92. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 15 Juni 1992 saa 8:15 usiku wa siku ya Jumatatu katika Lugha za Kihispaniola na Kiingereza.

Kihispaniola:

Wajua nini? Siku hii ya leo ilienda vizuri sana kwao. Unajua ulifanya nilichotaka ufanye na ulipumzika. Najua kuwa ulichoka sana kwa sababu ulikuwa unafanya kazi kwa juhudi kubwa kwenye kuandika Unabii. Angalia kitakacho fanyika katika siku za usoni. Itakuwa ngumu, ngumu sana kwa wale wanojua nini kitafanyika, lakini itabidi kifanyike.

Kutakuwapo na jasusi (Mwanamke), na watamtupa katika shimo. Shimo lile litamla yule Mwanamke kwa sababu mume wake atakasirika sana, kwa sababu jasusi lile halikuwa kwa ajili yake. Kitendo hicho kitamkasirisha kiasi ambacho yule mtu ataenda kufanya mambo mabaya kwa yule mtu ambaye amemtupa kwenye shimo, hata hivyo kumbe aliyemtupa kwenye shimo hilo ni Shetani mwenyewe. Na mtu yule alikuwa hajui hilo.

Angalia, mtu huyo ndiye yule mtu atakaye kuja kusema Maneno ya Uwongo kuhusu Maneno ya Mungu, siku atakapoanza kutumia ulimi wa shetani. Shetani atakuja kumla. Siku hiyo yeye na shetani watakuwa kitu kimoja. Kwa maana yeye atajiona kuwa ni mtu wa maana sana na anapenda sana fedha. Anapenda kuwaamuru watu kufanya hivi na kufanya vile, lakini Mungu wa Dunia na wa Mbingu, na wa yote yale yaliyeko na yatakayekuwapo, mtu yule pamoja na shetani watatupwa shimoni (Jehanamu). Katika shimo hilo, Yeye atamzika huko kwa namna ile ambayo kamwe hataweza kutoka huko. Kwa maana yeye alitumia neno la shetani. Ooh ni aibu gani. Ooh ni aibu gani.

Kiingereza:

Nataka wewe utege sikio, usikilize kwa makini Maneno Yangu. Huyu ni Yehova, Muumbaji wa Dunia na wa kila kitu kile kilichoko na kitakacho kuwapo, pamoja na Mwanangu Yesu Kristu wa Nazareti, na Roho Mtakatifu. Muda huu ambao tunaukaribia ni Muda wa kuagana na nyakati zile nzuri sana mlizokuwa nazo za kupumzika. Mwanzo wa mwisho umekwisha anza; ingawa hamjatambua bado, lakini saa imekwisha anza kuhesabu. Desemba 2, 1990 ilikuwa siku ya kwanza, siku ya tarehe hiyo; ilianza wakati ambako Mwanangu alianza vita vya kumaliza kusafisha kila kitu kilichokuwa kichafu Mbinguni.

Sitakuambia siku wala tarehe ambako Mwanangu atarudi kuwachukueni; ila tu nawaambia kuwa vita huko Mbinguni vinazidi kuwa vikali sana; tokea siku ile ilipoanza. Vita vinaendelea katika Sayari ya Dunia na wakati huo huo katika Ulimwengu wa Kiroho. Mtaona mambo yakibadilika. Mambo mengine yatabadilika haraka sana. Mambo mengine yatabadilika pole pole, lakini mambo yatabadilika kiasi cha kuwastusha ninyi, maasi, mapambano kati ya baba, mwana, mke, na binti. Watu watakuwa kwenye kikomo cha uvumilivu na kuwa kwenye uwanja wa machinjioni au wa machafuko. Maafa za kiasili zitatokea kwa wakati usiootegemewa na mahala zisizotegemewa.

Hizo ni utungu wa uzazi wa mwisho wa nyakati. "Wakati majani ya mtini yatakapobadilika;" kumbukeni usemi huo. "Wakati majani ya mtini yatakapobadilika," Itakuwa alama ya mwanzo na mwisho wa yote yale mtakayo kuwa mnafahamu au mliyokuwa mnafahamu. Kwa maana alama ya ishara za Mnyama zimefika. Nabii wa uwongo amefika. Ishara ya kila kitu kilicho andikwa kwenye Biblia kitaanza kuonekana mbele ya macho yenu. Kama hampo ndani ya Neno hayo yote wala hamtaziona zitakapokuwa zinatokea. Kwa hiyo nawaambia Wakristo Wangu, Watakatifu Wangu, mnakaribia kwa kasi wakati wa taabu na dhiki.

Watakuwapo Manabii fulani ambao watakuja kuwaambia mambo fulani fulani ambayo hayatakuwa mazuri sana, ambayo siyo matamu kiasi cha kutokutekenya masikio yenu, kwa sababu wakati wa kutekenya masikio umepita. Wakati wa kujitayarisha kwa ujio wa Mwnangu umefika. Naenda kufanya ukaripiaji kiasi, usafishaji kiasi. Wa kila kitu ambacho hakiendi sawa sawa na Neno Langu, Sitajali, JINSI unavyoisoma Biblia ile, na JINSI unavyoitafsiri Biblia ile, kwa maana kuna Neno Mmoja tu, na hilo ni Neno Langu, Mimi Yehova. Sikiliza Maneno Yangu. JEHOVA ANA NENO MMOJA, NA NENO MMOJA TU.

Ninyi Wanatheologia, ninyi Wachungaji ambao mmewapeleka Kondoo Wangu mbali na ukweli na kuwapeleka kwenye njia ya upotevu, mtawajibishwa. Siyo kwamba nawauliza. Bali Mimi ninawaambia. Mnatakiwa kunyoosha mambo yenu sasa hivi! Kwa sababu siku ile iliyoelezwa katika Biblia inawaangalia usoni. Kama hamta jifunga vibwebwe sasa hivi!, mtawajibika kwa kila kitu mlichokifanya kuwazuia Wanangu, Watakatifu Wangu wasisikilize Neno Langu kwa wakati uliotakiwa na kwa mahali ilipotakiwa.

Mnapenda kuwawajibisha Kundi lenu kwa njia na namna ambayo inalingana na Neno Lenu na Theologia yenu. Sasa!, ni zamu na wakati Wangu wakuwakaripia ninyi, kuwarudisha katika nafasi zenu. Kwa maana kizuizi pekee iliyobaki ni mfumo na tabaka la Kanisa. Ambayo iliisambaratisha na kukatakata Mwili wa Kristu kwa jinsi ambayo kumekuwa na msururu usio hesabika wa vidini ambavyo vinaenda kwa Jina la Mwanangu Yesu Kristu. Hamuelewani; wala kupendana. Wala hamsemezani. Mnadharauliana. Ninyi Wachungaji ni wabaya kuliko Watoto wenyewe kwa wenyewe. Badala ya kuungana na kupigana kwa sababu na kwa nia mmoja na kwa Neno mmoja, mapambano yamekuwa kati yenu ninyi kwa ninyi.

Kwa hiyo jihadharini, kwa maana tatizo halipo kwa Kundi (kondoo). Tatizo liko kwa Uongozi wa Kundi (Kondoo). Najua haya siyo maneno ya ukarimu. Najua haya siyo maneno matamu. Najua hayatekenyi masikio yenu kwa muda huu, lakini na iwe hivyo.

Nilisema Neno kwa Mwanangu Miaka maelfu iliyopita na ninyi mlipewa Neno hilo na ninyi hamlitii Neno Langu. Kwa hivyo mtaona vitu fulani fulani vikitokea siku za usoni. Kwa Wachungaji na Viongozi wa Kundi Langu, kwa njia ya Jina la Yesu Kristu wa Nazareti, kwa njia ya Roho Mtakatifu ambao HAWATII NENO LANGU, HASIRA YANGU ITAWAANGUKIA JUU YAO. Siyo kwa Kundi (la kondoo), kwa maana wao wanawajibika kwa Kundi na wanatakiwa kutoa hesabu ya kazi yao ya kuchunga Kundi.

Haya siyo maneno matupu ya mwenda wazimu fulani, kwa maana Nabii Wangu huyu anaongea Neno langu hivyo usithubuti kwenda kinyume na Neno Langu. Kwa maana kuna mahala palipo ruhusiwa kwa watu wanaoenda kinyume Changu Mimi. Je, mnaelewa ninacho sema? Je, mnatambua uzito wa yale niliyoyasema sasa hivi?

Nitasema tena. Nyoosheni mambo yenu sasa hivi! Safisheni matendo yenu. Leteni Mwili wa Kristo pamoja LEO! UMSILIJADILI! NATAKA ITEKELEZWE LEO! Kwa maana Hasira ya Mungu, Yehova, itawaangukieni kwa nguvu kiasi ambacho itawafanya vichwa vyenu vipatwe na kizunguzungu na hamtayatambua hayo. Imekaribia sana, kwa maana mkingojea kesho, kesho hiyo mnayoigojea hamtakuwa nayo.

Huyu ni Mungu wenu Yehova. Muumbaji wa Ulimwengu, wa kila kitu kilichopo na kitakacho kuwapo. Neno la kwanza, na la mwisho. Nendeni mitaani, hubirini Neno Langu, siyo kwa magari yenu ya kifahari, bali kwa miguu yenu, kwa miguu yenu, kwa miguu yenu, mtu kwa mtu, mlango hadi mlango. Sitajali jinsi mtakavyofanya. Mmekuwa mkistarehe. Muda huo wa kustarehe umeisha, wahudumieni wagonjwa Wangu, wahudumieni Watoto Wangu wenye njaa. Kwa maana unachowafanyia hao mnamfanyia Mwanangu, na mnanifanyia Mimi. Huyu ni Yehova. Huyu ni Yehova. Huyu ni Yahwe. Huyu ni Yahwe. Huyu ndiye yule Mimi Ndimi, Mimi Ndimi, Mimi Ndimi. 

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.