|
1234. Occurrence given to Raymond Aguilera on 12 February 1999 at 10:00 PM. Carl G., and old friend in Christ, telephoned me and asked if Ron V., and I could come over for dinner and prayer. I was not really sure if I wanted to go for all the warfare I had been having and my back was still hurting. I felt very tired, but I said yes, and after Ron took a shower we left for Carl’s house. As soon as I climbed into my car I started to become very sleepy. The closer we got to Carl’s house the sleeper I got. Ron and I sat around while Carl fixed our dinner. I got so sleepy I had to ask Carl if he had a soft drink with some caffeine. He said he did not. I usually try to stay away from soft drinks, but I knew if I did not get something in my body with something to keep me awake I would fall asleep on this couch. I tried eating an orange and kept myself walking and moving just to keep myself awake, but nothing helped or worked. So I had to tell Carl I had to leave and go to the store and get a soft drink with some caffeine (I do not drink coffee). He and Ron looked at me sort of strange and surprised, but I knew I had to do something. After returning from the store, Carl served dinner and during dinner my sleepiness began to leave me. Then after eating, we had Communion and prayed. Carl wanted to ask the Lord about the planting a new Vineyard church in Berkeley. He goes to a Vineyard Church in San Francisco and his church was moving to another location in San Francisco within weeks. So Carl wanted to ask the Lord if it would be alright to start a new Vineyard Church in Berkeley which is on the other side of the San Francisco Bay where Carl lives. The following was the Lord’s response to our prayers. Praying about the new Berkeley Vineyard church plant: Vision: The gave me a vision of a gravestone which was leaning to one side with one or two flowers placed in a clear vase in front of the gravestone. During this vision I was given a sense of the words, "An old death". Then the Lord said, "You have to die to yourself". Then the Lord gave me a vision of an electric toothbrush. This seemed to mean to me that one had to clean ones mouth or what comes out of ones month. Ron, Carl and I, discussed some of the following scriptures: Mat 15:11 What goes into a man's mouth does not make him 'unclean,' but what comes out of his mouth, that is what makes him 'unclean.'" Mat 15:17 "Don't you see that whatever enters the mouth goes into the stomach and then out of the body? Mat 15:18 But the things that come out of the mouth come from the heart, and these make a man 'unclean.' Mat 15:19 For out of the heart come evil thoughts, murder, adultery, sexual immorality, theft, false testimony, slander. Mat 15:20 These are what make a man 'unclean'; but eating with unwashed hands does not make him 'unclean.'" Luke 6:45 The good man brings good things out of the good stored up in his heart, and the evil man brings evil things out of the evil stored up in his heart. For out of the overflow of his heart his mouth speaks. When we prayed for the San Francisco Vineyard church: Vision: The Lord gave me a vision of a large white sheet being held at each of the four corners and there was a big black ball in the center of the white sheet and the black ball was being thrown up and down by whoever was holding the white sheet from it’s corners. Then we began to pray for other things on our prayer list: Vision: The Lord gave me an image of a clean White Beach with a White Candle in the air over the White Beach. Then the Lord said, "Go to the Beach!" (The White Candle represented Jesus standing over the Beach or the Body of Christ.) This made me think of the scriptures about the sand: Gen 22:17 I will surely bless you and make your descendants as numerous as the stars in the sky and as the sand on the seashore. Your descendants will take possession of the cities of their enemies, Gen 32:12 But you have said, 'I will surely make you prosper and will make your descendants like the sand of the sea, which cannot be counted.'" Then this White Candle changed into Jesus Christ walking along the sand. At one point I could see His foot steps make impressions on the sand. Each grain of sand was a Christian. The Lord was showing me that these foot impressions were His callings on individual believers or the burdens He had placed on believers carrying their cross. By Him making the foot impression on the grains of sand, also meant He was their covering. Then Ron mentioned the scripture: 2 Tim 3:12 In fact, everyone who wants to live a godly life in Christ Jesus will be persecuted, 2 Tim 3:13 while evil men and impostors will go from bad to worse, deceiving and being deceived. So we continued to pray; then the Lord said: Prophecy: I am going to turn this world inside out and kick it like a football. I am going to bury man’s church like that grave I showed you earlier, and you are going to wish you had a flower to place on it. Most of the Body of Christ thinks I am playing games, but the players have their scripts. The things are ready for the coming of the hammer and the sickle. The day of theology is finished! The day that the blood flows in the streets is here! The army in Heaven is prepared! The army on earth is getting ready. At this point we stopped praying for the whole atmosphere of our prayer time dramatically changed and we stopped our prayer. As the three of us discussed the above, Carl sensed we should proceed praying for our personal needs. Then the Lord said to me, "Do you want to hear some more! Neighbor will betray neighbor. Mother will betray child. Parents will eat their children for food. Some of you will wish that you were dead, but I will not let you die. The Ark of the Covenant is ready! The hammer and sickle are ready! The fall of Babylon is ready! But that’s enough for tonight!" This really shocked us, for we wanted to pray for our personal needs, and the Lord spoke about the end times. The above hit me very hard, for I remembered telling the Lord that if I kept delivering messages like the one above, people were going to call me a doomsday prophet. The Lord relied, He did not care what names they called me. Only to do what He told me. My problem was that I not only could see these things, but I could at times feel the pain of what I was seeing. So at that I told my brothers in Christ, I did not want to pray anymore. But my brother Carl did not want to stop. He still wanted to ask the Lord about the personal things. But I told him again I did not want to pray anymore. But he still wanted to. So we began once more to pray for the personal needs. So the Lord said to me, "Since you want to hear some more!" Then the Lord began once more showing me visions. Vision: The first vision was of people being burned alive. This shocked me even more than what the Lord had revealed before. I felt like crying and leaving the room. Vision: Then the next vision was of a hand held electric drill which was being used to drill out someone’s left eye. This was so vivid that I demanded the brothers to stop praying for I could not take anymore of what I was seeing. So we stopped, but later we did pray over Ron’s ears and the Lord did not give me anymore end time visions. (over)
|
1234. Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 12 Februari 1999, saa 4:00 usiku. Carl G., na rafiki yetu wa siku nyingi katika Kristo, alinipigia simu na kuniuliza kama Ron V., pamoja nami tunaweza kwenda kwake kwa ajili ya kujumuika naye kwenye chakula cha jioni pamoja na maombi ya pamoja. Mimi sikuwa na uhakika kama nilikuwa napenda kwenda kutokana na mapambano yote niliyokuwa nayo na huku mgongo wangu ukiwa bado unauma. Mimi nilijisikia kuwa mchovu sana, lakini mimi nikasema ndiyo, na baada ya Ron kuoga tuliondoka naye pale kuelekea nyumbani kwa Carl. Mara tu nilipoingia kwenye gari langu nikaanza kusinzia. Jinsi tulivyozidi kukaribia nyumbani kwa Carl ndivyo mimi nilivyozidi kulemewa na usingizi. Ron na mimi tulitulia pale tukiwa tunamgonjea Carl akiwa anatutayarishia chakula chetu cha jioni. Lakini kwa vile mimi niliendelea kubanwa na usingizia; nikaona nimwendee Carl ilikuomba kama ana kinjwaji chenye caffeine (aina ya kahawa). Yeye akasema kuwa hakuwa nayo. Kwa kawaida yangu mimi huwa na kwepa kunywa soda, lakini nilijua kuwa kama sitakunywa chochote cha kunifanya niwe macho; kuna hatari nitasinzia pale kwenye kochi. Nikajaribu kula chungwa na kutembea tembea huku na huku pale; ili kuzuia nisisinzie, lakini hilo nalo wala halikuweza kunisaidia. Kwa hiyo ikanibidi nimwambie Carl kuwa naenda kule dukani ilinijinunulie soda iliyo na kafeni. (Huwa kwa kawaida sinywi kahawa). Carl na Ron waliniangalia kwa mshangao na kunistaajabia, lakini mimi nilijua kuwa ni lazima nifachukue hatua hiyo la sivyo ningelisinzia hapo. Baada ya kurudi kutoka kwenye duka lile, Carl alituandalia chakula chetu cha jioni, na wakati tukila kula chakula hicho; mara usingizi wangu huo ukaanza kuondoka. Kisha sisi baada ya kula tulishiriki Chakula cha Bwana (Komunio) na kisha tuliomba. Carl alitaka kumwuliza Bwana kuhusu kama atapenda yeye kwenda kupanda au kuanzisha tawi jipya la kanisa la “Vineyard church” kule Berkeley. Yeye huwa anahudhuria na kusali kwenye kanisa hilo la “Vineyard Church” la pale San Francisco na kanisa hilo hivi sasa linahamia kwenye eneo lingine kule San Francisco katika muda wa wiki chache zijazo hivi. Kwahiyo Carl alitaka kumwuliza Bwana kama ni sawa kwa yeye kuanzisha tawi lingine la kanisa la “The Vineyard Church” kule Berkeley ambako ndiko anakuishi yeye na ambayo iko upande wa pili wa Ghuba hiyo ya San Francisco. Ifuatayo ni majibu ya Bwana kwa maombi yetu hayo. Maombi kuhusu uazishwaji wa tawi Kanisa la “The new Berkeley Vineyard”: Maono: Nilipewa maono ya jiwe la kuonyesha kumbukumbu la kaburi likiwa limeyumba upande mmoja na chombo ambacho ni angavu cha kuwekea maua kikiwa kimewekewa mbele ya jiwe hilo na likiwa na maua. Wakati wa maono hayo mimi nilipewa hisia ya maneneo yasmemayo, "Kifo cha kale". Kisha Bwana akasema, "Inakubidi ufe kwenye nafsi yako”. Kisha Bwana alinipa maono ya mswaki wa meno unao endeshwa kwa umeme. Maono haya yalikuwa yanaonekana kueleza kuwa mtu inamlazimu kupiga mswaki mdomo wake au kile kinachotoka kwenye mdomo wa mtu. Ron, Carl na mimi, tulijadili sehemu ya maandiko hayo: Mat. 15:11 Sikilizeni, mfahamu, Sicho kiingaacho kinywani kimtiacho mtu unajisi, bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi. Mat 15:17 Hamja fahamu bado yakuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni? Mat 15:18 Bali vitokavyo kinywani vya toka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi. Mat 15:19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uwasherati, uwizi, ushuhuda wa uwongo, na matukano; Mat 15:20 Hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi. Luka 6:45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake. Wakati tulipokuwa tunaomba kwa ajili ya Kanisa la “The San Francisco Vineyard church”: Maono: Bwana alinipa maono ya ya kitambaa cheupe kikubwa kikiwa kimeshikiliwa kwenye kila kona zake nne na mpira mweusi ulikuwa unatupwa juu na chini na huyo aliyekuwa akikishikilia kitambaa hicho cheupe kwenye kona zake. Kisha sisi tulianza kuwaombea wale wengine waliokuwa kwenye orodha yetu ya maombi: Maono: Bwana alinipa maono ya ufukwe wa pwani uliokuwa msafi ukiwa na Mshumaa mweupe uliokuwa unaelea hewani juu ya ufukwe huo. Bwana akasema, "Nenda Ufukweni!" (Ule Mshumaa mweupe ulikuwa unamaanisha Yesu akiwa amesimama ufukweni au Mwili wa Kristo.) Hili lilinifanya nikumbuke maandiko kuhusu mchanga: Mwa. 22:17 Katika kubariki nitakubariki na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za Mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani na uzao wako kama nyota za Mbinguni na kama mchana ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; Mwa 32:12 Nawe ulisema, hakika nitakutendea mema, nami nitaufanya uzao wako uwe kama mchanga wa bahari, usio hesabika kwa kuwa mwingi. Kisha Mshumaa huo Mweupe ukabadilika na kuwa Yesu Kristo; akiwa anatembea juu ya mchanga. Kuna wakati nilikuwa naweza kuona Nyayo za Miguu Yake zikiwa zinaacha alama kwenye mchanga huo. Kila punje ya mchanga huo ilikuwa ni mkristo. Bwana alikuwa ananionyeshea kuwa alama hiyo ya Nyayo Zake zilikuwa ni Mwito Wake kwa muamini mmoja mmoja au mzigo aliowawekea waamini waliochukua misalaba yao. Kwa kule kuacha alama za miguu Yake pale kwenye mchanga alikuwa pia anaeleza kuwa yeye ndiye kinga yao. Kisha Ron akataja maandiko haya: 2 Tim 3:12 Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. 