya mateso kutoka kwa jirani zao, mateso kutoka serikalini kutoka kila upande ambao Shetani amewagawia, hao watakwenda kuishi Milele na Milele.
Nawajua wako wale wengine wanaosikiliza Nabii huyu Mdogo watasema "Tazama kuna Mwenda wazimu mwingine anazungumzia kuhusu mwisho wa nyakati." Lakini hiyo ni sawa kwani Tunajua huo utakuwa mwisho wao. Kwa hiyo waache wasema wanachotaka kusema. Ila kwa ninyi, ambao mnasikiliza na mnaoisoma na mnaotafuta majibu kwa ajili ya Wokovu, fungueni Biblia na muisome.
Jifunzeni kuhusu Mfalme wenu, Bwana wa Mabwana, Mfalme wa Wafalme na mtamwona. Na mtaongea Naye kwa maana mtakuwa Mbinguni milele. Ingawa ninahisi hakuna mahali kama pale, lakini kuweni na maneno yangu maana Mungu ni wa ukweli.Ukweli ni kwamba kuna Mbingu: Ni pa ajabu, Pazuri sana ni pa milele. Akili zenu hazikuumbwa kuelewa raha furaha kubwa namna hiyo wala uzuri huo wala uadilifu wa aina hiyo.
Kwa sababu umekuzwa ndani ya ulimwengu wenye dhambi umeingizwa kwenye dhambi. Je, unawezaje kuhukumu jambo usilolijua? Ni zaidi ya uwezo wako maana kwa asili umekuwa na dhambi hivyo mkosefu hawezi kuhukumu haki. Hivyo hapo ndipo imani inapochukua nafasi yake, lazima tuamini Unabii na lazima tuamini kwenye sheria ya Mungu wetu Yehova "Biblia", Roho Mtakatifu atakuongoza, atakuelekeza, atakuonyesha lakini lazima tujizatiti wenyewe na lazima umwamini Mungu Wako.
Mtapata majaribu na mateso lakini tupo vitani. Lakini vita vinaenda kukoma. Nakama wewe ni mmoja wa Wanangu, kondoo Wangu wa Kiume, mmekwisha vishinda. Yote Ninayotaka mfanye nimuwaambie Ndugu zenu wengine wa kike na wa kiume, wale ambao hawajui ukweli bado. Mshirikishane, tawanyeni Neno kwa maana jinsi mnavyoimarisha Mwili wa Yesu Kristu jinsi hiyo hiyo mtakavyopata ushirikiano na misaada ninyi kwa ninyi. Jinsi mnavyo kuwa imara ni kwa jinsi hiyo hiyo mtakavyo kuwa na unafuu wa taabu yenu na masumbuko yenu mtakayopata katika nyakati hizo za dhiki kuu. Kwa maana vita hivyo vya mwisho vitamgusa kila mtu kwa njia ambayo hamtaweza hata kuiwazia, na wakati umwekwishaanza.
Kwa hiyo yasikilizeni maneno ya Baba yenu Mpendwa. Mtakuwa mnapata ujumbe kutoka kwa Manabii. Kama utaingia ndani ya Biblia nakuijifunza kwa undani kutoka Moyoni mwako, Nitaongea nawe Mimi mwenyewe. Nahutakuwa na haja ya kuhangaika sana unaposikia Unabii. Kwa sababu kama kweli wewe ni Kondoo mwema wa kiume na wa kike Mimi mwenyewe naweza hata kuongea nawe moja kwa moja, lakini Nataka wale tu wenye mioyo misafi, akili safi na tabia safi. Wakati mwingine ni ngumu kufikia hatua hiyo lakini mara unapojaribu, unapoifanyia kazi au unapoifanyia mazoezi siyo ngumu kiasi hicho unachodhania.
Mmezoea mno njia rahisi, ile njia nyingine ambayo inakupeleka kwenye shimo la Jehanamu. Msiwasikilize wale wanao wa shawishi kufanya maovu kwa ajili ya Mbingu. Kwa kweli inawabidi kuiamini Neno Langu kwanza, inabidi Mniamini hiyo ni hatua ya kwanza. Nawapendeni Nitawalindeni hata ikitokea nini Mimi niko pale karibu nanyi hata kama kwa wakati fulani mtajisikia kuwa mkopeke yenu. Hamta kuwa peke yenu ilimradi mtaweka malengo yenu kwa Yesu Kristu wa Nazareti. Atawaongoza Kwangu kwa kupita nguvu za Roho Mtakatifu. Sisi sote tutakwenda kufunga ukurasa huu wa mwisho wa maisha mafupi ya Sayari hii ndogo na kuifunga.
Kwa hiyo Watoto Wangu wafundisheni watoto wenu wawatiini, na kuwaaminini na ninyi mjifundishe kunitii Mimi na kuniamini na kisha Sisi sote tutakuwa Familia mmoja kubwa na yenye furaha. Leteni Mwili wa Kristu pamoja, kwani kunapokuwapo na umoja kunakuwa na nguvu. Mezeni ile kiburi, ubinafsi wenu kwani Mtoto wa Kristu hana kiburi wala ubinafsi. Wao ni waamini wa kilicho cha haki na cha ukweli, na wanajua jinsi ya kujinyenyekesha wenyewe mbele ya Bwana na Mwokozi wao na wao kwa wao. Inasikika kuwa maneno marahisi lakini dunia ni dhalimu kiasi ambocho kama huna majivuno au huna majigambo ya ubinafsi unajisikia kama wewe wala siyo binadamu.
Nawapendeni kwa Moyo Wangu wote, inabidi mniamini. Mjiimarishe wenyewe na mtii sheria ya Yesu Kristu. Kutakuja siku na wakati ambapo mnyama na wafuasi wake watawateseni ninyi. Atafanya kila awezalo na kila kilichoko kwenye uwezo wake awaangamize ninyi kiakili, kimwili, na kiroho kwa maana siku za Mnyama zimewadia. Lakini kumbukeni kuwa nguvu zote na Utukufu na Sifa ziende kwa Yehova, Yesu Kristu na Roho Mtakatifu.
Kwa maana nambari ya yule Mnyama itawekwa kwa wanyonge, kwa wenye dhambi. USICHUKUE, Nitairudia Tena! USIICHUKUE ALAMA YA MNYAMA. Kwani kama utaiuchukua, hutapata wokovu. Nitairudia tena. USIICHUKUE ALAMA YA MNYAMA. Bila kujalia itakuwa ngumu kiasi gani, bila kujali itakuwa rahisi kiasi gani, kama unathamini, namaanisha kama unajali maisha yako ya baadaye, USICHUKUE ALAMA YA MNYAMA, Kwa maana utatupwa kwenye BONDE LA KIFO KWA MILELE YOTE.
Hiyo itakuwa KUFURU KUU kushinda yote ambayo utawahi kumfanyia Bwana Yehova, na MIMI KAMWE SITAKAA KUKUSAMEHE KWA HILO. Wakati alama ya Mnyama itakapoanza kutolewa wewe kimbia sana na ujifiche, fanya uwezalo kufanya, ili mradi USICHUKUE ALAMA YA HUYO MNYAMA. Nadhani nimeieleza ya kutosha. Nadhani nimejaribu kuifanya iwe rahisi, wazi na mmoja kwa mmoja. Nitarudia kuisema kwa mara nyingine tena, USIIPOKEE ALAMA YA MNYAMA, kwa maana utapata BONDE LA KIFO MILELE.
Kwa hiyo Watoto wangu, natumaini masikio yenu yamezibuliwa. Natumaini nimeweka hofu kiasi ndani yenu, kwa maana ninalosema ni ukweli. Itawabidi mjifanye kuwa imara wenyewe, imara kushinda nyakati zozote za maisha yenu yote siku na wakati huo utakapowadia. Kwa maana itabidi mwende kumwomba Baba yenu Yehova. Someni Biblia, leteni Mwili wa Kristu pamoja, kwa maana vita hivi vinapiganwa Mbinguni na wakati huo huo vinapiganwa Duniani. Hivi ni vita ambavyo vitazingira ulimwengu wa Roho na wa mwili wa unachokiona na unachokigusa, kila kilichokiovu, popote kilipo iwe katika roho au katika maumbile, kitasafishwa mara moja na kwa mara ya mwisho.
Kwahiyo mjihadhari, muwe imara mnijue Mimi, Kwa sababu nawapenda. Huyu ni Yehova, Huyu ni Yehova, Muumbaji wa Mbingu na dunia, wa yote yanayoonekana na yasiyoonekana, Muumbaji, na Mvunjaji wa Ulimwengu.
Amani na Utukufu iwe kwa Baba, Amani na Utukufu iwe kwa Baba, Amani na Utukufu iwe kwa Baba ndivyo asemavyo Yesu Kristu wa Nazareti, pamoja na Nguvu za Roho Mtakatifu. Kwa maana tunawapenda ninyi Watoto, Msikilizeni Baba Yangu kwa maana hana kitu ila Upendo tu. Na amenipa Mimi Nguvu na Mamlaka kutekeleza Sheria Yake. Kwa hiyo kumbukeni alilo waambia. Amani iwe nanyi kondoo Wangu wa Kiume na wa Kike kwa maana nitakuwa pale kwa wakati uliowekwa kuwachukueni na kuwa pelekeni mbinguni, Muwe na ujasiri muwe imara. Sifa na Utukufu zimwendee Baba. Sifa na Utukufu zimwendee Baba.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )