|
1489. Occurrence given to Raymond Aguilera on 8 April 2000 at 2:00 PM. This past week and a half, I have been going to sleep about 1:30 AM, and I have been spending many, many hours proof reading Prophecy Book (2 and 3). These past several days it has been more like 3 AM, and my body is beginning to feel it, for I am always tired. Well, Eva has been telling to slow down. She was noticing how tired I have been lately. Well, she mentioned it again last night, but this something kept telling me not to stop, and to keep working. So I went back on the computer this morning about 1:30 AM, after a short break. I did not finish proofing Prophecy Book 3, but I almost did. Well, this gives you an idea of what I have been doing this past week, but this is not why I am writing this Occurrence. This morning, I turned on my computer and began again the long process proofing the Prophecy Book 3. I finished the proofing of Prophecy Book 3, but I needed to proof the Book cover. All I needed was to print the covers to Book 2 and Book 3, read them and make the necessary changes, but I had forgotten that my printer was running out of black ink, since I last used it. During the first cover printing, my computer printer began to flash a warning that it was out of black ink. This put a lot of pressure on me, because the Publisher had given me only two weeks to proof these two Prophecy Books, and for some reason the Lord was telling me to stay up all nights and early mornings to finish these proofs. Well, the problem was, I am over drawn in my bank account by $200, and I have no money to buy a $25 dollar black ink cartridge. The publisher did not bother me - it was the Lord. I knew there was some reason for Him keeping me up and working me so hard, but I was dead in my tracks. So I went downstairs, and asked my brother Ted, if he had any money to lend me, so I could buy the ink cartridge. He said this and that, but he did not look like he was going to give me the money. So I went back upstairs and decided to print and see what I could, with the colors that came out of the printer, or print until the printer stopped. Well, I started the printing process and removed the out of ink warning from my monitor and began to print what I could. I do not know how many people are going to believe this, but as my printer began to print - the printer ink gage said my black ink cartridge was FULL of black ink. I was in total shock. How was this possible I kept telling myself. I have e-mailed my data to the publisher. Now, I am finished, and waiting for the next two Prophecy Books (Book 1 & 4) to proof read from the publisher. Well now, a few hours later, I seem to be in the spirit, and I cannot come down. My body does not seem to know what to do. I have been praying for an hour or so, and I cannot come down from this spiritual level. During this prayer time, I felt like I was out of control, and prayed to the Lord for help. Then the Lord Jehovah gave me a vision of His Hands throwing and unrolling this large scroll into the Heavens. I could see this one end of the scroll unroll into the sky of Heaven. I am still a little uncertain about "What is next". I am totally broke without any money and my body seems to be trashed (tired) again. Well, I will never understand the Lord's timing and ways. I praise you Lord, and I am still trying to hang on! But what about the South America Mission Trip?
|
1489. Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 8 Aprili 2000 saa 8:00 mchana. Wiki mmoja na nusu iliyopita, mimi nimekuwa nikienda kulala mnamo saa 7:30 usiku nami nimekuwa nikitumia muda mrefu sana kupitia na kusahihisha vitabu vya Unabii (2 na 3). Katika siku chache zilizopita imekuwa ni kama muda wa saa 9 usiku ndipo naenda kulala, na mwili wangu umeanza kuhisi tatizo hilo nami nimekuwa nikijisikia kuchoka kila wakati. Naam Eva amekuwa akiniambia ni punguze kasi ya kufanya kazi hiyo. Yeye amekuwa akiona jinsi nilivyokuwa naanza kuchoka katika siku za hivi karibuni. Naam yeye alinikumbusha tena usiku wa leo, lakini kulikuwa na kitu kilicho kuwa kinaniambia kuwa niendelee