83. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 10 Juni 1992 saa 8:01 usiku Jumatano katika lugha na Kihispaniola.
Kwanini? Kwanini? Kwanini? Vile vitu unavyotaka vinakuwa vya maana kuliko Mungu wako, Mungu wa Mbingu, wa Dunia, wa Nyota zote, na wa kila kitu kilichoko, na kitakacho kuwapo? Watu wa Dunia watakuja kuamka siku mmoja lakini watakuwa wamechelewa, kwa sababu shetani atakuja na atawala vichwa kwanza. Kwa maana hawakunisikia kwa Masikio yao. Siku ile niliyosema nanyi, miaka, miaka na miaka iliyopita kwa Baba zenu, na kwa Baba wa Mababa zenu, imeanza!
Ni aibu gani! Ni aibu gani! Mnafikiri zaidi mali zenu, nyumba zenu, magari yenu, marafiki wenu wa Kiume, marafiki wenu wa Kike, Waume wenu, wake zenu, wana wenu wa kike na wa kiume kuliko Mungu wenu. Ni aibu gani!
Ninayasema hayo kwa upendo utokao Moyoni Mwangu ukipitia kwenye Midomo Yangu. Nawaambia kwa njia ambayo mtanielewa. Kwa Upendo wa Moyo Wangu Nawapenda, pamoja na Mwanangu, Yesu Kristu pamoja na Roho Mtakatifu. Mnisikilize Mimi! Huyu ni Baba yenu. Ninawaambia kwa upendo ule niliokuwa nao nilipo waumbeni, nilipoumba Dunia, Nyota, na kila kitu unachokiona na unacho kigusa, lakini muda umewadia. Najua kuwa hamniamini Mimi, Najua kuwa hamtamwamini Reymundo. Najua mioyo yenu migumu ni kama jiwe. Mioyo yenu hiyo ya migumu kama mawe utawapatia mahala pale niliyo iumba kwa ajili ya Shetani.
Iko hapa. Hiyo ni yote nitakayo sema. Nimewaambia kwa miaka, miaka na miaka, lakini hamnisikilizi. Hamnitafuti Mimi. Mnaweka hayo maneno matamu midomoni mweni lakini mioyo yenu ni migumu kama jiwe. Ni aibu gani kwani Mimi naenda kusafisha kila kitu kilicho kichafu.
Huyu ni Baba yenu anayesema maneno hayo kwa Upendo, kwa maana Mimi ndiye lile Neno lililofanya kila kitu, Dunia na Nyota. Nitamwambia Mwanangu Yesu asafishe kila kitu na asiache chochote. Narudia kusema tena! Asiache chochote kilicho kichafu. Nilicho nacho ni kisafi na kilicho nyooka.
Haijalishi kama unaamini kuwa Mchungaji wako atakuokoa, au Malaika yule unayemwomba, au mama yako, au baba yako au fedha zako, au gari lako, au au nyumba yako. Mimi nitamwambia Mwanangu, kile tu anachokipenda, ambacho ni kisafi, kiingie milango ya Mbinguni, kwa sababu Mwanangu ni Sheria na anafanya kile ninacho mwambia Mimi.
Hivyo ndivyo Wana wa Kiume wanavyotakiwa kuwa kwa Baba zao. Hivyo ndivyo Baba alivyo kwa Mwanawe Yesu Kristo. Wawili hawa ni wamoja katika Mawazo na Roho. Mwanangu alikufa kwa ajili yenu, lakinininyi bado hamtaki kubadilisha Mioyo yenu. Miaka mingi imepita sasa lakini ninyi bado hamjabadilika kimawazo na kiroho. Yote mnayo waza ni fedha na vitu ambavyo mnataka kuvipata. Mtakachopata ni mahala pa pamoja na Shetani, mungu wenu. Sintangoja zaidi kwa sababu nimekwisha wapa nafasi na fursa ya kutosha ya ninyi kuja Mbinguni pamoja Nami. Watakatifu wale ambao wanani tafuta watakuja pamoja Nami Mbinguni na kukaa nao kwa muda wote ambao kuna muda, kwa sababu niliwapa Neno Langu: "Yakuwa kama Watanitafuta Mimi, Mimi nitawaokoa."
Kwa walio salia, Inaniumiza Moyo Wangu kwa sababu nitawapoteza wao. Kwani niliwapa muda lakini wao waliamua kukimbia na mungu wao ambaye ni Shetani, na wanaamini kuwa wanajua mengi sana. Watakuja kushangaa kwa sababu siku inakuja ambayo Mimi nitakifunga Kitabu cha Uzima.
Kisha Mwanangu atawaita nakuwauliza "Je, mlifanya nini ili kumsaidia Baba Yangu kusafisha dunia hii?" Itawabidi mseme kweli kwa sababu Yeye anaweza kusoma Mioyo yenu, Mawazo yenu, na roho zenu. Na atakacho waambia itabidi mkitekeleze. Akikuambia hutaenda Mbinguni, hutaenda. Hicho ndio kitu pekee kilichopo! Hivyo ndivyo itakavyo kuwa.
Huyu ni Mungu wako, Baba wa Mbinguni, wa yote yaliyoko na yatakayo kuwapo. Nimechoka sasa na nikiwa na machozi Machozi machoni Mwangu. Wakati umefika ambako kitabu kitafungwa kuhusu Dunia hii. Sitawaambia siku ila iko hapo mbele ya pua zenu. Hayo ni yote yale ambayo Baba yenu atawaambia na Reymundo Wangu kwa tarehe hii ya leo. Ila angalieni, itabidi MFUNGUE MACHO yenu, pamoja na MASIKIO yenu, kwa sababu Reymundo hawezi kuwasaidia!
Hakuna anayeweza kuwasaidia ila Kristu, Roho Mtakatifu, na Mimi Baba yenu. Kumbukeni hayo kwa maana Mwanangu Reymundo ni Neno Langu tu. Mungu wenu ni: Kristu, Roho Mtakatifu, na Baba yenu. Je, mmenisikia Mimi? Hayo ni yote, nitawaambia kwa furaha kubwa. Huyu ni Baba yenu. Huyu ni Baba yenu na Neno lililo nyooka. Mnisikilize Mimi! Mnisikilize Mimi! Mnisikilize Mimi!
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )