100. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 19 Juni 1992 saa 6:26 usiku katika lugha za Kihispaniola, na Kiingereza.

Kihispaniola:

Mwendawazimu. Yeye ni Mwendawazimu. Yeye ni Mwendawazimu. Mtu yule. Yeye ni Mwendawazimu kwa sababu, ana amini kuwa anaweza kumshinda Mungu. Ana amini kuwa anaweza kumua Mungu, iwapo atawaua wale wanaomwamini Mungu. Ni Mwendawazimu. Ni Mwendawazimu. Ana hasira sana amemkasirikia sana Mungu kwa sababu shetani alimwambia kuwa kila kitu kibaya kilichomtokea wakati wa utoto wake kimesababishwa na Mungu. Na sasa anataka kumua kila mtu anayempenda Mungu, Mungu wa Dunia, wa Mbingu, wa kila kitu kilichoko na kisicho kuwapo.

Hivyo ndivyo itakavyokuwa katika siku zinazokuja. Inabidi uandike ili kuwataarifu Watakatifu kuwa waweke masikio yao ardhini. Ili kusikia mshindo wa nyayo za mtu yule, ambaye ni Mwendawazimu. Kwa sababu atakwenda kutaka kuua kila kitu kilicho na imani katika Kristo, na Roho Mtakatifu, na katika Baba.

Anakwenda kuwa na askari wengi sana, ambao watamsaidia kuwatafuta wale wanaoamini katika Kristo, na kama hawataacha kusali na kusoma Biblia, atakwenda kuwaua Wakristu kama wanyama, kwa sababu anahasira nyingi, nyingi sana, kwa Mungu, kwa sababu shetani anamwambia mambo. Ni aibu gani, kwa yale yatakayotokea katika siku zinazokuja.

Kiingereza:

Nakwenda kukupa ushauri wa upendo. Ushauri huu unatoka kwenye Mdomo wa Baba yenu wa Mbinguni Yehova. Kwa maana Yehova ni mwanzo wa kila kitu. Ushauri huu ni kwa ajili ya Wakristo ambao itabidi wavumilie misiba fulani, ambayo itawakumba hapo baadaye wakati ambapo itabidi wateswe. Ushauri huu kimsingi ni mrahisi: Mwangalie tu Yesu Kristu, Mwokozi wako kwa njia ya nguvu ya Roho Mtakatifu. Utaokolewa iwapo utajiweka kuwa msafi (kiroho) na kuweka matumaini yako yote kwa Yesu Kristo.

Kwa maana wakati Mpira utakapo julikana (kinyago cha mpinga kristo ambacho ataagiza kiabudiwe), mpira utaanza kuacha Muhuri wa Msalaba wa Balaa kwenye mpira, na katika mwili na katika Mwili wa Kristo. Kwa maana Muhuri wa Msalaba wa Balaa utatekelezwa kwa wakati muafaka. Kwa maana shetani atakuwa na alama yake kwa maana muhuri utamaanisha Mateso ya Milele Jehanamu.

Kwa hiyo mjihadhari na mhuri. Mjihadhari na Mnyama, kwa maana kuja kwa ule mwisho umewadia, na utawafikieni ghafla kabla ninyi hamjatambua. Mbingu ipishilie mbali; kwa mtu yeyote yule, atakaye chukua muhuri huo, kwa maana hiyo alama itafunga imani yake na matakwa yako ya kwenda Jehanamu. Mjihadhari, mjiweke imara, katika kujua Neno. Someni Biblia. Wekeni umakini na matumaini yenu kwa Yesu. Roho Mtakatifu atawaongoza. Huyu ni Baba yenu, Muumbaji wa Ulimwengu, Yehova. 

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.