2 Tim 3:13 Lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu wakidanganywa na kudanganyika. Kwa hiyo sisi tuliendelea kuomba; kisha Bwana akasema: Unabii: Mimi naenda kuipindua dunia hii ndani nje na nje ndani na kuipiga teke huku na huku kama mpira. Mimi nitaenda kuizika kanisa la binadamu; kama kaburi lile nililo kuonyeshea hapo kwanza, nanyi mtaenda kutamani kuweka maua juu yake. Wengi wa wale walioko kwenye Mwili wa Kristo wanadhania Mimi nafanya mzaha, lakini waigizaji tayari kila mtu anayo maandiko ya sehemu yake ya kuigiza. Mambo yako tayari kwa kuja kwa nyundo na mundu. Siku za theologia zimekwisha! Siku zile za damu kumwagika katika mitaa zimewadia! Jeshi la kule Mbinguni liko tayari na limekwisha kujitayarisha! Jeshi la duniani linaendelea kukamilisha matayarisho yake. Tulipofikia hapo tuliacha kuomba kwa sababu mara hali yote ya hewa ya mahali pale ikabadilika, nasi tukalazimika kuacha kuomba. Wakati sisi sote watatu tulipokuwa tukitafakari na kujadili hayo, Carl mara akapatwa na hisia ya kuwa tuendelee na maombi kwa ajili ya mahitaji yetu binafsi. Kisha Bwana akaniambia, "Je unahitaji kusikia zaidi! Jirani atamsaliti jirani yake. Mama atamsaliti mtoto. Wazazi watakula nyama ya wana wao kwa chakula. Wengine wenu mtatamani kufa, lakini Mimi sitawaruhusu mfe. Sanduku la Agano liko tayari! Nyundo na mundu ziko tayari! Kuanguka kwa Babiloni iko tayari! Lakini hayo yanatosha kwa leo!" Hili kwa kweli lilitutisha sisi, kwa sababu sisi tulikuwa tunaomba kwa ajili ya mahitaji yetu, na Bwana akaanza kuzungumzia kuhusu mambo ya siku za Mwisho. Hayo ya hapo juu yaliniumiza sana, kwa maana mimi nilikuwa nakumbuka kumwambia Bwana kuwa; kama mimi nitaendelea kutoa ujumbe kama huo wa hapo juu; watu wangeliniita mimi nabii wa nyakati za maangamizi. Bwana alinijibu kuwa; Yeye hajali kama watu watanipa jina gani. Ila mimi nifanye kile ambacho Yeye alichoniambia nikifanye. Tatizo langu halikuwa si tu nilikuwa naweza kuona mambo hayo, lakini nilikuwa pia naweza wakati fulani kusikia maumivu ya yale niliyokuwa ninayo yaona. Kwa hiyo kutokana na hayo mimi niliwaambia ndugu zangu walio katika Kristo kuwa; mimi sitaki kuendelea kumba tena. Lakini ndugu yangu Carl yeye hakutaka kuacha kuomba. Yeye bado alitaka kumwomba Bwana kuhusu mambo yake ya kibinafsi. Lakini mimi nilimwambia tena kuwa mimi sitaki kuendelea kuomba tena. Lakini yeye bado alitaka kuendelea kuomba. Kwa hiyo sisi tulianza tena kuomba kwa ajili ya mambo yale ya kibinafsi. Kwa hiyo Bwana akaniambia mimi, "Kwa vile wewe bado unahitaji kusikia zaidi!" Kisha Bwana alianza tena kunionyeshea maono. Maono: Maono ya kwanza yalikuwa ni ya watu waliokuwa wanachomwa moto wakiwa bado wako hai. Hili lilinishtua mimi zaidi hata kuliko mambo yale ambayo Bwana aliyo kwisha nionyeshea mimi. Mimi nilitamani kulia na kuondoka kule chumbani. Maono: Kisha maono yaliyofuata yalikuwa ni ya kekei inayotumiwa na mafundi kwa kutobolea mbao na vyuma; na inayo endeshwa na umeme, kekei hiyo ilikuwa inatumiwa kutobolea jicho la kushoto la mtu fulani. Hili lilikuwa halisi kiasi ambacho mimi niliomba ndugu waliokuwa wanaomba waache kuomba kwa sababu mimi nilishindwa kuvumilia zaidi; kuona yale niliyokuwa ninayaona. Kwa hiyo tukaacha kuomba, lakini baadaye sisi tuliomba kwa ajili ya uponyaji wa masikio ya Ron; naye Bwana hakutupa maono zaidi ya kuhusu siku zile za Mwisho. (Mwisho).
|
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )