72. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 2 Juni 1992 saa 4:47 asubuhi katika Lugha ya Kiingereza.
Nataka uendelee kwa mwendo wa taratibu wakati unapoandika Unabii huu. Nataka urudie rudie kuusoma na kuufanyia masahihisho Unabii huu mpaka ujisikie kuwa Neno Langu, kwa njia ya Roho Mtakatifu, na kwa kupitia midomo yako limenakiliwa vizuri kama Nilivyo linena kwa kadiri ya uwezo wako. Msikilize Roho Mtakatifu, fuata atakavyo kuelekeza, jipe moyo kwa maana unachokiandika siyo chako. Naona unajaribu kutumia kipimo cha kibinadamu, cha kidunia kuandika/kupima ninacho sema. Inawezekana utashindwa kuelewa ninachojaribu kusema, au kwa njia ninayo jaribu kusema au katika lugha ninayosema, lakini Ray Niamini. Inawezekana isiwe sahihi kisarufi. Inawezekana isikike tamu masikioni.
Inawezekana kwako isiwe kwenye hali mipangilio unayotaka. Lakini Neno Langu au Maneno Yangu kamwe hayatarudi tupu ila wewe jiimarishe na ujitayarishe kwani kutakuwa na Kaka na Dada zako ambao watakuja kukushambulia wewe. Kwa jinsi na namna ambayo Neno Langu umelitafsiri katika lugha ya Kiingereza, lakini usikubali jambo hilo likusumbue. Kwa maana siku zote kungelikuwako watu kama hao. Watu walio na mioyo migumu. Watu ambao hawawezi kuona na wala hawataki kuona. Hawata iona wala hawataitafakari, hata kama itakuja imeandikwa kwa usahihi sana hadi herufi ya mwisho au kwenye nukta ya mwisho ya kila (i). Kwa maana nimetayarisha mahali pa watu kama hao, Ray. Kumbuka hilo!
Kwa hiyo uwe imara, uwe mjasiri na piga taipu kile unachosikia. Kwa mapangilio wa jinsi kinavyo kuja. Usijaribu kuichambua na kuibadilisha. Msikilize tu Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu atakuongoza kiakili, kimwili, katika matamshi (spelling) katika fasihi ya muundo wa sentensi. Sasa sikiliza! Hii siyo kwa ajili yako. Najua kuna wakati unataka kuifanya ili isikike vizuri.
Niamini, Ray! Kwa maana Bwana Yehova anaposema hakuna kamwe makosa. Kwa hiyo vuta subira, uwe imara na umsikilize Roho Mtakatifu. Sikiliza ile sauti inayo kuambia ni herufi ipi uiweke kuwa herufi kubwa, na ipi uifanye kuwa herufi ndogo, nini cha kukazia. Wewe ni Mtumishi Wangu. Wewe ni Rafiki Wangu. Wewe ni Kondoo Wangu dume, ebu jiachie na utii tu. Usiwe na wasi wasi. Kwani nitakuambia ni kwa njia gani na wakati gani ugawe Unabii na Maono hayo. Kwa maana kutakuwa na Unabii na maono mengine mengi zaidi, kwa hiyo kaza mwendo. Usijali, ila uwe na subira na uvumilivu, uwe imara. Kwa maana na kwenda kukulinda.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )