1345. Occurrence given to Raymond Aguilera on 25 June 1999.

Letter to e-mail list:

Hello Brothers and Sisters,

I have been trying to prepare myself for the upcoming Israel mission trip the past week. I have been praying, reading the Bible, and spending quality time with the Lord everyday, and trying to keep my focus. It feels like I am inside a spiritual military foxhole with bombs and bullets flying over the foxhole. The spiritual warfare has been intense the past few weeks, but the past few days this inner strength has been coming upon me. Yesterday, even my throat, which has been giving me trouble, began to cough madly for about a half an hour and when I was finished coughing my throat seemed to be healed. The pain just left.

And this spiritual inner strength keeps getting stronger and stronger the more I read the Bible. I will be leaving on the July 10, so I have about two weeks left before I head off for Finland and then to Israel on the 19th. I keep seeing this strange vision, as if I can see myself in this spiritual fox hole - I take a long DEEP breath - and jump over the embankment and run as fast as I can with my swinging sword. I have no idea what is out there in the spirit, but the Lord said to go - so I am going. I wish I could better explain myself in what I see, but there are no words to explain it.

I have no doubts of not having enough money or where we are to stay. The only thing I can think about is where will I anoint the ground, but even that I know the Lord will show us. For He has already given us the first place (outside of Tel Aviv the first day). So I guess all that is left to do is to jump over the embankment, swing that sword and LET THE LORD DO THE FIGHTING!

Yours in Christ, ray

PS: We will still need a prayer cover during this Israel mission trip. God bless.

1345. Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 25 Juni 1999.

Barua kwa ajili ya kutumwa kwenye mtandao:

Wapendwa Kaka na Dada zangu katika Kristo,

Nimekuwa nikijaribu kujitayarishwa kwa ajili ya safari ijayo ya kwenda Israel kwa wiki yote iliyopita. Nimekuwa nikiomba na kusoma Biblia, na kukaa mbele za Mungu ilikupata muda mzuri wa kuwa naye kila siku, na kujaribu kuweka umakini wangu. Mimi ni kama niko kwenye handaki la Kijeshi katika ulimwengu wa kiroho, na mabomu na risasi zikiwa zinaruka juu ya kichwa changu kwenye handaki hilo. Mapambano ya kiroho yamekuwa ni makali sana katika wiki chache zilizopita, lakini wakati huo huo, nguvu ya ndani yangu inazidi kuongezeka. Jana hata lile koromeo langu lililokuwa linanipa shida likaanza kukohoa kwa nguvu mfululizo kwa kiasi cha nusu saa hivi, na nilipo maliza kukohoa nikaona kama koo langu lilikuwa limepona kabisa. Maumivu mara yakatoweka.

Na nguvu hii ya ndani ya kiroho inaendelea kukua na kuwa na ujasiri zaidi na zaidi kwa kadri ninavyo soma Biblia. Mimi natarajia kuondoka tarehe 10 Julai, kwa hiyo ninakiasi cha wiki mbili tu; ya kukamilisha matayarisho kabla ya kuondoka kwenda Finland na kisha kuelekea Israel kwenye tarehe 19 Julai. Mimi napatwa na maono haya ya ajabu ajabu ya kuwa ni kama ninajiona nikiwa ndani ya handaki la kiroho – nami mara NAVUTA pumzi kwa wingi - na kuruka kutoka humo ndani ya handaki na kukimbia kwa nguvu zangu zote na huku nikiwa na zungusha upanga wangu. Mimi kwa kweli sijui kuna nini pale katika ulimwengu wa kiroho, lakini Bwana aliniambia kuwa niende – kwa hiyo mimi naenda. Natamani ningelikuwa na namna nzuri zaidi inayoeleweka ya kujieleza mwenyewe, lakini hakuna maneno ya kuyaeleza hayo.

Mimi sina wasiwasi ya kuwa labda sitakuwa na fedha za kutosha safari hiyo au kuhusu ni wapi nitakapokaa. Kitu pekee ninacho waza; ni kuhusu ni maeneo gani nitakayo enda kuyaweka Wakfu, lakini hata hilo mimi najua kuwa Bwana atatuonyeshea sisi pale. Amekwisha tuambia sehemu ya kuanzia (nje ya ya Jiji la Tel Aviv katika siku ya kwanza). Kwa hiyo mimi nadhani kile kilicho baki ni kuruka kutoka ndani ya handaki hilo (la kiroho) na kuanza kuzungusha upanga na KUMWACHIA BWANA AFANYE MAPAMBANO!

Wako katika Kristo,

 ray

Ilani: Sisi bado tunahitaji maombi ya kutufunika kwenye safari hiyo ya kwenda nchini Israel. Mungu awabariki.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.