|
1456. Vision given to Raymond Aguilera on 16 February 2000 at 9:50 PM. I had a vision of a Lion sitting at the edge of a cliff and looking down at the jungle below. I could see a deep green valley that had overgrowth all over the place. As I watched the Lion, he just laid still, looking down into the valley. Then I asked the Lord, "What does this mean? What is the Loin doing?" So the Lord showed me the valley, and there were all kinds of trees and tall grass, and undergrowth, and overgrowth. As I looked closer, I saw the head of a wolf hiding behind a bush. All I could see, was the wolf's head, with red eyes staring at the Lion. Then the Lord showed me the Lion again, sitting on the edge of the cliff. (over) Vision: Then I was shown an image of a bell, and the bell was ringing. As the bell rang, I was given another vision. Vision: The vision was of a dark black pot, full of boiling water, and inside this pot there was this snake. I could see the snake's head with its fangs and mouth open. This snake was being boiled, and I could see it sinking into the water, and trying to keep its head out of the boiling water. Then finally the snake sank into the water, and it did not come back up. (over) Vision: Then I was given a vision of an eagle on a cliff, feeding its babies. Then the image stopped. (over) |
1456. Maono aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 16 Februari 2000, saa 3:50 usiku. Mimi niliona maono ya Simba kwenye ukingo wa korongo na huku akiwa anaangalia chini kwenye msitu uliokuwa kwenye bonde au korongo hilo kwa makini. Mimi nilikwa naweza kuona bonde au korongo hilo likiwa na maoteo au msitu mnene uliokuwa umeshikamna sehemu yote. Nilivyokuwa nikimwangalia Simba huyo; yeye alilala chini na huku akiwa anaangalia chini kwenye bonde (au korongo lile). Kisha mimi nikamwuliza Bwana, "Je, hii ina maana gani? Je, huyo simba anafanya nini?" Ndipo Bwana akanionyeshea bonde hilo kwa ukaribu, na humo kulikuwa na miti ya kila aina; pamoja na majani, na maoteo ya chini ya msitu huo. Nilivyozidi kuangalia kwa ukaribu, mimi niliona kichwa cha mbwa mwitu huyo akiwa amejificha nyuma ya kichaka fulani. Yote niliyokuwa naweza kuona ni kichwa cha mbwa mwitu huyo; pamoja na macho yake myekundu, akiwa amemkondolea simba huyo. Kisha Bwana akanionyeshea simba huyo tena, akiwa amekaa kwenye ukingo wa korongo hilo. (Mwisho). Maono: Kisha mimi nikaonyeshewa Maono ya kengele na kengele hicho kilikuwa kinalia. Wakati kengele hicho kilipo kuwa kinalia, mimi nikapewa maono mengine. Maono: Maono hayo yalikuwa ni ya chungu zee nyeusi, ikiwa imejaa maji yaliyo kuwa yakichemka na ndani yake kukiwa na joka fulani. Naweza kuona kichwa cha joka huyo na mdomo wake ukiwa uko wazi pamoja na meno yake ya sumu. Joka hilo lilikuwa linapikwa, nami nilikuwa naona alipokuwa anazama na huku akiwa anajaribu kuweka kichwa chake juu ya maji hayo yaliyokuwa yanachemka. Kisha mwishoni joka hilo likazama kwenye maji hayo, na hakuibuka tena. (Mwisho). Maono: Kisha mimi nikapewa maono ya tai kwenye ukingo wa korongo; akiwa anawalisha vikinda vyake. Baada ya hapo maono hayo yote yakakoma. (Mwisho).
|
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )