|
404.
Occurrence given to Raymond Aguilera on 7 February 1994 that day and the
next morning. My friend drove and found a place to camp approximately an hour outside the Utah border. We decided to camp there for the evening since it was about 1 AM. So we camped inside the truck. During prayer, that early morning, I saw a vision of six figures in a circle, they looked like American Indians by appearance, and they were spiritual. As I watched the six figures, they started summoning or calling an angel of death to come after us.
When I realized this I went into prayer and their curses were neutralized by the Lord. What they were calling looked like a bird of some kind and it had a long neck that resembled the end of a pencil eraser with two eyes and a black body. I could see it flying in our direction and flying in a stalking pattern like what an eagle would do.
The Lord instructed me to stay put where we were camped and not to move. So we camped all day at the same desolate spot in our truck. I didn't say it, but I was afraid to camp outside of the truck because of all the spiritual warfare, the day before at Brigham Young University, and for the actual physical attacks I received the following evening. I didn't want to be caught out in the open, and I was still in a lot of physical pain from the day before. I remember, as I was changing my socks, a long white hair had grown on the side of my foot where no hair grows. It freaked me out, for this hair was about an inch and a half to two inches long and there was no way I could not have seen it before, and it was in the same area that my foot was squeezed the night before as I was driving out of Utah. Even in pain, I had a hard time staying put. I remember how hard it was for me to sit in the truck and do nothing and wait on the Lord. I felt like I was going to go out of my mind. So I tried to occupy myself. My roommate didn't seem to have a problem with staying put, but I sure did. Since the Lord said to stay put we did. We didn't remove any of our camping equipment, we just sat until the Lord gave us instructions to leave. So we stayed in our truck and waited, and waited, and waited until the Lord instructed us to spend another night there. It was a good thing we spent the night in the truck, for a major storm hit the area that night, with lighting and hail, that beat our truck like we were being hit by golf balls, and the lightning was extremely close. My roommate said, after the thunder, there was only a count of one before the flash of the lightning was seen. This was a scary storm. It seemed to me like we were in a middle of an air attack and we were being bombed, and the wind was incredible, it was actually blowing my truck from side to side and it felt like someone was rocking it and going to push it over. My friend said that it was a good thing we had stayed inside the truck as instructed, for the storm would have damaged our camping equipment and possibly hurt us. Then the next morning the Lord said, "You can leave, but drive slowly and keep your eyes and ears open." We did, but about two hours later, while I was in prayer, a sleepiness fell over me as my partner drove. I couldn't keep my eyes open. I felt my groin hurting again as I prayed. So I changed into some better fitting clothes, then I started praying again, but the sleepiness persisted and I could not keep my eyes open. The Lord kept telling me, "Keep your eyes open and pray and pray." I tried as hard as I could for about twenty minutes and I think at one point I fell asleep.
|
404.
Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 7 Februari 1994, siku hiyo na siku
iliyofuata. Rafiki yangu yule niliyekuwa ninasafiri naye aliendesha gari na kupata mahali pakuweka kambi kitu kama mwendo wa saa mmoja kutoka mpaka wa Utah. Sisi tukaamua kuweka kambi pale kwa ajili ya jioni ile kama maana ilikuwa tayari ni kitu kama saa 7 usiku. Kwahiyo sisi tukapiga kambi ndani ya gari letu hilo. Wakati wa sala, mapema asubuhi ile, mimi niliona maono ya maumbile ya kitu kama watu sita wakiwa katika mviringo, walikuwa wanaonekana kama wale Wahindi wekundu wa Amerika, nao walikuwa katika ulimwengu wa kiroho. Wakati mimi naangalia maumbile ya wale watu sita; ambao wana sura ya wale wahindi wekundu, walianza kuita au kuwaamuru malaika wa kifo ili watufuatie sisi kwa nyuma ilikutuua.
Wakati nilipo tambua hivyo mimi nilianza kuomba na laana yao ile ikavunjwa mara na Bwana. Walichokuwa wanaliitia lilikuwa ni aina fulani ya ndege ambaye alikuwa na shingo ndefu sana ambayo inafanana sana na ncha ya kalamu ya risasi kwa mbele akiwa na macho mawili na mwili mweusi. Mimi nilikuwa ninamwona akiruka kuelekea upande wetu na alikuwa anaruka kama mwewe arukavyo anavyo jaribu kushika windo.
Bwana akatuagiza tukae hapo hapo tulipo piga kambi, na tusiondoke kwenda popote. Kwa hiyo tulipiga kambi siku nzima hapo kwenye eneo hilo ambalo lilikuwa ni ukiwa mtupu ndani ya gari letu. Mimi sikusema, lakini kwa kweli niliogopa kwenda kupiga kambi nje ya gari kwa sababu ya vile vita vyote vya pale, siku ile ya kabla pale kwenye Chuo Kikuu cha “Brigham Young”, na kwa ajili ya mapambano ya kimwili ambayo mimi nilipata jioni ile kabla ya siku ile. Mimi sikupenda ni kamatwe pale nje, na mimi bado nilikuwa na maumivu makubwa kutokana na mapambano ya siku ile ya kabla ya leo. Nakumbuka nilikuwa ninabadilisha soksi yangu ambako nilikuta unywele mrefu sana mweupe ukiwa umeota kwenye sehemu fulani ya mguu wangu mahali ambapo kwa kawaida hakuna unywele unaotarajiwa kuota. Ilinitisha sana, kwa maana unywele huo ulikuwa na urefu wa kitu kama nchi mmoja na nusu au kama nchi mbili na hapakuwa na njia yeyote ambayo mimi ningelishindwa kuuona hapo kabla na ilikuwa kwenye eneo hilo hilo ambako mguu wangu ulikuwa umebanwa usiku uliopita wakati mimi nilipokuwa ninaendesha kutoka kwenye Jimbo la Utah. Wakati nikiwa bado niko kwenye maumivu nilikuwa na patwa na wakati mgumu wa kuendelea na mapambano. Nakumbuka jinsi ilivyo kuwa ngumu kukaa ndani ya gari nikawa sifanyi lolote zaidi ya kumgojea Bwana kutoa maelekezo zaidi. Nilikuwa najisikia kana kwamba ningelirukwa na akili. Hivyo nikajaribu kujipa moyo. Yule mwenzangu alikuwa anaonekana kama hana shida yeyote ya kukaa na kutulia akiwa anamgojea Bwana atoe maelekezo yake, lakini mimi nilikuwa na wakati mgumu. Kwa kuwa Bwana alisema tukae tumngojee, sisi ilitubidi tufanye hivyo. Sisi hatukuondoa vifaa vyetu vya kupiga kambi pale, bali tulikaa tu mpaka Bwana alipotupa agizo la sisi kuondoka. Kwa hiyo sisi tulikaa kwenye gari letu tukawa tuna ngoja na kungoja hadi Bwana alipoagiza kuwa tukae usiku mwingine tena pale. Ilikuwa ni jambo njema kuwa tuliamua kulala ndani ya gari lile, kwa maana dhuruba kubwa iliipiga mahali pale usiku ule ikiwa na radi na umeme na mvua ya mawe ikawa inaipiga gari letu utadhania kuwa inapigwa kwa mipira ile ngumu ya kuchezea golfu, na umeme na radi ilikuwa inapiga karibu karibu sana. Mwenzangu akaniambia ulikuwa unaweza kuhesabu mmoja tu baada ya ngurumo la radi kabla hujaona umeme ukipita kuonyesha kuwa radi ilikuwa ina piga kwa mfululizo na katika umbali mfupi tu na pale. Hili lilikuwa ni dhoruba iliyokuwa inatisha. Kwangu mimi ilikuwa inaonekana kana kwamba sisi tulikuwa ndani ya vita vya angani na kana kwamba sisi tulikuwa tunapigwa mabomu, na upepo ulikuwa mkali sana, ulikuwa unaisukasuka gari letu kutoka upande huu kwenda upande ule, na utadhani kulikuwa kuna mtu aliyekuwa anaitingisha tingisha na kujaribu kuisukuma sukuma ili kuipindua. Yule rafiki yangu akaniambia ilikuwa ni jambo jema kuwa tulilala ndani ya gari kama tulivyoagizwa, kwa maana dhoruba ile ingeliweza kuharibu vifaa vyetu vya kambi na pia inawezekana ingelituumiza hata na sisi pia. Kisha asubuhi iliyofuata Bwana akaniambia, "Unaweza kuondoka, lakini endesha kwa uangalifu na hakikisha macho yako na masikio yako yawe wazi." Sisi tulifanya, lakini baada ya masaa mawili hivi baadaye, wakati mimi nilipokuwa bado niko kwenye maombi, usingizi ukaanza kunishika wakati yule mwenzangu alipokuwa anaendesha. Nilikuwa naweza kufungua macho yangu. Nilianza kusikia nguo zangu (groin) zikianza kuniaumiza kwa hiyo nikavaa nguo zingine ambazo hazini bani sana, kisha nikaanza kuomba tena lakini usingizi ukaendelea kunizonga na nilikuwa nashindwa kuacha macho yangu wazi. Bwana akaendelea kusema “Acha macho yako wazi na uombe na uombe sana.” Mimi nilijaribu kwa bidii zote kwa kadri ya uwezo wangu kwa muda wa dakika ishirini hivi na nadhani kuna wakati nilishindwa na kulala usingizi.
|
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )