1459. Vision given to Raymond Aguilera on 17 February 2000 at 1:27 AM.

During prayer I had a vision of a long curtain rod. You could see it going miles and miles, as far as the eye could see. Then there was this lion that was walking on the curtain rod or pole. Then with it's claws the lion pulled up the red curtain, and the whole curtain went up.

Vision:

Then the next image was of a lion walking on top of the curtain rod. Then the image changed, and the lion was sound asleep, lying on its side, on the curtain rod.

Vision:

Then there was a vision of a triangle that was on fire. In the center of the triangle I could see the Statue of Liberty. Then the Statue of Liberty disappeared and in the center appeared several horsemen, and they were riding fast. I could see they were coming over an embankment.

Vision:

Then I saw an image of a rhinoceros in the spirit. As it was walking away, it turned around, and looked at me.

1459. Maono aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 17 Februari 2000 saa 7:27 usiku.

Wakati wa maombi mimi niliona Maono ya mti au mwamba mrefu wa kutundikia pazia. Mwamba huo ulikuwa unaenda kwa urefu wa mamaili na mamaili; hadi upeo wa macho kuweza kuona. Juu yake kulikuwa na simba aliyekuwa akitembea juu ya mwamba au ufito huo wa kutundikia pazia. Kisha kwa kutumia kucha zake, huyo simba, alivuta pazia hiyo iliyokuwa na rangi nyekundu, na mara pazia hiyo yote ikapanda juu.

Maono:

Kisha maono yaliyo fuata yalikuwa ni ya simba huyo huyo; akiwa anatembea juu ya mwamba huo wa kufungia pazia. Baada ya hapo maono hayo yalibadilika na kuwa ya simba aliye kuwa amelala fofofo, akiwa amelala kiubavu ubavu juu ya mwamba huo wa kutundikia pazia.

Maono:

Kisha kulikuwa na maono ya pembe tatu mraba iliyokuwa ikiungua. Katikati ya pembe tatu mraba huo; nilikuwa naweza kuona Sanamu ile ya Uhuru (Liberty) wa Amerika. Mara sanamu hiyo ya uhuru ikapotea na mahala pake kukatokea wapanda farasi kadhaa na walikuwa wakipiga mbio kali. Mimi nilikuwa naweza kuwaona wakiwa wanaujia ukingo au mtelemko fulani mkali.

Maono:

Kisha mimi nikaona maono ya kifaru fulani katika ulimwengu wa kiroho. Wakati akiwa anaondoka kwenda zake, aligeuka nyuma na kuniangalia mimi.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.