Sound 78

Sehemu hii ya sauti 78 imehaririwa (kufupishwa) na kuwa ya dakika 15:40 (1.8 MB) kutoka kwenye habari yenyewe ya kwenye mkanda wangu mdogo wa kurekodia. Kwanza fanya majaribio kutoka: sound.htm kuona kama mitambo yako ya kutoa sauti inafanya kazi sawasawa. Kuna sauti ya kukwaruza kwenye kanda au faili hii. Unabii huu uko katika lugha ya Kihispaniola. Soma ujumbe wa hapa nchini wakati unaposikiliza mkanda huu wote iliuweze kupata matokeo mazuri.

Ilikusikiliza mkanda huu unahitajika uwe na Kadi ya sauti, na Modamu ya 14.4 au 28.8 kwenye komputa yako. Ili kupata "the RealAudio Player" ya kusikilizia mkanda huu kama haipo kwenye komputa yako, bonyeza kwenye kitufe hiki.
 

78. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 6 Juni 1992 saa 6:01 mchana katika lugha ya kihispaniola.

Kwa sababu siku imefika, wewe angalia, angalia mwili wako. Mwili wa Kristu kwa sababu mwili wa Yesu unakwenda kuteswa, kama hutatibu mwili wa Kristu. Wewe utateseka zaidi, kwa sababu mimi ni Mungu wa kila kitu kilichopo, na kitakachokuwa ninawaeleza ninyi. Wewe tibu mwili wa Mungu, Mwili wa Yesu Kristu, kwa sababu mlango wa shetani unakwenda kufunguka, na atakwenda kutaka kuwala nyinyi kwa meno matupu.

Atautafuna mwili kwa nguvu zote awezavyo, na kama wewe hutafanya mwili wa Kristu imara, atakuwa chakula chake. Utaliwa kwa njaa ya mbwa kichaa, angalia, ninakueleza ukweli. Huyu ni Mungu wako, kwa Yesu Kristu, na Roho Mtakatifu. Mimi ni Baba wa vyote, wa kila kilichopo na kitakachokuwa. Tazama, siku iliyosemwa katika Arabia hii hapa, kama utajifanya kiziwi mwenyewe utakwenda kupoteza kila kitu. Kama hutaimarisha, namna unayoishi hutakuwa na nafasi. Nakwambia, namna sahihi, kwa moyo wangu, kwa upendo wa moyo wangu.

Angalia, Ninaupenda ulimwengu, nawapenda watakatifu wote, lakini nawataka wawe safi. Siwataki wawe wachafu. Walio safi tu ndio watakaokuja kwangu, kwa sababu yote niliyo nayo ni safi. Ninawaambia kwa midomo yangu, kwa upendo wa moyo kwa sababu najua nini kitakacho tokea. Nawaambia tabia sahihi, kwa sababu siku niliyowaambia hii hapa, kwenye Biblia, katika siku za zamani.

Sio muhimu ulifanya nini jana. Si muhimu unataka kufanya nini. Ni muhimu tu jinsi unavyotembea. Ninakutaka wewe utembee umenyooka kumwelekea Kristu na Roho Mtakatifu, na mimi, Baba yako, hiyo yatosha, hayo ni muhimu hasa dakika hizi. Kwa sababu nitasamehe yote uliyoyafanya na yote yale unayotaka kufanya, kama sio kitu kilichonyooka.

Tazama, unakuja wakati ambapo hutakuwa na nafasi nyingine. Wakati nyundo itakapogonga kila kitu kilicho kibaya, hamtapata nafasi. Ninawaambia dakika hizi kwa sababu nataka ninyi mnisikie mimi!

Angalia, Mimi ni Mungu yule awapendaye kwa Upendo. Hiyo ndiyo maana ninawaambieni mambo haya sasa, lakini kama mtaufanya mioyo yenu kuwa migumu, ninyi hamtaenda kuwa na nafasi. Kutakuwa na wale wengine wenu ambao hawatani amini Mimi. Mimi sitafanya lolote kuwa zuia wao kwa sababu Mimi nimekuwa nikiwaambia na kuwaambia lakini wao wamefunga macho yao na masikio yao. Wao wananenda kuishi pamoja na shetani kwa muda wote ambako kuna muda, na wanaenda kuteseka sana.

Sasa Neno hili ni kwa ajili ya Watakatifu wale wanaopenda kusikia, wale wanaotaka kujiokoa wao wenyewe. Wao wanamtafuta Mungu yule aliumba Vyote, Nyota, Mwezi, Miezi, na Dunia ile ambayo wanakoishi hivi sasa, na yote yale wayaonayo, na yote hayo Mimi nimeyaumba kwa Neno Langu.

Angalieni Watoto Wangu inaumiza Moyo Wangu kama nitawapotezeni ninyi. Nitatokwa na machozi kama nitawapotezeni ninyi, lakini inawabidi ninyi mjiimarishe. Kwa maana siku zinakuja ambako wote wale wanaoishi duniani wataenda kuteseka, kama hamtasikiliza Neno la Baba wa Mbinguni. Baba wa wote pamoja na Mwanaye Yesu Kristo na pamoja na Roho Mtakatifu, Mimi ninawaelezeni kwa njia ile iliyo sahihi, lakini ninyi inawabidi muifanye ninyi wenyewe.

Hakuna yeyote atakaye wasukumeni kuelekea kulia au kushoto. Inawabidi mtumie yote yale mliyonayo, katika Roho zenu, katika Akili zenu, katika miili yenu. Itawabidi mchague kati ya shetani na Mimi, Mungu wenu aliyefanya kila kitu. Itawabidi mkachague, siyo ngumu. Hayo ni yote yale ambayo itawabidi mkafanye. Changueni kwa namna ile ambayo mnahitaji kwenda, kwa sababu Mimi nina Mahali palipo tayarishwa kwa ajili ya Watakatifu, na Mahali kwa ajili ya wale wasionipenda Mimi.

Inawabidi mnisikilize Mimi, Mimi ninaongea kwa Midomo Yangu ambayo ni Misafi na Iliyonyooka kwa sababu kila kitu kile ambacho ni Changu Kusafi na kimenyooka pamoja na Mwanangu na Roho Mtakatifu. Mimi ninaenda kuwaambieni, na kuwaambieni na kuwaambieni na kuwaambieni hadi mtakapo weka mikono yenu kwenye masikio yenu, kwa sababu hatataka kusikia tena.

Kisha Mimi nitaenda kujua mahali mioyo yenu ilipo; kama mnanipenda Mimi au lah, kwa sababu Mimi ninaenda kuwaambieni hadi mtakapo choka, nami ninaenda kuwa ambia hayo hayo. Mimi ninataka ninyi muenda mkatubu dhambi zenu. Mimi ninataka muende mkawatafute Kaka zenu na Dada zenu. Mimi ninataka ninyi mkaishi kwa Amani. Mimi sitaki ugovu.

Wachungaji ni wabaya pia. Inaniumiza moyo wangu, kwa yale mambo wanayoyafanya. Tazama! Mimi nimechoka kwa sababu wanafikiri wao ni miungu pia kwa mikono yangu iliyonyooka, nitawarekebisha mara moja. Watateseka kuliko watakatifu kwa sababu hawakuwatafuta. Hawakuwatafuta watakatifu wangu wanaohitaji misaada kwa sababu wao wanafikiria nafsi zao wenyewe.

 

Mikono yangu itawapiga wao kama vile nimpigavyo inzi, itakuwa haraka. Wao wanafikiri wanayo amani yangu sasa. Wanafikiri wanayo maneno yangu sasa. Washangazwa kwa sababu Watakatifu wangu wanaishi mitaani, bila chakula bila mavazi na wao hawawatafuti.

 

Wanaongea maneno mazuri midomoni mwao, lakini hawafanyi lolote kuwasaidia. Siku moja au siku mbili kwa wiki, kwa maneno mazuri midomoni mwao, hawana imani ya kufanya kile wakisemacho. Ndio maana nawaambia nyie sasa, ninyi wachungaji. Mimi ninajua mtapata kichaa kwa haya nitayowaambia.

 

Mtachukua mawe na mtakimbia kufuatia maneno yangu kwa mawe; Kufunga masikio yenu na mioyo, kwa sababu hamtaki kusikia. Ninachowaambia ninyi, na mtamwua Raymundo kwa sababu hampendi kile anachokisema. Tazama! Kama yeyote atanyanyua mkono wake kwake, mimi nitanyanyua mkono wangu kwako, na utajua kwamba Reymundo hana nguvu zozote, lakini Mimi ninazo nguvu za kila kitu. Reymundo hawezi kufanya kitu isipokuwa kujificha. Kama mtachukua mawe yenu, hakuna kitu ambacho mmewahi kufanya kitawaokoa.

Muda ni huu sasa, ule ambao nimekuwa nikiwaambia ninyi katika Biblia kwa miaka na miaka na miaka, na mmefunga macho yenu na masikio yenu. Mimi nawahitaji, watakatifu wangu ambao bado hawajalipokea neno la Mungu, na roho mtakatifu kwa kusikia. Mimi najua ninyi hamfanyi kazi mimi niliyowatuma kufanya.

Ndiyo maana, mimina maneno yangu mimi nitakwenda kuwaeleza ninyi mwenyewe kwa sababu muda unapita,. Mimi sijali kama wewe utakuwa kichaa. Sijali nini mnataka kufanya, kwa sababu mimi nitawaua ninyi kama inzi. Huyu ni Mungu wenu, Baba wa kila kitu, nawaeleza ninyi sasa.

Msipate kichaa kwa ajili ya mwanangu kwa sababu hamtafanya kitu. Mimi ni neno la kwanza na la mwisho na mimi nataka ninyi mkumbuke hilo, kwa sababu mikono yangu ni mizito sana. Nawahitaji ninyi mkumbuke haya, ninayowaambia ninyi sasa. Mimi nahitaji hili liwake mioyoni mwenu nyie wachungaji.

Roho mtakatifu atakwenda kuanza, na atabadilisha sheria, ambayo mnawapa watakatifu wangu, kwa sababu sheria mnayotumia ni sheria ya binadamu, sio sheria ya Mungu. Angali makanisa mangapi mnayo, vipi maneno mengi tofauti mliyonao, ninyi ni vipofu na viziwi.

Mimi NAONGEA neno MOJA TU, na katika namna moja, na iliyonyooka na kweli. Kwa sababu kondoo wangu wanahitaji msaada, na watakwenda kuhitaji msaada zaidi katika muda wote tangu wao wazaliwe, kwa sababu nitafunga kitabu cha dunia hii. Maneno yangu kila mara hufanya kile mimi ninachosema. Huyu ni Mungu wenu, pamoja na Yesu na Roho mtakatifu. Mnitafute mimi, mnitafute mimi, watakatifu.

Malaika wako tayari kwa sababu vita vimekwisha anza. Vimeanza! Kile nilichoanzisha mimi hakuna atakaye simamisha! Kumbuka kuwa! hakuna atakayesimamisha kile ninachokisema! Huyu ni Mungu wa upendo, katika upendo, wa upendo kwa Watakatifu wangu ambao hawana mtu wa kuwasaidia. Wao hawana mwingine zaidi ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Mimi ninaongea nanyi kwa sababu mimi ni kichaa, mimi kichaa kwa sababu nyie wachungaji hamnisaidii kama nilivyowaambia ninyi wakati nilipomtuma mwanangu. Kila mmoja anafanya kile anachotaka, na kuna wengi sana wanaohitaji msaada. Ninawaambia ninyi kwa mdomo wa upendo, lakini mimi ni kichaa.

Mimi nawahitaji ninyi mumkumbuke mtu wangu ambaye anawapa ninyi maneno yangu,. Raymundo wangu. Yeye yu mkononi mwangu. Ninawaambieni tena, kwa sababu anapokuja na Neno mkononi mwake ili kuwapeni ninyi nami nakwenda pia kuwatazameni ninyi, kuona ni nini unatakachofanyia neno hilo.

Nataka kusaidia, lakini nawataka ninyi kunitafuta mimi na kunitumikia, na msijitukuze wala kujiangalia wenyewe. Hamwezi kufanya jambo lolote pasipo mimi kumbuka kuwa, wakati ukisoma neno hili kwa sababu namfahamu Raymundo wangu, na kwa kiasi kidogo pindi ninapokwenda kumweleza yeye kuyatuma maneno yangu. Hivi sasa bado hafahamu ni kwa jinsi gani, lakini kwa kiasi kidogo pindi ninapokwenda kumweleza yeye.

Ninajua ya kwamba mtamkimbia ila yeye ni Mkono wangu. Ni hayo tu ninawaeleza ninyi kwa upendo, kwa sababu mawe ambayo mmechagua kuyabeba au mnayopenda kuyabeba, yatawaangukieni kichwani mwenu. Kumbuka! Huyu ni Mungu wenu. Huyu ni Mungu wenu, na Yesu na Roho Mtakatifu.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.