Sauti 74

Sehemu hii ya sauti 74 ni ya dakika kama 6:24 (768 KB) imehaririwa (kufupishwa) kutoka kwenye habari yenyewe ya dakika 19 ya kwenye mkanda wangu mdogo wa kurekodia. Kwanza fanya majaribio kutoka: sound.htm kuona kama mitambo yako ya kutoa sauti inafanya kazi sawasawa. Kuna sauti ya kukwaruza kwenye kanda au faili hii. Unabii huu uko katika lugha ya Kiingereza na lugha isiyoeleweka. Soma ujumbe wa hapa nchini wakati unaposikiliza mkanda huu wote iliuweze kupata matokeo mazuri.

Ilikusikiliza mkanda huu unahitajika uwe na Kadi ya sauti, na Modamu ya 14.4 au 28.8 kwenye komputa yako. Ili kupata "the RealAudio Player" ya kusikilizia mkanda huu kama haipo kwenye komputa yako, bonyeza kwenye kitufe hiki.
 

 

74. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 5 Juni 1992, Ijumaa saa 8:45 usiku katika lugha, Kiingereza, na lugha isiyoeleweka.

Naam! Mna hali gani, Kondoo wangu wa Kiume na wa Kike? Nitawaongoza Mimi, kadiri itakavyo lazimu, kwa maana kuonekana kwa nyota itatokea ghafla na bila kutegemewa, lakini saa na wakati, kwani kisu kimekwisha wekwa kwenye koromeo la dunia. Mnyama atajaribu kuutafuna mwili wa Kristu. Atakuwa na mipango kadhaa ya jinsi ya kusambaratisha na kufuta Mwili wa Bwana. Washiriki wa Mpinga Kristu watakusanyana kumzunguka Nabii wa Uwongo. Kwa maana Nabii wa Uwongo atatunga hila ya kudhoofisha sifa na uhalali wa Ukristu. Na kwa mpango huo au amri/agizo hiyo ambayo itatimizwa, itaweka katika utekelezaji wa lengo kuu la Mnyama wa kuhodhi Mamlaka yote bila kuingiliwa kutoka mahali popote.

Mnyama na Nguruwe watapanga mipango dhabiti ya kuuteka Ulumwengu wa mangaribi. Kwa maana maendeleo ya fedha, ya hali ya uchumi ya dunia zitaanguka juu ya Mnyama, ambaye ataamua nani aokoke kutokana na mwanguko wa mfumo wa kifedha wa Dunia. Kwa maana uweza wa utajiri, uweza wa silaha, uweza wa mabadiliko yote ya siasa zitaangukia mahala pake pamoja na mwanguko wa mfumo wa fedha ambao utamleta Mnyama kwenye Mamlaka pamoja na wafuasi wake.

Kwa maana madaraka ya Mnyama yanatoka kwa Shetani mwenyewe kwa kupitia kwa Nabii wa Uwongo, ambaye atamshauri na kumwongoza huyo Mwenda Wazimu. Nitaleta kwenye utimilivu nilichokiandika katika Biblia kwa wakati uliopangwa, kwani mwanguko wa mfumo wa fedha utatokea. Kwa maana kuja kwa taabu ya dunia kwa mara ya kwanza itaanza pale ambapo Mafuta na Biashara zitakapokuwa zinaongoza Dunia, (lugha isiyoeleweka?) milki za Mbinguni zitakuwa zinaongoza vita ambavyo vita vitaongeza kasi ya ukali kwa kadri mfumo wa kijamii utakavyokuwa unaongeza kasi ya kusambaratika. (Lugha isiyo eleweka?)

Nawapenda Watoto Wangu, Nawapenda, msikilizeni Nabii, yasikilizeni Unabii, kwa maana ndege ile itakayofika na kutua kwenye mwisho wa kiwanja itakuwa kitovu cha ajali katikati ya Jiji. Pamoja na uchanuo utakaotokea wa miali ya jua ya nyakati za katikati ya majira ya joto itakapo kuwa inapenyeza kwenye ardhi. Maangamizo ya Ndege yatatokea wakati Mnyama atakapokuwa anamlaumu Waziri wa Fedha kwa kutokutii sheria yake. Kwa maana Waziri wa Fedha atampinga Mnyama, lakini matokea hayatakuwa na madhara mabaya kwa Mnyama pamoja na chama cha mnyama. Kwani Mnyama atamzunguka na kumshinda Waziri huyo kwa kutumia mbinu na hila za ujasusi wa chini kwa chini na mlolongo wa wapelezi chini kwa chini.

Ugunduzi na uundaji wa Bomu, ambalo litapeleka chembe chembe ya hewa ya sumu angani itawaangamiza majeshi ya upinzani kwa haraka na ghafla. Kwa hiyo jihadharini na siasa, mjihadhari na majeshi, mjihadhari na kila kitu ambacho sicho cha Yesu Kristu wa Nazareti. Kwa maana mateso ya Kanisa yatatokea wakati wa mwezi mpya na mpevu utakapoanza kuchomoza na wakati makubaliano ya amani na Mnyama yatakapowekewa sahihi. Je, Mnanisikiliza ninyi Watoto Wangu?, Kwa maana inawabidi msome Biblia na kuijifunza na kumtii Baba yenu wa Mbinguni, Yesu Kristu wa Nazareti na Roho Mtakatifu. Kwa maana maangamizi yatakayotokea yatawafanya mshtuke sana kiasi cha kuwafunya msiwe na imani. (Lugha isiyoeleweka?)

Kwa hiyo Kondoo Wangu wa Kiume na wa Kike muangalie na mjihadhari na mikono ile, muangalie na mjihadhari na maandamano na mihadhara ile, muangalie na mjihadhari msije wenyewe mkageuka kuwa kama Mnyama. Mimi ni Yehova. Mimi ni Yehova. (Lugha isiyoeleweka?) Nawapendeni ninyi. Nawapendeni ninyi Watoto Wangu. Yehova ni wa kwanza na wa mwisho. Mungu wa Upendo, Mungu wa kila kitu.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.