70. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 30 Mai 1992 Jumamosi saa 9:23 usiku kwa lugha na Kihispania na Kiingereza.

Kihispania:

Safina! Safina! Mwanangu huo ni ukweli, unachokifikiria. Kila ninachosema kinatoka kwa Mungu wako; Kristu; Roho Mtakatifu, na Baba, kwa sababu muda sasa umeisha. Umekwisha, kwa maana unasema Neno Langu kwani Baba ni Ukweli. Inakubidi uangalie angani kwa maana dunia inakwenda kubadilika. Kila kitu unachodhania kipo na kitakacho kuwapo kitakuja kubadilika.

Kwa tarehe ambayo sintakuambia, lakini ninachokuambia utakuja kuishuhudia .Yote yatakayotokea yako karibu yenu, kwa sababu kutakuwapo na ishara nyingi. Ishara zilizoko kwenye Biblia zitakuja ongezeka na kutimizika zaidi kuliko ilivyokuwa kabla. unapaswa kuwa mwangalifu na makini kwa vile yataanza pole pole na kisha kitu popote kitaenda kwa kasi.

Mpaka siku ile itakapokuja mtakuja kutishika sana. Kwani nchi zote ambazo mnafikiri mnazifahamu zitakuja kukoma na kufikia mwisho wao. Nchi za miji, nchi za kila kitu ambazo mnafikiri zipo na hazipo, lakini zitakuwapo. Ni vigumu sana kuelezea kitakachokuja kutokea kwa sababu hamwezi kuja kuamini.

Atakuja kutokea mtu ambaye shetani atakuja kumtuma. Ni mtu mchafu sana ambaye anadhania kuwa anaweza kuiongoza dunia vizuri kuliko Mimi. Atakuja fikiri kuwa yeye ni mungu. Lakini yeye hana nafasi, kwa sababu yeye ni binadamu tu. Kwa kuwa binadamu hawezi kufanya jambo ambalo Mungu wa Dunia, wa Nyota, wa Mbingu, wa kila kilichopo, anaweza kufanya. Kwa kuwa Mimi nililiumba Dunia na vyote nilivyoyasema; yeye si kitu.

Atakuwa na Shetani upande wake, kwa sababu Ibilisi atakuja kumsaidia. Lakini shetani amekwisha kupoteza, lakini angalia, kutakuwa na watu ambao mtu huyu atakuja kuwaua, watu wengi, kwa mdomo ama vinywa vyake, midomo ambayo itasema vitu ambavyo wote watakuja kuamini, na watakuja kumpenda yeye, kama vile alikuwa mtakatifu, lakini ni mtakatifu wa shetani.

Ndiyo, anakuja kuwaua watu wengi kwa bunduki, kwa mabomu, kwa ndege, kwa meli na kwa njaa. Kutakuwa na watu wengi ambao watakuja kufa, kwa sababu hawatakuwa na chakula.

Amerika ya Kusini itakuja kuteseka sana. Katika Amerika ya Kusini watu watakuja kuhama, kwa sababu itakuja kuwa vigumu sana kuishi. Watakuja kutafuta mahali pakuishi, lakini kamwe hawatapapata. Hatimaye watu watakuja kukusanyika na kujazana kwenye miji mikubwa ili kutafuta kazi, zaidi kuliko nyakati zilizopita.

Mtu mbaya, niliyekwisha waambia habari zake atakuja kuwa na makao, na atakuja kuwaua kama wanyama. Hatakuja kuwajali kama wanateseka au la, kwa sababu atakuja kuwa mfalme wa dunia. Atakuja kuiweka dunia mikononi mwake.

Lakini kitakachokuja kutokea,nitakwenda kuyakata mikono yake, nikiwa pamoja na Mwanangu Yesu. Watu watakuja kula mbwa, na paka, na mapanya, na wanyama wote ambao watawapata, au kuwa kamata, kwa sababu hawatakuwa na chakula. Sheria haitakuwa kuwa sheria tena sheria. Kwa maana yule mtu anayejidhania kuwa ndiye Mfalme wa dunia ndiye atakuwa sheria.

Kiingereza:

Njoni Kwangu! Watoto Wangu msikilizeni Nabii Wangu kwa masikio yenu ambayo mmeyafungua. Tegeni masikio yenu na Mnisikilize kwa uangalifu sana; kwani haya siyo Maneno matupu ya Mwenda wazimu. Haya ni maneno ya Nabii ambaye niliyokuwa naongea naye kwa muda mrefu sasa. Naye hata anapata taabu kunielewa, kwa maana naye ni kama ninyi. Anafikiri kama dunia inavyofikiri, lakini nimekuwa nikimfundisha na kumwelimisha jinsi ya kutambua na kusikiliza Neno Langu.

Kwa hiyo Watu Wangu wa Duniani tegeni masikio yenu kwa maana hayo siyo maneno yake, ni Maneno ya Mungu Wenu, Yehova. Saa na siku inakuja kwa kasi sana. Nimekuwa nikimweleza yeye, haya kwenye Nabii zilizopita na ninazirudia kuyaeleza tena kwa sababu sitaki hapo baadaye mniambie kuwa hamkujua.

Kwa sababu mnajua mambo fulani fulani kwenye Biblia, kama vile kufufuka kwa Mwanangu na kurudi tena duniani kwa Mwanangu, lakini sasa nawaambia kwa undani zaidi kwa manufaa yenu. Kwa maana wakati huu wa mateso utatokea, kama ilivyoelezwa katika Biblia.

Ujerumani yote itaungana. Urusi itajiunganisha itajipanga upya. Nabii wa uwongo atainuka kutoka Mashariki ya Kati na atajiunga na Mnyama kwa wakati na saa iliyopangwa. Huyu Nabii wa Uwongo kutoka Mashariki ya Kati, Mashariki ya Kati atakwenda kutumia nguvu za Shetani kudanganya. Atakwenda kufanya miujiza. Atakwenda kufanya vitu ambavyo mtaviona kuwa vya ajabu, mambo Makuu.

Nawaonya sasa, chunguzeni, jaribuni, hukumuni kila Unabii kwa kadiri ya uwezo wenu, msishutumu. Kwa sababu hamwelewi, kwani mambo ya ulimwengu wa Kiroho, mwili hauwezi kuyaelewa kila wakati, hiyo haimaanishi kuwa ni uwongo, lakini nayo haimaanishi kuwa ni kweli. Njia ya pekee ya kuyapima ni kwenda kwenye Biblia na kuisoma na kuijifunza. Miujiza mingine iliyotokea na miingine iliyoelezwa itatokea. Kwa maana mtaishi kwenye nyakati ambazo mtashuhudia mambo hayo yakitokea. Nimekuwa nikiwaonya watu Wangu mara kwa mara kuhusu mambo ya nyakati za mwisho. Kwa maana Nawapenda ninyi nyote.

Mnatakiwa mjitayarishe wenyewe. Muingie kwenye Biblia siyo kama jambo la kujifurahisha ila kama jambo la kufa na kupona. Kwani katika Biblia mtapata nguvu mnayohitaji, nguvu za Roho Mtakatifu. Mjihadhari mnakwenda kumtupia jiwe lile nani, kwani jiwe lile linaweza kumwua mmoja wa Manabii Wangu. Na njia pekee ya kujua ni kama una Roho Mtakatifu ndani yako.

Kwa maana kuna majeshi mengi sana ya Mapepo Wachafu huko, itawafanya mpatwe na kizunguzungu. Wengine wenu mtakwenda kuogopa, kwa yale tuu ninayo waambia sasa hivi, lakini hiyo ndiyo hali halisi. Ninyi Wachungaji hamjajizatiti itakiwavyo. Hamjui hata kidogo Pepo Wachafu walivyo. Mnatafuta na kutoa utatuzi wa kubabaisha. Mnadhani mnaweza kutoa jawabu kwa kuyapeleka matatizo ya kipepeo kwa mtafiti bila kujua kuwa huyo mnayempelekea yeye mwenyewe anaweza kuwa anapepo. Shetani amefanya kazi yake vizuri sana, lakini huna haja ya kujali kama uko kwenye mwili wa Kristu. Na kama mko imara katika Mwili wa Kristu. Kwa maana ni wale walioko imara tu ndio watakao weza kufika, Waliotakata, wasio na mawaa, waaminifu, waliona haki. Kwani kuna wengi wanaojiita Wakristu lakini walio wabaya kuliko wasio Wakristu, katika mawazo yao na katika theologia zao.

Sasa sikilizeni! Ukristu kimsingi ni rahisi. Unamgeukia Yesu Kristu wa Nazareti, Mfalme wako wa Wafalme, Bwana wa Mabwana. Yeye ni Mlizi wako. Yeye ni kiongozi wako. Kwa maana Yeye amekwisha kushinda vita. Lakini tatizo nikuwa unahitajika uende mwendo wote. Inabidi ubebe msalaba wako, kwani kila mtu inabidi atoe hesabu ya maisha yake, hapo mwishoni. Kila mtu aliyewahi kuishi duniani inabidi afahamu kuwa siku ya hukumu itakapokuja kila ulimi itabidi uungame kuwa Yesu Kristu ni Bwana wa Mabwana na ni Mfalme wa Wafalme na kila goti na nina maanisha kila goti itabidi ipigwe kuanzia mtu wa kwanza hadi mpaka mtu wa mwisho wakati huo. Shetani mwenyewe naye itambidi apige goti, lakini inabidi afungwe kwa mnyororo na kutupwa shimoni pamoja na wengi wenu Watoto wangu wale ambao wana mioyo migumu na akili zilizofungwa. Msidanganywe na maisha marahisi, maisha maovu ya dunia hii, kwa maana dunia hii imekaribia kufikia hatima yake. Someni kitabu cha Nuhu. Habari ya Nuhu iko katika kitabu cha Mwanzo, historia ya Mwanzo.

Soma kuhusu Nuhu. Yeye alijua kilichokuwa kina kuja kwa maana Nilimwambia. Na alijitayarisha na kujitayarisha na kisha alipanda kwenye ule mtumbwi mdogo. Na kisha akangoja kwa subira kwa sababu alijua ni nini kinakuja. Wakati wa Nuhu kwa mara nyingine umefika. Nabii huyu siyo mwenda wazimu. Anaongea Neno la Mungu Yehova. Kwa maana wakati huo utakapokuja utakuwa umechelewa, kwa hiyo inabidi ufanye msingi imara juu ya Mwamba, sasa! Leo! Yesu Kristu wa Nazareti ni Mwamba wako, Ujishike juu yake kwa namna yeyote unayeweza, lakini Roho Mtakatifu atakuongoza kwa njia yoyote ile unayohitaji ili kujishikizia kwenye mwamba huo.

Kwa maana ninyi nyote mna matatizo mbali mbali na mna njia mbali mbali za utatuzi, lakini uamuzi ni wenu. Mnahiari ya kuchagua na mnahiari ya kutokufanya lolote. Adhabu ya kutokufanya lolote ni sawa na kuchagua kwenda kwenye upande wa upotovu. Mwokozi wako ni Yesu Kristu, hiyo ni rahisi kumbuka hilo, kwa maana Mwanangu atakuongoza, na atakusaidia kupita salama kwenye vita pamoja na Roho Mtakatifu na Mimi Yehova.

Kwa maana Mungu wa Mbinguni na Dunia hajawahi kupoteza na wala hatakaa kupoteza. Kwa maana niliumba kila kitu kutoka patupu. Nilisema na ikaundwa. Wengi wenu hata hamwezi kutafakari usemi huo mdogo. Katika ulimwengu wa kiroho ni Ukweli, Tulikuumba wewe, tulikuunganisha, tuliyaweka pamoja, lakini Roho Wachafu walizibomoa lakini yote hayo yanakuja kufikia ukomo wake. Angalieni ishara, ziko hapo tele zimewazunguka. Mungu wenu hatawaacha, lakini inabidi mgeukieni Yesu Kristu wa Nazareti. Yeye ni Mlango. Yeye ni njia ya Wokovu.

Amani na iwe nanyi Watoto Wangu, najua wengine wenu mtahitaji kupata ujumbe zaidi ya huu. Lakini inawabidi kufanya wenyewe, inabidi mjifunze, kujisomea Biblia, mzungumze na Ndugu zenu wa Kikristu wa kiume na wa kike ambao ni imara katika imani. Siyo wale wanaojisifu wanaojigamba kwa maana wa aina hiyo ni wengi ambao wamepotea wakiwa wamejificha chini ya kivuli cha Yesu. Muwasaidie ndugu zenu wa Kiume na wa Kike, wapendeni waleeni, Mama zenu, Baba zenu, kaka zenu, dada zenu, kwa maana wote mtakuwa katika hali hiyo moja. Kwa hiyo tafadhalini sikilizeni Maneno Yangu. Wapendeni jirani zenu, Mniombe. Tubuni dhambi zenu, na Mniamini Mimi, bila kujali litatokea nini, kwa maana saa imewadia. Baba yenu wa Mbinguni, pamoja na Mwana na Roho Mtakatifu siku zote Watakuwapo. 

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.