tu na wala nisisimame kufanya kazi hiyo. Kwa hiyo mimi nikarudi kwenye kompyuta yangu saa 7:30 usiku wa leo baada ya kupumzika kwa muda mfupi. Mimi japo sikuweza kumaliza kusahihisha kitabu hicho cha Unabii namba 3, lakini nilikuwa karibu sana kufanya hivyo. Naam, hii natumaini itawapeni ninyi mwanga kuhusu ni nini nilicho kuwa na kifanya katika wiki hii iliyopita, lakini hii siyo sababu kuu ya mimi kuandika tukio hilo. Asubuhi hii, niliwasha kompyuta yangu na kuanza tena shughuli ndefu ya kusoma na kufanya masahihisho ya kwenye Kitabu cha 3 cha Unabii. Mimi nilikamilisha kazi ya kusoma na kufanya masahihisho ya Kitabu hicho, lakini nilihitaji kuhakiki Jalanda la Kitabu hicho. Yote ninayo hitaji kufanya ni kuchapa nakala ya jalada la Kitabu Namba 2 na 3 cha Unabii namba 2 na 3, na kuzisoma na kufanya marekebisho yatakiwayo, lakini nilisahau kuwa mashine yangu ya kufanya uchapachi ilikuwa haina wino mweusi, kutoka wakati nilipoitumia kwa mara ya mwisho kwai ilisha anza kutoa ishara ya kuwa wino mweusi ulikuwa umeisha. Wakati wa kuchapa nakala ya jalanda ya kitabu cha kwanza, mashine yangu ilishaanza kutoa ishara ya tahadhari ya kuwa wino mweusi wa mashine hiyo unaelekea kwisha. Hili limeniletea shinikizo kubwa kweli kweli kwa maana Wachapaji walinipa muda wa wiki mbili tu, ili kufanya masahihisho ya vitabu hivyo viwili, na kwa sababu fulani ambayo sielewi, Bwana amekuwa akiniambia nikeshe usiku kucha na asubuhi yote ili kumalizia masahihisho hayo. Naam, tatizo ni kuwa, mimi nimemaliza Fedha zangu benki na kukopa benki Dola $200, nami sina Fedha ya kununulia wino huo mweusi wa mashine hiyo, wino ulio na dhamani ya Dola 25. Wachapaji hawakunishinikiza sana - ila Bwana. Mimi nilijua kuna lazima kuna sababu fulani inayo mfanya Bwana kunishinikiza kiasi hicho na kunifany nikakukesha nikiwa nafanya kazi kwa juhudi zote, lakini mimi niko hoi taabani hivi sasa. Kwa hiyo mimi nilienda kwa kaka yangu Ted aliye kule chini na kumwomba anikopeshe hela kidogo, ili niweze kununua wino huo. Yeye alisema hivi na vile, na ilikuwa inaonekana wazi kuwa asingeliweza kunipkopesha kwa muda ule. Kwa hiyo mimi nikaamua kurudi kule ghorofani na kuanza kuchapa; ilikuona kutatokea nini na rangi ile itakavyotokea humo kwenye mashine hiyo ya kuchapia, au niandike mpaka hapo mashine hiyo itakapo goma kabisa na kusimama. Naam, mimi nilianza kutayarisha mashine hiyo ya kuchapia kwa kuondoa taa ile ya onyo na kuanza kuchapa kwa wino wowote uliokuwapo humo. Mimi sielewi ni watu wangapi watakao weza kuamini hili, lakini pale mashine yangu ya kuchapa ilipoanza kufanya kazi – ishara ile ya kupimia wino, ilinionyeshea kuwa kidao cha kutunza wino mweusi wa kuandikia, ilikuwa IMEJAA. Mimi nilishangazwa sana. Nakujiuliza itawezekanaje hayo. Mimi nimekwisha watumia Wachapaji wa vitabu, nakala iliyofanyiwa masahihisho kwa barua pepe tayari kwa kuUchapaji. Sasa, mimi nimemaliza, na ninangojea vitabu viwili vinavyofuata vya Unabii huu. (Kitabu cha 1 & 4), ili kuvisoma na kuvifanyia masahihisho tayari kwa Uchapaji. Naam sasa, masaa machache baadaye, mimi ni kama nilikuwa katika ulimwengu wa kiroho, nami nilishindwa kurudi kwenye ile hali yangu ya kawaida ya kidunia. Mwili wangu ulikuwa unaonekana haujui ni nini la kufanya. Mimi nimekuwa nikiomba kwa kiasi cha muda wa saa mmoja hivi, lakini nami nilikuwa nimeshindwa kurudi kutoka kwenye hali hiyo ya kiroho. Wakati huo wa maombi, mimi nilijiona kama nimeshindwa kujimiliki na kwa hiyo nikamwomba Bwana msaada. Kisha Bwana Yehova alinipa maono ya Mikono Yake ikiwa inatupa na kukunjua karatasi mmoja kubwa; kama zile za zamani za kuandikia, iitwayo scroll, Mbinguni. Mimi nilikuwa naweza kuona mwisho mmoja wa karatasi hiyo ikijifungua hadi kwenye mawingu ya Mbinguni. Mimi bado sina uhakika na kile "Kitakacho tokea baada ya hapo". Mimi nimeishiwa kabisa na bila ya fedha yeyote na tena mwili wangu ukiwa umechoka kabisa kabisa. Naam, mimi nadhani sitakuja kukaa na kuelewa Ratiba ya Bwana. Nakusifu Wewe Ee Bwana, nami bado najaribu kuvumilia! Lakini je vipi kuhusu safari ya Amerika ya Kusini?
|
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )