101. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 19 Juni 1992 saa 7:49 mchana siku ya Ijumaa katika lugha ya Kiingereza.
Hasira yako itakuja kupoa pale Roho Mtakatifu atakapo kuwekea ile cheche ndani ya Moyo wako. Kisha uta elewa utaelewa ni nini Nabii wangu anacho kifanya. Jinsi anavyo fanyakazi ili kukamiliha kile ambacho ni lazima kitekelezwe. Mweke kwenye maombi yako. Msaidieni kama mtaweza, kwa maana watoto wangu ni lazima waungane. Inabidi kuleta mwili wa Kristu pamoja kwa maana wakati wa majaribu na wa dhiki kuu umewadia.
Inabidi tuanze mara mmoja. Inabidi tuwaongoe majirani zetu. Inabidi tuwaongoe Kaka zetu na Dada zetu, kila mmoja, kila mtu anaye sikiliza. Huyu ni Yehova, Baba yenu, Muumbaji wa Mbingu na Dunia. Mnyama anakusanya utajiri na Habari kwa wakati huu kwa maana Mnyama hana wakati wa kungoja hata nukta, ili kutimiza kila alicho amua kukikamilisha. Anaweka masaa mengi sana kwenye kazi yake kwa muda huu.
Kwa hiyo Mwili wa Kristo, sikilizeni Unabii huu na muangalie, na mjifunze kwa maana mtakuja kustushwa kwa jinsi ambayo hali ya mambo itakavyo kwenda, kwa maana wakati wa kusambaratika kwa sheria kumewadia, wakati wa kusambaratika kwa utaratibu umefika, kwa maana wakati wa kuanguka kwa haki zenu umefika, kwa maana wakati wa kuanguka kwa amani umefika, kwa maana wakati wakuanguka kwa utulivu umefika, kwa maana wakati wa kuanguka kwa Shetani umefika. Kumbukeni ninyi wenye Mioyo misafi, akili safi, na Nafsi safi, wekeni macho yenu na umakini wenu kwa Yesu.
Kwa maana yeye ni Mwokozi wenu. Yeye ni wokovu wa kila kitu kile kilicho Kisafi na kinyofu. Roho Mtakatifu atawaongoza katika kila hatua ya njia. Inabidi mjifungue na kuwa tayari kwa kuelekezwa. Kwa maana kuelekezwa haitakua na maendelea kama hamkubali Yesu Kristo wa Nazareti kuwa Mfalme wenu wa Wafalme, na Bwana wenu wa Mabwana kwa undani kabisa; wa Mioyo ya Nafsi zenu na wala siyo tu kijuujuu kwenye midomo yenu. Kwa maana kukiri kwa midomo yenu pekee haina maana kabisa.
Kwa hiyo, msikilize kwa makini Watakatifu Wangu, na muendelee kusoma Unabii kwa maana Unabii huu utazidi kuwa mzito zaidi, na wa huhakika zaidi, kwa maana niliwahidi Watakatifu Wangu kuwa; ningeliwaonya wao kabla ya ule mwisho, kwa hiyo kwa wale wengine wenu mulio na Roho safi, akili safi, na nafsi safi, wale wanaotafuta njia ya kwenda kwa Mungu wenu Yehova, Muumbaji wa Mbingu, na Dunia na wanaotaka kujiokoa wenyewe kutoka kwenye mwanguko, ule mwanguko mkuu, mateso makuu, dhiki kuu amabyo itaiangukia Sayari hii, sikilizeni, someni na mjifunze Biblia. Watafuteni Kaka na Dada zenu na muisome.
Someni kana kwamba maisha yenu yote yanategemea hicho. Kwa maana kila dakika unapokuwa ndani ya Biblia unakuwa karibu mno na Mimi Yehova. Inabidi mniamini Mimi. Inabidi mniamini kuwa nitwaokoa ninyi. Najua itakuwa vigumu lakini mnaweza kufanya hivyo. Kwa maana Mimi sitaki chochote ila kilicho Kisafi, Kinyofu na kilicho takasika. Kwani nilishaeleza hapo kabla kuwa vyumba vyenu viko tayari. Viti vyenu, vile mbavyo mnavipenda sana sana, vinawangojeeni kule Mbinguni.
Kwa hiyo muwe na imani katika Yesu Kristo wa Nazareti. Roho Mtakatifu ataaongozeni a kila hatu ya njia ya ile safari yenu, lakini inawalazimu msikilize. Msikilize kwa makini sana kwa maana mambo ya kuvuruga mawazo yenu hapa duniani yataongezeka kwa kasi kubwa sana, kiasi ambacho hamgeliweza kudhania kamwe. Kama kuna tamaa ndani ya mioyo yenu, ndani ya mioyo yenu hiyo midogo, Mimi naenda kuijenga na kuifanya yaelekee upande wa Yesu.
Yeye atawaonyesheeni, lakini inabidi ninyi muwe tayari kufanya na kuendeleza wenyewe, kwa maana Mimi ninachotaka tu ni wale ambao kwa hiari yao wanataka kweli kuja; wale walio imara wale walio na upendo; wale wanaowasaida Kaka na Dada zao, wale ambao wanajaribu kwa hali na mali kuleta Ulimwengu wa Yesu Kristo kwa Ulimwengu huu.
Mimi nitawachungebi ninyi. Nitawalinda ninyi. Kwa maana ninawapenda kwa Moyo Wangu wote. Huyu ni Yehova, Muumbaji wa Mbingu na wa Dunia, wa kila kitu kile kilichoko na kitakacho kuwako, Yeye ni Ukweli, nani Ukweli mtupu. Kwa maana Mungu wenu ni Ukweli na kilicho cha Ukweli ni Kinyoofu, kilicho cha Ukweli na kilicho Kinyoofu ndicho tiketi zenu ya kwenda Mbinguni. Hivyo ndivyo asemavyo Yehova pamoja na Mwanangu Yesu Kristu wa Nazareti pamoja na Roho Mtakatifu.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )