79. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 7 Juni 1992 saa 6:54 asubuhi Jumapili katika ndimi isiyoeleweka, Kiingereza na Lugha isiyoeleweka.

Kiingereza:

Mimi ninakupenda. Wakati mkono (wa saa) utakapo gonga nane katika bonde. Mahali pale ambako uta/upinde za walenga shabaha (wapiganaji) zitakapo kuwa zimekazwa (tayari kwa vita), itakuwa uwanja wa vita hapo Mnyama na ……(Lugha isiyoeleweka?).

Wakati ule mbwa atakaporudia matapishi yake ni ishara ya mahala moyo wake ulipo, katika uchafu, katika takataka ambayo inatawala roho yake. Hiyo ndiyo sababu ya Mnyama kurudi kwenye bonde. Bonde la hatima yake, ambayo itafunga mtego juu wa hatima yake. Ambayo ilikwisha pangwa miaka mingi iliyopita.

Wakati viatu vyako na miguu yako itakapo kuja pamoja, nakukusaidia kwenda haraka juu ya ardhi/nchi ambayo bado haijalipuka; hadi ile ardhi/nchi ambayo usingeliweza kuifikiria katika Mwili wako huo wa Kidunia; Nchi ya Jeshi la Mbinguni, mahali ambako kuna Utaratibu, kuna Amani, Kuna Utulivu. Mahali ambako Watakatifu wa Yehova wanaishi kwa Maelewano na utulivu milele.

Kwa hiyo sikiliza, kuwa makini kwa maana ishara ambazo unapewa sio za kuzipuuza kwa wepesi, hizo ni ishara za mambo ambayo hayana budi yatokee na kupita. Wakati vita vya bondeni vitakapokuja kukoma, kwa maana majeshi ya Mema na Mabaya yatapambana yenyewe kwa yenyewe. Kwa maana Baba yenu wa Mbinguni alikwisha nena siku nyingi zilizopita kabla haijatokea, wakati, siku, saa ya Yesu Kristo wa Nazareti.

Wakati utakapoona Farasi, pamoja na mpanda Farasi, akiwa na Uta/Upinde na Mshale ukiwa umewekwa kwenye uta na kulenga upande wa kushoto, huo utakuwa ni wakati na saa ya maangamizi ya Mpinga Kristo. Kwa maana alikuwa amemkufuru Baba na kila kitu kile ambacho ni Kitakatifu. Na Baba hawezi kuruhusu aina ya dhambi hiyo kutokea bila ya Hukumu juu ya makundi yote yanayohusika.

Kwa hiyo mjihadhari na Muhuri wa Mpinga Kristo, kwa maana Muhuri wa Mpinga Kristo utakuwa ni sababu ya Kuanguka kwako kama utaipokea. Hivyo ndivyo asemavyo Yehova, kwa maana Nguvu, Uweza Mamlaka inakaa juu ya Yesu Kristo wa nazareti, mara moja na kwa mara zote.

Kwa hiyo funguo za Ufalme wa Mungu ziko Mikononi Mwake. Yeye anaweza kufungua Mlango kwa mtu yeyote, na kwa wakati wowote kama atatubu dhambi zake, atafungua moyo wake, atasafisha maisha yake na kumgeukia Yesu Kristo wa Nazareti. Kwa maana Yeye ni njia, barabara, mlango wa kuingilia Mbinguni.

Kwa hiyo angalia ishara angani, angalia ishara katika Sayari ya Dunia. Kwa maana ishara zimekwisha anza kutokea. Jifunzeni Biblia mara kwa mara, mjueni Mungu wenu, kwa maana kwa njia ya Nguvu za Roho Mtakatifu, kwa njia ya Mwanangu Yesu Kristo wa Nazareti, na kwa njia Yangu Mimi, ndipo mahala mtazamo wenu unapotakiwa kulenga, siyo kwenye mambo ya kidunia na raha zake na njia zake za dhambi. Kwa maana hivyo vitawapatieni shimo kama hamtamgeukia Yesu wa Nazareti. Inawabidi mkaharakishe kwa maana muda uliopangwa unazidi kukaribia kwa kadiri siku zinavyoyoyoma.

Pamoja na Upendo Moyoni Mwangu, Upendo Midomoni Mwangu, pamoja na Mikono Yangu iliyofunguliwa, Njoni Kwetu mbinguni, kwa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Nanyi mtapata Wokovu, geuzieni migongo yenu dhambi, na kukimbia kwa kasi iwezekanavyo, kwa maana Mikono ya Baba yenu iko wazi wakati wowote ambako mtaamini kwa dhati, ndani ya mioyo yenu, katika Jina la Mwanangu Yesu wa Nazareti. Kwa maana Yeye ni Mwokozi wenu. Kwa maana Yeye alikufa kwa ajili yenu. Yeye alishinda Mauti kwa milele yote, mgeukieni Yesu wa Nazareti, na mwanzo wa Amani ya kudumu utaanza baada tu ya mapambano kwenye bonde lile. Hivyo asemavyo Yehova, Muumbaji, Mvunjaji wa Ulimwengu, wa yote yale yaliyoko, na yote yale yatakayokuwa, Neno lile la Mwanzo, na ni Neno la Mwisho.

Baba wa Mbinguni Mimi sihitaji lolote ila tu kile ambacho ni Kisafi, Kilichotakata, Moyoni, Adilifu, kilicho Kizuri bila ya Mawaa.

Kwa hiyo tubuni. Ungameni dhambi zenu. Ni rahisi. Ni moja kwa moja. Ni njia ya kwenda kwa Yesu Kristo, Mwanangu.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.