|
1358.
Vision given to Raymond Aguilera on 19 July 1999 at 7:10 PM. During prayer the Lord showed me a night scene of a large city somewhere in the world. The city was all lit up. The streets, towers and buildings, everything was lit up and it looked so beautiful. Vision: Then the next vision was of a man wearing some sort of covering over his loins (his private parts) with his chest bare. He was lying flat on the ground on his stomach. What was so unusual to me was he was looking down this deep wide and dark cliff or embankment. As I looked and stared at this man he was stretching as far as he could to see downward. I could not see his face, but I could see he had long dark hair, and I could only see the back of his head. This sounds strange, but in the spirit I sensed it was Adam from the Book of Genesis. But he was in the sky or in the heavens looking down through outer space towards earth. This place was not really a real cliff, but a place (maybe heaven) where one could look down at all the twinkling stars of outer space. Vision: Then the next image was of a male penis. Then the imaged stopped. Prophecy: Then the Lord said, "All good things come from the Lord!" (over) Note: The Lord was letting me see Adam looking down at today's time on the planet earth. As if God was letting Adam see all of the things his seeds had accomplished. I felt so privileged to see and experience this, that I thought about it for hours and hours and remembered how the Lord showed Moses the promised land from on top Mt. Nebo. Deu 32:48 On that same day the LORD told Moses, Deu 32:49 "Go up into the Abarim Range to Mount Nebo in Moab, across from Jericho, and view Canaan, the land I am giving the Israelites as their own possession. Some questions I have: Why was God letting Adam see this? Adam was there at the beginning of creation; is Adam going to see the end of the planet? This vision gave me goose bumps. (over) |
1358. Moano
aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 19 Julai 1999 saa 1:10 usiku. Wakati wa maombi Bwana alinionyeshea hali halisi ya Jiji fulani kubwa lililoko mahali fulani duniani wakati wa usiku. Jiji hilo lilikuwa limewashwa mataa. Mitaa yake yote pamoja na maghorofa yake maefu na nyumba zake pia. Kila kitu kilikwa kimewashwa na ilikuwa inaonekana kuwa ya kupendeza na kuvutia sana. Maono: Kilichofuata kuonekana kilikuwa ni maono ya mtu fulani aliyekuwa amevaa majani mbele (kufunika sehemu zake za siri) na huku kifua chake kikiwa kipo wazi. Yeye alikuwa amelala kwa tumbo ardhini. Kile kilicho kuwa ni cha ajabu kwangu kilikuwa ni kule yeye Adamu kuchungulia chini kwenye bonde hilo lenye kina kirefu na pana na lenye giza nene. Nilivyokuwa ninamwangalia na kumkazia macho mtu huyo; yeye alikuwa anasogeza kiwiliwili chake kwa umbali mkubwa uwezekanavyo mbele kwa tahadhari ili aweze kuna chini zaidi kwa urahisi (na bila ya kutumbukia humo). Mimi nilikuwa sioni uso wake, lakini mimi nilikuwa naweza kuona kuwa alikuwa na nywele ndefu na nyeusi, nami nilikuwa naweza kuona kisogo cha kichwa chake. Hili najua kuwa linasikika kuwa ni kitu cha ajabu, lakini katika ulimwengu wa Kiroho mimi nilikuwa na patwa na hisia kuwa huyu alikuwa ni Adamu wa kwenye kitabu cha Mwanzo. Lakini yeye alikuwa yuko angani au labda Mbinguni akiwa anaangalia chini kupitia anga za juu kuelekea duniani. Huo haukuwa mwamba wa kawaida au ni ufa wa kawaida, (labda ilikuwa ni Mbinguni) mahali ambapo mtu anaweza kuangalia chini kwenye vimulimuli vya nyota za anga za juu za dunia hii. Maono: Kisha maono yaliyofuta yalikuwa ni ya sehemu ya siri ya mwanaume. Kisha maono hayo yakakoma mara. Unabii: Bwana akasema, "Yote yaliyo mazuri yanatoka kwa Bwana!" (Mwisho). Ilani: Bwana alikuwa naniwezesha kumwona Adam akiwa anaangalia chini kwenye nyakati zetu hizi katika dunia yetu. Inaonekana kana kwamba anamfanya Adamu aone ile mbegu yake aliyoiacha duniani ili fanya mambo gani na ni mambo gani wameyakamilisha. Mimi niliona kama mtu aliyekuwa na bahati ya pekee ya kuona haya na kuyahisi, ikanifanya niyatafakari kwa muda mrefu wa masaa na masaa na huku nikiwa ninayakumbuka jinsi Bwana pia alivyo mwonyeshea Musa ile nchi ya ahadi kutoka kwenye kilele cha Mlima Nebo. Kumb 32:48 Bwana akasema na Musa siku iyo hiyo, akamwambia, Kumb 32:49 "Kwea katika mlima huu wa Abarimu, mpaka kilima cha Nebo, kilicho katika nchi ya Moabu, kueleke Yeriko; ukaangalie nchi ya Kanaani niwapayo wana wa Israeli kuimiliki. Maswali niliyo nayo: Ni kwanini Bwana anamwacha Adam kuona hayo? Adam alikuwapo pale kwenye mwanzo wa maumbile; je, Adam anaenda kuona Mwisho wa dunia hii pia? Maono hayo yalinipa msisimko kama mtu aliye mwagiwa maji baridi. (Mwisho).
|
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )