1118. Occurrence given to Raymond Aguilera on 20 October 1997 at 12:30 PM.

I would like to share a few things that happened this week. After doing some running around, I came home and I approached my front door. I noticed a very strong odor that smelled like women's perfume. The first thing that came to my mind was, "We have a woman visitor." But as I walked inside the house, I found the house was empty. There was no one to be found. But near the front door in a circular area of about 10 feet inside of the house, it smell like a perfume factory. But as I walked away from the front door, the perfume scent seemed to get less and less. So I walked back toward the front door and the perfume scent was so strong - one could almost taste it. Your whole body seemed to be able smell it or taste it. I don't know how else to describe it. It smelled like flowers. I even walked back to the front door to smell it to see if someone had poured some perfume on the door, but the front door smell did not have any perfume scent! So then I checked all of the furniture without success. Only near the front door in an circular area of 10 feet was where this Wonderful Scent seemed to be! It seemed to go up into the ceiling. I wish - I could describe it better, but I do not know how else to explain it!

A few minutes later, I told Ron about it, but my mind tried to make some kind of sense of it and figured my daughter or granddaughter had just spilled something. Ten minutes later my daughter came home, and I asked her what she spilled in the living room. She said, she didn't know anything about it, for she had been gone all morning. Then I suddenly realized Scent was TOTALLY GONE!

Then two days later, at almost the same time, the perfume Scent came back and left just as fast, but this time, I had enough time to run downstairs to get Ron. By the time we came back it was almost all gone except for a small amount of it. Very, very strange

1118. Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 20 Oktoba 1997, saa 6:30 mchana.

Mimi ningelipenda kuwashirikisha tukio fulani la aina yake iliyonitokea wiki iliyo pita. Baada ya kukamilisha shughuli za kukimbia kimbia hapa na pale mimi nilirudi nyumbani nami nikajongelea malango wa mbele wa nyumba yangu. Nilipokua karibia mlango huo nilianza kuhisi harufu kali sana ya manukato ambayo ilikuwa inasikika kama harufu ya manukato ya mwanamke. Kitu cha kwanza kilicho nijia kwenye mawazo yangu ilikuwa ni, "Tuna mgeni wa kike hapo." Lakini jinsi nilivyo tembea ndani ya nyumba, mimi niligundua nyumba ilikuwa iko tupu. Hapakuwa na mtu yeyote kule ndani. Lakini karibu na mlango wa mbele katika eneo la mduara au mviringo wa futi 10 ndani ya nyumba; palikuwa pananukia kama kiwanda cha manukato. Lakini nilivyo jaribu kutembea kutoka mlango huo kwenda zaidi ndani manukato hayo yakawa yanapungua ukali wa harufu. Kwahiyo mimi nikarudi kuelekea kwenye mlango wa mbele na hiyo harufu ya manukato mara ikaongeza ukali wake kiasi ambacho – unaweza hata kuuonja. Mwili mzima unaweza kuunusa au kuuonja. Mimi sijui njia nyingine ya kuielezea. Ilikuwa inanukia kama maua. Mimi hata ikafikia mahala nikaenda kunusa mlango wa mbele kujua kama kuna mtu labda kamwaga manukato kwenye malango huo, lakini mlango wa mbele haukuwa na manukato hayo! Kisha baada ya hapo mimi nilienda kunusa samani yote ya humo ndani bila ya mafanikio ya kujua ilipokuwa inatokea hiyo harufu. Ila harufu hiyo ya manukato hayo ya ajabu ilikuwa inaonekana kutokea kwenye eneo la mviringo wa futi 10 karibu na mlango wa mbele! Ilikuwa inaonekana kwenda hadi juu kwenye dari la nyumba. Laiti kama ningeliweza – kuwa na njia nyingine ya kuilezea vizuri zaidi hali hiyo, lakini mimi sijui njia nyingine ya kuielezea vizuri zaidi!

Dakika chache baadaye, mimi nilimwambia Ron kuhusu jambo hilo, lakini akili yangu ilijaribu kutafakari na kuwaza kuwa labda ni manukato ya binti yangu au labda mjukuu wetu kamwaga kitu fulani pale. Dakika kumi baadye binti yangu akawa amerudi nyumbani nami nikamwuliza alimwaga nini pale sebuleni. Yeye akajibu kuwa yeye hafahamu lolote kuhusu kitu kilicho mwagwa au kumwagika pale sebuleni kwa maana yeye alikuwa ametoka nje ya nyumba yetu hiyo kwa asubuhi yote ya siku hiyo. Kisha mimi nikatambuka kuwa ile harufu ya manukato ilikuwa IMEKWISHA ONDOKA YOTE!

Kisha siku mbili baadaye, na karibia na wakati huo huo, ile harufu ya manukato mara ikaja tena na kuondoka kwa haraka kama ilivyo kuwa hapo awali, lakini safari hii, mimi nilipata nafasi ya kukimbia mpaka ghorofani ili kumwite Ron. Lakini hadi tulipo fika pale mlangoni sehemu kubwa ya harufu hiyo ilikuwa imeondoka, lakini bado kulikuwa na kiasi kidogo cha harufu ambayo imebakia pale. Ni kitu cha ajabu sana sana.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.