|
Taarifa
fupi kutoka kwenye repoti ya safari ile ya kuweka Wakfu eneo la kilometa
300, nchini Israel.
Bwana alinikataza nisitumie kinasa sauti cha kunasia kumbukumbu ya unabii na maono wakati wa maombi ya komunio, au wakati tulipokuwa safarini kwenye gari letu. Mimi nilijaribu kuweka kumbukumbu ya maono mara mmoja wakati wa maombi ya Komunio na mara Bwana aliniambia nizime kinasa sauti changu hicho mara mmoja. Hata hivyo Bwana aliniruhusu kunasa unabii mchache na maono wakati wa maombi ya usiku wa manane; kwenye chumba changu cha Hoteli. Naam, kwa vile Carl alikuwa akiweka kumbukumbu ya matukio ya maeneo yote tuliyokuwa tunayatembelea na kuyaweka Wakfu, yeye alituandikia ripoti ya kwanza kwa niaba yetu. Ripoti ya hapa chini ni kutoka ripoti ya Carl. Na sehemu iliyobaki ni sehemu ya ripoti yangu niliyokuwa nimeinasa kwenye kinasa sauti changu; pamoja na yale ninayo weza kuyakumbuka. Mungu awabariki ninyi nyote! Hafuatayo hapa chini ni majina ya maeneo tuliyo weka Wakfu. 1. Tel
Aviv/Yafo
(Bonyeza hapa kupata ramani ya kubwa ya maeneo hayo) Hapa chini ni ripoti ya Raymond Aguilera: 1359. Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 20 Julai 1999. Sisi mara tulipotua kwenye uwanja wa ndege wa Ben Gurion, tulikwenda kutafuta gari la kukodi kwa ajili ya safari yetu hiyo. Na tulipopata gari letu hilo la kukodi tuligundua kuwa lilikuwa ni ndogo sana kuliko gari tulilo kuwa tumeliagiza, na pia ufunguo wa kuwashia gari hilo ulikuwa haufanyi kazi vizuri. Kwa hiyo baada ya ucheleweshaji wa kiasi cha saa mmoja hivi, sisi tuliondoka pale kwenda kutafuta eneo la kwanza la kuwekwa Wakfu kwenye ule mzunguko. Ilikuwa inaonekana kama sisi tulikuwa tunaenda na kuzidi kwenda na kuanza kupotea. Unabii: Kisha Bwana alinipa Neno, "Tafuteni Mwanga au tafuteni nuru." Kwa hiyo sisi tulianza kuangalia kila aina ya taa mahali hapo, kuanzia taa za barabarani hadi mwanga wa jua. Kisha baada ya kuhangaika kwa kitambo cha kama saa mmoja hivi, tulipata eneo au uwanja wazi wa kupumzikia karibu na eneo la zizi la wanyama na kanisa. Sisi tukatambua kuwa eneo la kuwekwa Wakfu lilikuwa kwenye uwanja huo wa kanisa, lakini sisi hatukuwa na uhakika, na kanisa hilo lilikuwa limefungwa na tulikuwa tumeshindwa kupata njia yeyote ya kuingia ndani yake. Kwa hiyo sisi tukarudi kwenye gari letu na kuelekea kwenye uwanja huo uliokuwa nyuma ya kanisa hilo na kuliacha gari letu hilo hapo nasi kuelekea kwenye fensi iliyokuwa inaigawanya sehemu hizo mbili na kumwomba Bwana ili atupe uelekeo kwa maana tulikuwa tumepotea na kuchanganyikiwa bila ya kujua ni wapi eneo la kuwekwa Wakfu. Kisha wakati wa maombi Bwana akasema, "Alama X inaelekeza sehemu iliyo sahihi!" Nami nilivyo angalia chini kwenye miguu yetu niliona alama kubwa ya X katika ulimwengu wa kiroho katikati ya miguu yetu, nami nikamwambia Mark na Carl hii ndiyo sehemu yenyewe ya kuwekwa Wakfu. Maono: Kwa hiyo sisi tukaiweka eneo hilo Wakfu nakuona Taji la Mfalme katika ulimwengu wa kiroho. Unabii: Kisha Bwana akasema, "Sasa kwa haraka ondokeni kutoka eneo hilo!" Hili lilinishangaza kwa maana Carl alikwisha sema hapo mwanzoni kuwa yeye angelipenda kukaa kwenye uwanja huo wakupumzikia kwa muda kidogo ili aweze sinzia kidogo. Kwa maana alikuwa anapata taabu kukaa macho baada ya safari ile ndefu ya ndege. Yeye pekee ndiye aliyekuwa na kibali cha kuendesha gari, nasi ilikuwa inatubidi tuendeshe gari letu hilo hadi Yerusalemu kwenye hoteli yetu ambayo ilikuwa iko umbali wa kiasi cha zaidi ya saa 1 kutoka hapo. Lakini kwa mshangao wangu mara Carl akaanza kupiga picha ya eneo hilo baada ya kupaweka Wakfu, na yote yaliyokuwa ndani kichwa changu ilikuwa ni lile agizo la Bwana kuwa, "SASA NA KWA HARAKA ONDOKENI KUTOKA MAHALI HAPA!" Mimi niliuangalia uso wa Mark; nao ulikuwa unaonekana kama mtu anayetaka kuondoka pia. Naam, sisi tuliingia kwenye gari letu na kuondoka kutoka hapo kwa haraka iwezekanavyo na huku Carl akiwa bado anahitaji kupumzika kidogo kwa vile alikuwa anasinzia. Baada ya kitu kama saa mmoja hivi Carl alianza kuwa na tatizo la kuwa macho wakati sisi tukiwa tunaelekea Yerusalem. Mwishoni tulilazimika tusimame nje kidogo ya Jiji la Yerusalem ili Carl apate kupumzika kidogo kwa maana alikuwa anapata shida ya kuwa macho. Kwa maana kama Mark asingeli piga kelele tungali panda kwenye vizuizi vya pale barabarani kwenye njia ambavyo vimewekwa makusudi ili kuzuia magari yasipite kwenye njia iliyo zuiliwa. Ilikuwa ni jambo jema kuwa Mark aliweza kuona vuzuizi hivyo vilivyo kuwa na misumari kwa maana tungeliweza kuharibu tairi zetu mbili za miguu ya mbele mara mmoja. Wakati huo jua lilikuwa limetua na giza lilikuwa limekwisha kuingia. Kwa kweli mimi sikuwa na uhakika kama tungeliweza kupata hoteli usiku ule. Kwa maana Carl aliyekuwa anaendesha, alikuwa bado na lile tatizo la kusinzia mara kwa mara, na huku sisi tukiwa ni wageni na hatulijui Jiji lile vizuri. Mimi sielewi na kwa jinsi gani Carl na Mark walivyo fanikiwa kupata hoteli kwa maana hata majina ya mitaa tulikuwa tunashindwa kuyasoma kwa maana yalikuwa yameandkiwa katika lugha ya Ki-Ebrania ambayo tulikuwa hatujui kusoma herufi zake. Lakini tulifanikiwa kupata hoteli fulani ndogo ya vyumba 18 kwenye eneo fulani ya barabara ndogo inayo pitisha magari kwenda upande mmoja tu kama barabara binafsi ya mtu kuendea nyumbani kwake. Ninaloweza kusema ni kuwa - “Bwana alituongoza vizuri sana katika siku ile ya kwanza. Bwana asifiwe!!!" Wasafiri wa tatu walioenda kwenye safari ya Israel. Carl akiwa kwenye ufukwe wa ziwa Galilaya
Mimi sikutaka Carl achukue picha yangu wakati nikiwa nakula aisikrimu, lakini nilishindwa kumzuia. Carl akasema, picha hiyo nikwa ajili ya mtandao: kwa hiyo hiyo hapo nimeiweka! (Tabasamu) Mimi nilikuwa na tatizo la kula aisikrimu wakati wa ziara yangu hiyo. Nchi ya Israeli ilikuwa na joto kali sana wakati huo. Kutoka kwenye kumbukumbu ya ripoti ya Israel aliyo andika Carl.
Sisi tulifika pale Tel Aviv, Israel. Tulienda kwenye uwanja wa kupumzikia karibu na kanisa fulani la Kikristo la Kiothodoksi na kuomba hapo; ili kupata maelekezo ya ni wapi pa kuweka Wakfu. Ndipo Ray akapata neno. Neno la Ray: Alama "X" ni kielelezo cha eneo husika. Maono: Sura ya Taji la Mfalme. Neno: "Sasa, kwa haraka ondokeni hapa! 21/7/99 Neno: Msumari wa kiroho utaenda kupigiliwa katika kila sehemu iliyo wekwa Wakfu. Maono: ya kamba ya ngozi ikiwa inaunganisha sehemu hizo. Neno: Mfuniko kama wa bakuli utafunika eneo hilo lote. Anga litakuwa jeusi. 21/7/99 Sisi tuliomba asubuhi ili kujua ni wapi Bwana alipotaka twende kwa siku ile. Neno: "Tafuteni nanyi mtapata" "Sojourners" (Sisi tulielewa kuwa sisi ndugu watatu katika Kristo ni wasafiri “sojourners” katika safari hii). Maono: Mawimbi nyuma ya ukuta mrefu wa kuzuia bahari uliokuwa na ufukwe mwembamba. Ukuta huo mkuu uliendelea hadi ndani ya nchi kama ule ukuta mkuu (wa Kichina). Neno: Amani (itakuwa pamoja nanyi; inaenda juu na kwenda chini). Maono ya Usiku wa manane ya siku iliyopita: Ray aliona maono ya binti fulani mdogo aliyekuwa amemwona pale kwenye Ukuta wa Magharibi, ambaye karibu angelimpiga picha. Maono: Kisha akaona maono ya msichana huyo akiwa amekwisha kuwa mtu mzima labda akiwa na umri wa miaka (18-24). Neno: Hayatatokea mpaka hapo huyo binti atakapokuwa amekua. Neno: <Mungu> "Ataenda kumwua mtu fulani" Tarehe 22/7 Saa 3:40 asubuhi Neno: "Kusifu na kuabudi ni nzuri - lakini utii ni aheri zaidi." Maono: “Kisu” kikubwa kilicho na sura kama ile ya mchezo wa sinema wa “Crocodile Dundee” ukiwa unakata kitu fulani. Maono: "Mimi nitaenda kuchana ngozi ya kuhifadhia mvinyo na kuwa wazi." Maono: Kitu chenye sura ya mfuko wa ngozi kama ule wa kuhifadhia mvinyo, ambayo ina sura ya harage au mfuko wa tumbo la mtu. Tarehe 22/7/99 Neno: "Nenda" Maono: Kamba iliyokuwa imefumwa kwa kamba - 3. Tafsiri yake: Siyo rahisi kuikata. Saa 6 mchana Maono: Kitu kama daraja na watu wakiwa wanarukia juu yake. Tafsi yake: Watu itawalazimu kuruka ili wafike upande wa pili. Neno: "Mlima Nebo tu" yale mengine yaliyo baki ni jangwa tupu la wapagani ambalo halina thamani yeyote." 22/7/99 Tulifanya maombi ya kujua ni lini tuondoke kuanza safari ya kwenda nchini Yordani. Neno: "Je, unapomng’oa unyoya bata mzinga yeye anaruka? (Ambayo sisi tuliitafsiri kuwa tuchukue usafi wa gari binafsi ya kukodisha itakayo patikana kwenda nayo Yordhani). Sisi tuliondoka kutoka Yerusalemu kuelekea Tel Aviv na kuelekea kusini kwenye karibu na ile nusu kipenyo chetu cha maili 30 kutoka Yerusalemu. Tulisimama pale Yavne. Neno kwa ajili ya kuweka Wakfu: "Hapa"
Sisi tulisimama karibu na uwanja wa kupumzikia karibu na Sinagogi. Neno: "Hapa" (Sisi tulielewa hiyo kuamaanisha kuwa inatulazimu kuweka Wakfu sehemu iliyo inuka ya uwanja huo wa kupumzikia) Kisha sisi tuliendelea kuendesha gari letu kupitia Qavat Malakhi. Sisi tuliomba kuhusu ni wapi pa kusimama tena. Neno: "Sogeni mbele!" Tulipofika Qiryat Gat tuliomba na kusikia. Neno: "Sawa" Neno: "Songeni mbele!" Saa 10:30 mchana. Kisha sisi tuliendelea kuendesha gari hadi kwenye mji wa Uza na kusikia Neno: "Tafuteni nanyi mtapata!" Sisi tuliamua kusimama kwenye Uwanja wa kupumzikia wa City Park, ambao ulikuwa na tanki kubwa sana la zege kwa ajili ya kuhifadhia maji; lililo kuwa tupu. Pamoja na Sinagogi. Sisi tuliona ni vyema kuweka wakfu ardhi ya eneo hilo la hapo. Saa 12 jioni. Baada ya hapo sisi tulisonga mbele hadi Edh Dhahiriya – kiasi cha kilometa 8 ndani kutoka eneo la kukagua magari kwenye mpaka wa Ukingo wa Magharibi. Neno: "Msiendelee mbele zaidi tena!" Sisi tulisimama na kuegesha gari letu pembeni mwa mwa barabara na kuweka Wakfu ardhi iliyokuwa hapo kutoka mlango wa nyuma wa gari letu. Kisha sisi tuliondoka kutoka eneo hilo la Ukingo wa Magharibi na kuendelea kupitia Barabara Kuu Na. 31 na kupokea Neno. Neno: Simameni na kuegesha gari kwenye eneo la usalama hapo. Saa 12:30 jioni. Maneno: "Kile kilicho enda juu kitarudi chini!" "Kung’uteni mavumbi ya kwenye viatu vyenu!" Ray akasema, "Ebu tusimame na kununua tikiti maji hapo." Tarehe 22/7/99 saa 3 au saa 4 usiku. Sisi tulifika kwenye hoteli ya ufukwenu mwana Ziwa la Chumvi kiasi cha maili 5 kusini mwa Massada, kwenye eneo la kuegesha magari. Neno: ''Songeni mbele''. Sauti ya adui: ''Ninyi hakuna haja ya kusimama hapa'' - ''Ninyi matapeli''. Tulipofika eneo hilo Ray aliiweka Wakfu eneo hilo. ''Ninyi natumaini hamhitaji kufanya hivi!" Neno: ''Ondokeni hapa kwa haraka'' ''Asanteni watumishi waaminifu'' Sauti ya adui: ''Punguzeni mwendo na msimame. Pumzikeni kidogo.'' 23/7/99 saa 4 asubuhi Neno: ''Maisha ni kama mti wa mzeituni, una shimo'' Maono: Mizania ya kupimia inayo bembea. Neno: ''Kaeni hali ya kuwa wima na waangalifu na kuweka umakini.'' Neno: ''Mjiweke Wakfu kwa kujipaka Mafuta kila mmoja wenu.'' ''Kumbukeni kile nilicho kisema ya kuwa kile kiendacho juu kitarudi chini – itakuwa toka milele hadi milele, na milele. Mawe au matofali ya ujenzi wa Hekalu Jipya – kwa hiyo muwe wachapa kazi hodari, wenye busara waangalifu, imara, wenye nguvu na shujaa, na walio wajanja kama nyoka. ''Ni la umuhimu mkubwa sana kuwa mnaweka umakini wenu wote'' Saa 5:40 asubuhi. Neno: "Kuna vita ambavyo vinavyo vinaendelea kule Mbinguni kwa ajili ya yale tunayo yafanya" Maono: "M" (Maono ya Herufi) Neno: Herufi inasimama kwa neno “Marriage of the Lamb” yaani ndoa ya Mwana Kondoo – Inaandaliwa hivi sasa. Maono: Vita huko Mbinguni na majeshi ya pande mbili zinatwangana. Neno: "Nendeni Kaskazini". Maono: 1. Mguu mmoja mkubwa wa Ndege. 2. Chombo cha muziki – uliokuwa unafanana na zeze (harp) 3. Mdudu akiwa anamkodolea macho Ray. Saa 7:30 usiku. Maono: Namba "9". Saa 7:50 usiku. Neno: "Vita ya kule Mbinguni vinazidi kuwa vikali sana". "Songeni Mbele". "Tunapotea kutokana na ukali wa vita vya kule mbinguni." Saa 8.00 usiku. Neno: "Safari ijayo mtakaposimama wekenu Wakfu gari lenu hilo." Saa 8.02 usiku Neno: Wekeni Wakfu kwenye pembe zake 4." Saa 8.10 Usiku. Wekeni Wakfu mji wa Petah Tiqwa kwenye uwanja wake wa kupumzikia ulioko kwenye eneo la Kusini Mashariki mwa mji, kwenye umbali wa kilometa 9 kutoka kwenye kona ya kuingilia kwenye Barabara Kuu Na. 40. Neno: "Ninyi mmeenda umbali wa kutosha, mnaweza kutafuta chochote cha kula." Sisi tulienda kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi kutafuta mgahawa katika mji wa waarabu. Neno: "Mnataka kula pamoja na mbuzi?" Kisha sisi tuliondoka huko kwenye mji wa Kiarabu na kwenda kutafuta mgahawa kwenye eneo la mji wa Waisraeli; nje ya Ukingo wa Mngharibi ili kupata chakula. Tarehe 24/7/99 saa 1.05 asubuhi Neno: "Sehemu inayofuata itakuwa ni kwenye Mlima Nebo". Sisi tuliomba kuhusu kwenda Shekhem. Neno: "Ninyi hakuna ulazima wa kufanya hivyo". "Hakuna eneo lingine la kuwekwa Wakfu tena". Neno: "Kama mwezi hautakuwa mpevu wakati mtakapo kuwa mnarudi kutoka kwenye safari ya kuweka Wakfu Mlima Nebo ndipo hapo ambako mnaweza kurudi na kuweka Wakfu eneo kuanzia Shekhem hadi Yordani". Saa 5.50 asubuhi. Maono: "Mnara wa Eiffel wa Paris na wembe ukiwa unakata sehemu yake ya chini kuanzia upande wa kushoto kuelekea kulia". Tarehe 25/7/99 Neno: "Nendeni kwa haraka". "Watumishi wazuri na waaminifu". Sauti nyingine ikisema "Msiende, Msiende". Neno: "Mtaenda kupitia kwenye njia iliyo na miiba." Maono: Farasi 6 au 7 wakiwa wanakunywa maji kwenye chombo kilichokuwa cha mviringo – kama handaki ikiwa na maji maji ya rangi nyeupe.
Neno: “Sanduku la Agano” – Alisema hivyo kama mara 6 hivi. Neno: "Je, unanipenda Mimi" – Hili lilitamkwa kama mara 6 hivi au zaidi. 25/7 Jumapili saa 10:25 jioni (Wakati tukiwa kwenye hoteli juu ya Mlima Mizeituni, ambao ulikuwa unauelekea Mji Mkongwe wa Yerusalemu pamoja na Mlima wa Hekalu au a “the Temple Mount”) Maono: Mnara wa moto - ukiwa na mwanga mwembamba, ambao ulikuwa ukizunguka na kugusa paa la Msikiti ule wa “Dome of the Rock”. – Kilele cha mwanga huo ulikuwa unatokea mashariki - Ray anasindwa kuona kilele chake. Unageuka na kuwa mwekundu na mwanga wake unapanuka. Ulikuwa mpana sana - (Kilometa kadhaa) Upinde wa mvua ukiwa unakuja kwa nyuzi - 80 ulikuwa unaonekana kwa uwazi kwenye eneo la kaskazini mashariki ya anga hilo. Ilikuwa na rangi nyekundu katika kila ukingo wake wa nje, na rangi ya kijani kibichi na bluu katikati yake. 26/7/99 Neno: "Inakulazimu uachie moyo wako". (Neno kwa Ray) Maono: Ncha ya mshale uliokuwa umefungiwa kitamba cheupe nyuma tu ya ncha yake kali ya mshale huo. Wakati tulikpokuwa tunatembea juu ya Mlima Nebo kwenye saa 9.50 jioni. Neno: "Kamera, Kamera, Kamera, Kamera". Saa 10.10 jioni. Wekeni Wakfu eneo la hapo juu ya Mlima Nebo karibu na ukuta.
Saa 10.15 jioni. Neno:"Imekamilika". Kutoka Hoteli ya Grand View kwenye Mlima Petra baada ya kula chakula tuliona mwezi ukiwa kama ni mpevu kabisa. 27/7 saa 5:20 asubuhi wakati tukiwa tunapita kwa kupandisha kwenye kinjia cha “El Siq” kutoka Petra, tulipofika kiasi cha 1/3 ya safari ya kufika kwenye bonde hilo Ray aliweka Wakfu sehemu zote mbili ya ukuta wa bonde hilo.
Jioni: Sisi tuliona mwezi ukiwa ni mpevu wakati tukiwa tunarudi Yerusalemu kwa gari letu. 28/7 Neno: "Baraka inaenda kukoma". Maono: "S". "US". Maono: Kuzuio cha kuoteshea mti kilicho cha mviringo; ambako ndani yake kulikuwa na mti usio kuwa na majani ambao ulikuwa unaota na kisha ukaendelea kukua kwa urefu na kutoa majani. (Ulikua kuanzia futi 2 hadi futi 6 hivi). Kuomba kwa ajili ya Ray aliyekuwa anaumwa saa 2.30 usiku. Neno: "Alikuwa ni aduia aliyemfanya Ray kuugua kwa sababu mlikuwa wajasiri kiasi cha kudhubutu kuweka wakfu kuta za El Siq. Kwa ajili ya ujasiri wenu miungu yote katika ulimwengu wa kiroho ilikasirika. (Huu ulikuwa ni mlango pekee wa kuingilia kwenye mji)”. Neno: "Kamba ya nyuzi – 3 ni ngumu kukatika". Wakati tulipokuwa tunaomba kwa ajli ya ulinzi kwa ajili yetu sisi 3. Neno: "Msile uyoga". 1) Mark aliweka Wakfu ukuta wa je wa Mji Mkongwe, nje tu kidogo ya Msikiti wa “Dome of the Rock” 2) Carl aliweka Wakfu eneo lililokuwa karibu na mlango ule uitwao “Golden Gate” karibu “Dome of the Rock” na kuomba ndani ya “Dome karibu na mwamba huo. 3) Kisha Mark na Carl waliomba kwenye kinjia karibu na mlango ule uitwao “Golden Gate”. Saa 29/7 saa 3 usiku Maono: Washeni mshumaa katikati ya mviringo huo unaowaka – kisha wakati tukiwa tunauelekea, ulisogea kuelekea upande wa kulia, lakini eneo hilo lililokuwa linawaka liliendelea kukaa likiwa linawaka. 30/7 saa 6.15 usiku. Neno: "Mnaweza kwenda kwenye eneo hilo kuangalia, lakini ni kwanini kuangalia jadi ya ustaarabu kufa. Yeye achukuaye jembe huwa haangalii nyuma tena. Tafuteni mambo ya agano mpya na wala siyo yale ya agano la kale." Baada ya chakula cha jioni tulitembea kupitia Mji Mkongwe na kuishia kwenye Ukuta wa Magharibu. Neno: "Kwanini, Kwanini, Kwanini". (Ray alisikia hiyo ikisemwa kwa sauti ya chuki). Ray alijibu: Sisi tunashindwa kuondoka hapa – kwa maana Carl ndiye aliye na ufunguo wa gari na yuko huko ndani (kwenye eneo la ndani la kuomba kwenye Ukuta ule wa Magharibi). Neno: "Kaeni chini na mkamgonjee Carl huku mkiwa mmeugeuzia migongo yenu Ukuta huo wa Magharibu na wala msiangalie nyuma tena." Neno: "Na kamwe wala msirudi hapa tena." Ilani: Ray alianza kuhisi kuwa kulikuwa bado na mambo ambayo Bwana na Wayahudi hawaja ya maliza kuyapatia suluhu. (Ray yeye hajui mambo hayo ni yapi.) Tarehe 31/7 Maono: Taa liyokuwa inawaka ikiwa inaning’inia kutoka kwenye jengo. Neno: "Angalia taa hiyo, angalia taa hiyo." Maono: Kijiko kikubwa sana, kikubwa kuliko chumba chetu. Kisha kitu fulani cha kishetani au cha kipepo kikapanda juu yake; kwenye ukingo wa kijiko hicho na kujaribu kula au kunywa hicho kitu kilicho kuwa kwenye kijiko hicho. Kisha kijiko hicho kikasukumizwa kwenye mdomo wa fuvu la kichwa kilicho kuwa juu ya Mlima wa Fuvu la Kichwa. Neno: "Njoo". Maono: Picha (picha iliyo chorwa kwenye karatasi) zilionyeshwa zikiwa zina zunguka kwenye eneo hilo tulilolizunguka, ilikuwa inaonekana kama inazunguka kwenye eneo ambalo lilikuwa na jukwa ambayo ilijitokeza juu ya eneo hilo. Michoro hiyo iliyokuwa kwenye karatasi zilikuwa zinagusana. Na mwanaume na mwanamke walikuwa wanacheza ndani yake kama ilivyo kwenye ukumbi wa kucheza dansi, (Kama ilivyo kwenye picha ya Fred Astaire na Ginger Rogers lakini wakiwa kwenye mavazi ya kisasa) juu ya jukwaa – ambayo naamini ni Kristo na Bibi arusi wake. Maono: 1. Pale ambako Kristo na Bibi Arusi wake walipokuwa wanacheza dansi kulikuwa na jukwa lenye watu wengi juu yake. 2. Kijiko kikubwa kikaja chini na kujikunja kwa nyuzi 90 na kuingia mmoja kwa mmoja ndani ya nuru mkubwa. (Ilikuwa inaonekana kama ni Baba). Maono: Mchipuo wa mto karibu na bahari na katikati ya tawi hilo au mchipuo huo, kulikuwa na kuzuizi – kilicho kuwa kinaonekana kama kizuizi cha kurudisha nyuma maji ambacho kilijitokeza katikati ya tawi la mto huo ambaoo ilizuia mwendo wa maji hayo. Kichwa cha farasi – farasi mwenye rangi ya udongo ulio chakaa na mwenye sehemu ya panda la uso wake ukiwa ni mweupe ambayo ulienda hadi kwenye macho na masikio ya farasi huyo na chini hadi kwenye pua yake (Farasi ambaye alikuwa anaonekana alikuwa ni kama yule farasi wa kwenye kitabu cha Ufunuo). Tai akiwa anaruka kumwelekea Ray – Kichwa chake na mdomo wake ulikuwa unaonekana na ndani ya mdomo wake kulikuwa na gogo kubwa zito jeusi. Alikuwa anaruka juu ya bonde mmoja kubwa la ufa ambalo lilikuwa linaonekana kama halikuwa na kina na akakiangusha gogo hilo kwenye bonde hilo la ufa. Kuomba kuhusiana na tetemeko. Maono: Mlingoti wa kawaida ulio kuwa na rangi ya udogo uliochakaa ukiwa umeelemea kwenye nyuzi 80- na kukiwa na mligoti mwingine uliokuwa umeishikilia ili usianguke. Maono: Namba "4" ikiwa inabadilishwa na kuwa alama ya nanga kutoka kwenye Kaburi la kwenye Bustani (ambayo yule kiongozi wa msafara alitujulisha kuwa ni alama ya iliyoletwa makaburini na wafuasi wa Kristo). Neno: "Amechafua" Neno:"Sukuma, sukuma". Tarehe 1/8/99 saa 4:20 asubuhi. Neno: "Y".
Maono: Mnara wa moto uliokuwa mviringo na wenye upana wa futi 11/2 ft. na urefu wa futi 6 au 7 hivi ambao ulikuwa ukizunguka. Neno: "Njooni" "Njooni, leteni chupa ya mvinyo na kuiweka Wakfu tako la kuzunguka Mnara huo". Maono: Herufi Omega ya Kigiriki iliyokuwa kichwa chini. Maono: Mlingoti uliogeuka na kuwa msalaba. Neno: "Acha chupa hapo". Word: "Mimi nitaenda kumchukua mmoja wenu".
Neno: "Wakati mtakapo kuwa mna nawa kwa maji Mimi nitakuwa nikiwatakasa". "Tawi, tawi". "Mimi Ndimi. Mimi Ndimi". "Je, mtanipa Mimi mioyo yenu?" "Panya yule yuko tayari". "Isikilizeni Bahari". 4/8/99 saa 9 Mchana. Wakati tukiwa tunatembelea Nazareth kwenye kanisa la Kupashwa Habari. Neno: "Mimi nilikuita lakini wewe wala hujaja. Nilikuita nawe wala hujaja." Saa 10 jioni. Sisi tulisali kwenye eneo la juu la milima ya Nazareti. Maono: Shimo lililo kuwa la mviringo kwenye uzio wa waya. Neno: "Nendeni". (ondokeni) Tarehe 5/8/99 saa 1 jioni. Kwenye kijiji cha ujamaa cha Kibutz kilicho kuwa kwenye Ziwa Galilaya. Maono: Mifupa ya mtu (mtu mzima) na mikono yake, akiwa ameweka kama afanyavyo mtoto mchanga aliye tumboni mwa mama yake, akiwa chini ya barabara karibu na daraja. Saa 4.30 asubuhi. Maono: Megiddo. (Angalia picha ya hapo chini). Neno: "Uiweke Wakfu (Megido) ili kuitayarisha ardhi hiyo ya hapo" - "Ule Mwisho uko mbele yenu". Saa 5:10 asubuhi. Maono: Mkuki wa Dhahabu utachomekezwa kwenye ardhi ya maeneo hayo tuliyo yaweka Wakfu (Njiwa akiwa yuko juu ya mpini wa mkuki huo). Maono: Mtoto aliyekuwa kwenye tumbo la mama yake – ni kama anavyo angaliwa kwa darubini ya aina “sonogram” (ya kupimia ujauzito) na kichanga hicho kikiwa kinatembea ndani ya tumbo.
Sisi tuliweka Wakfu sehemu ya karibu na ukuta ambako ilikuwa karibu na miti ya mitende 3 kwenye katikati ambayo ilikuwa unatazamana Kusini mashariki. Ilikuwa inafanana na maono yale ambayo Ray alikuwa ameyaona hapo awali. Neno:
Ndiyo, hiyo ni sehemu ile inayotakiwa. Imefanyika na kukamilika. Agusti 6, 1999 Maombi pale kwenye Kibutz (kijiji cha ujamaa cha Kiisraeli) tulichokuwa tunakaa kabla ya kuondoka. Maono: Mavazi ya kijadi yaitwayo “ballerina”. Wakati wa saa za alasiri wakati tulipokuwa tunaondoka kutoka ufukwe wa Herzlyya (kaskazini mwa mji wa Tel Aviv). Neno: Asante Ray. Kwa nini, kwani nimefanya nini? Ray aliuliza. Neno: Ebu wewe pokea tu asante. Agusti 7, 1999 saa 7.25 mchana. Maono: Meza yenye sura ya pembetatu mraba na yenye miguu 3. Maono: Nyota ya Daudi – ikiwa na pembe 6 ikigeuka na kuwa nyota ya pembe 5. Maono: Kisu cha kuwindia cha wakazi wa Amerika ya kusini kiitwacho “Boomerangk” Maono: Samaki mwenye jicho.
Agusti 8, 1999 saa 11 jioni. Maono: Mlango mweupe ukiwa na kitasa cha chuma chenye marembo ya “curlicue lattice” kuizunguka (katika staili ya kifahari au “garland style”) ukiwa hauna kishikizo. Maono: Mimba changa. Sisi tuliomba kuhusu kama tuende kanisani kule Yerusalem (Kwenye kanisa liitwalo “King of Kings Assembly”) Neno: "Kutakuwa na kitoweo hapo." Neno: Angalia kanisa hilo lote na watu walio simama hapo. Kanisa hilo na makanisa mengine yote watakuchukia wewe na kutaka kulipiza kisasi. Lakini wewe usijali, mimi nitaenda kuwa pamoja nawe. Agusti 9, 1999 saa 3:40 asubuhi. Neno: "33" Maono: Vyuma vya aina ya springi ikiwa na nguzo 2 za chuma kwenye kila mwisho. Ilikuwa imefungwa pamoja. Mtu alikuwa yuko ndani ya vyuma hivyo vilivyo kuwa vimefungwa kama mfano wa jela. Maono: Mnara uitwao “Eiffel Tower” wa Paris ukiwa na kitu ambacho kilikuwa kinauzunguka kwenye “katikati yake” – kama sehemu ya mashine au taji la miiba. Tafsiri: Mtu yule aliyekuwa ndani ya vyuma vilivyo mzunguka ilikuwa inaashiria mafungo aliyenayo binadamu. Maono: "Maono ya chombo cha kusikilizia" (Kama ishara ya kuwa Mungu anasema, "Sikilizeni").
|
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )