71. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 1 Juni 1992 saa 7:22 Usiku katika Kiingereza.

Naam Ray. Unaendeleaje? Naam, Sanduku la Agano litazinduliwa. Ndiyo hiyo ni sawa, Nilisema kuwa Sanduku la Agano litaletwa kutoka sehemu ya maficho yake na kuwekwa upya kwenye Hekalu Langu; jipya, la mwisho naya timati ambayo itajengwa na Binadamu.

Sanduku la agano litawekwa mahala pake palipo tayarishwa maaluma kwa ajili ya anzisha Neno Langu. Ile iliyotolewa kabala kwa kupitia kwa Manabii, Mitume, kwa ajili ya yale niliyokuwa nakuambia kwa wiki zilizopita. Yote yale ni ukweli na nisahihi, Nilikuwa nakupa vipande vipande vya mambo ya siku chache za kabla ya mwisho.

Mambo mengine yapo katika mafumbo ili watu fulani fulani wasigundue maana ya mafumbo hayo kwa wakati muafaka. Ingawa muda uko karibu sana, lakini ulichoambiwa ni kweli, na halisi kabisa. Kwa maana Mimi ni Mungu wa kila kitu, wa Ulimwengu wa kila kilichopo na kitakacho kuwapo. Mimi ni Yehova na Mwanangu Yesu Kristu na Roho Mtakatifu.

Sanduku la Agano litazindiliwa. Kutakuwa na sherehe Mbinguni na kwenye Hekalu na kila mahali ambako kuna Wazawa wa Abrahamu amabao wataweza kufanya sherehe. Kutakuwa na furaha na chereko chereko na amani kwa siku saba amabazo zitaruhusiwa. Kwa sababu hiyo Sherehe zitakuwa zimeanza mipangilio ya mwanzo wa mwisho kama ilivyo elezwa katika vitabu Manabii: Ezekiel na Daniel na Yohana.

Kwani nilichosema kitafanyika bila badiliko la aina yeyote. Mpinga Kristu pamoja na Nabii wa Uwongo watatokea kwa wakati uliopangwa na watashindwa sawa sawa na nilivyoeleza. Kwa hiyo mjihadhari na Mhuri wa Mpinga Kristu. Kwa maana kosa la kuwa na Mhuri huo mwilini mwako ni kitu ambacho hakitasamehewa kabisa kwa hali yeyote. Kwa maana Mhuri huo ni maasi makubwa ya sheria Yangu. Ni dharau na maasi makubwa ya utaratibu wa uadilifu. Ni maasi makubwa ya sheria iliyoandikwa. Mhuri wa Mnyama nikielelezo cha upande ambao umeweka utiifu wako, na kila kitu ambacho ni kichafu siyo mali ya Yehova. Mwanangu Yesu Kristu wa Nazareti, ana mamlaka ya kuangamiza, ondosha, haribu, na kumtupa kila mtu aliye na Mhuri wa Mnyama. Kwa maana ufalme wao utakuwa kuta za Jehanamu. Kwani wanastahili kuishi na Wafuasi wake kama Watakatifu wangu walivyo na stahili ya kuishi mbinguni. Kilicho cha haki ni cha haki! Mwanangu ana sheria ya haki na ataitekeleza bila huruma kwa Uchaguzi wake, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana na ni Mfalme wa Wafalme. Kwa wale Kondoo wa Kiume na wa Kike wote ambao watakao vumilia mateso na majaribu katika maisha yao wataenda Mbinguni.

Uwepo wa Jehanamu utaanza kwa ajili ya wakazi wapya ambao watachukua mhuri wa Mnyama kwa wakati uliopangwa. Kwa ajili ya msaada wao katika maasi katika kumfuata Lusifa katika mipango yake ya kuchafua Jina langu na kila kitu nilicho kiumba. Huyu ni Mungu wenu Yehova, aliye Mwanzo na Mwisho, na Mwanazo wa Mbingu mpya utaanza pale Mwanangu Yesu Kristu atakapo funga na kuangamiza kitu cha mwisho cha katika Sayari hii.

Najua Watakatifu Wangu wamekuwa wakingoja na kungoja na kungoja, lakini kama nilivyosema kupitia kwa Manabii Wangu kuwa wakati na saa vitafika, na tumeukaribia muda huo. Sitawapeni ninyi tarehe au wakati, kamwe haitatolewa mpaka itakapotokea. Kwa hiyo mwangalieni Baba yenu Yehova, Mfalme wenu wa Wafalme, Bwana wa Mabwana na kwa kupitia kwa nguvu za Roho Mtakatifu utapapata Mbingu na Sisi katika Ufalme mpya. Ambayo itaanza kwa wakati ulio pangwa.

Kwa hiyo tubuni dhambi zenu. Mtuombeni Nasi tutawaonyesheeni njia. Kwani wakazi wa dunia watashtuka sana watavunjika moyo watakapo gundua kuwa kuna Mungu Yehova na siku zote alikuwapo. Kwa maana Lusifa amefanya kazi ya kuwadanganya wengi, wengi sana, kwani wengi hata hawawezi kufikri kuwa au kujua kuwa Yehova yuko, lakini wacha na iwe hivyo, na iwe hivyo.

Kwa maana Sheria Yangu na Njia Zangu zimekuwapo kwa Maelfu ya miaka, na uwepo wangu umekuwepo hapa hata kabla wa Mwanzo lakini wao waligeuza migongo yao na kwenda zao. Kwa hiyo kwa nafsi hizo maskini zenye bahati mbaya Nami nageuza Mgongo Wangu kwao na kuondoka nikiwa na tokwa na machozi Machoni Mwangu na moyo wenye masikitiko makubwa. Walikuwa na uamuzi wao na walifanya mioyo yao kuwa migumu. Kwahiyo na iwe hivyo!, Kwa hiyo na iwe hivyo!

Huyu ni Yehova, Muumba Mbingu na Dunia, wa kila kilichopo na kitakacho kuwapo. Kumbuka hivyo, Kumbukeni, Kondoo Wangu wa Kiume na wa Kike, kwa ajili yenu niko masaa ishirini na mine kila siku nikiwa pamoja na Mwanangu na Roho Mtakatifu. Muwe na shangwe muwe na furaha, kwani yataisha hivi karibuni na tutaanza tena kwa upya, na kwa ubichi. Kwani Vyumba vyenu viko tayari, muwe na subira zaidi kidogo. Huyu ni Yehova. Huyu ni Yehova akiwa na Upendo na Amani Moyoni mwake. Nawakaribisheni. 

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.