|
649.
Occurrence given to Raymond Aguilera on 27 November 1990 at 10:30 PM.
On Thanksgiving Day, November 28, 1990 four years ago and almost at the same time another miracle happened to me. On the night of the 27th the day before Thanksgiving 1990, I had been hearing all kinds of voices some from the devil and some from God and had been doing a lot of arguing with God about my special friend. I was totally mixed up. I tried to explain to the Holy Spirit that I couldn't believe anything that was being said. So I just got mad at God and I told Him that I didn't want to hear anymore from Him. That I was going to stop listening to any voice. Voices kept telling me that my special friend was no good and other voices kept telling that she was okay. During this time in my life every conceivable thing was said to me. So I got mad at God. I started arguing with Him the minute His Presence came into my room that Thanksgiving eve. At about 10:30 PM. that evening I remember I argued with the Holy Spirit and kept saying No!! to everything He said. The Holy Spirit kept saying this and that, and I kept saying No!, No!, No! to everything the Holy Spirit said. I would cover my ears and say, "No!, No!, No!, go away. I am not going to listen to anyone anymore. For I thought He was a demon. I was very adamant about it. I tried binding it and rebuking it. You name it, I tried it. Finally the Holy Spirit stopped. I thought whatever it was; it finally gave up. By this time it was 3 AM., Thanksgiving morning. So after a few hours of sleep I got out of bed about 9:30 AM.. I took a shower and was getting ready for a Thanksgiving Church service. I didn't know what time it was suppose to start. So I placed my wrist watch on the bathroom sink so I wouldn't forget it and proceeded to get ready. Once I had gotten myself cleaned up, I was on my way to church and still mad at God. I had been on the road about twenty minutes and realized I didn't know if I was early or late for the church service. So I looked at my watch and noticed I had no watch and had left it on the bathroom counter. I was still very upset and decided to proceed even if I was an hour early and wait in my car until the service started. To my surprise, I reached the church about fifteen minutes before it started. I went into the church and sat down near the front. During the worship I saw an image of Christ in the front of the church behind the pastor, but I still didn't know what I was seeing, what it was or who it was. I still had a lot of doubt. I remember telling a friend that sat next to me what I saw. She was shocked of what I could see. The pastor started giving a sermon after the worship and during the sermon the pastor said we should thank the Lord for all the blessing we had received during the year. I was still feeling bad because I didn't know who I was rebuking. So I repented. I said, "Lord I am sorry if I offended you, but I really don't know who was talking and who to believe and I apologized to you Lord if I am wrong." Then within a second or two after I had repented. I noticed something on my wrist. My watch appeared on my wrist out of nowhere. It totally surprised me. I was shocked. I told my friend that was setting next to me. I said to her, "The Lord placed my watch on my wrist. It wasn't there before." She said, "What!! I said, "The Lord placed my watch on my wrist for I had left it at home on the bathroom counter and look I have my watch." She was all excited and I was too. So after the service I told the pastor what had happened and that I had gotten into an argument with God. And that the Lord was showing me His power. "No," said the pastor, "I don't think it has to do with power, I think it has to do with time. I don't think it has to do with power," he said again. I think it has to do with time. But I didn't believe him. Then a day later I was telling a sister in the Lord what had happened and she said the same thing. She said, "If the Lord wanted to show you His power. He could send you to China. He didn't need to place your watch onto your wrist." With this second confirmation, I was beginning to see that they were right. That evening the Lord appeared again. And that was the evening that the Lord told me to go an anoint Mt. Diablo on, Sunday, December 2, 1990, and to tell the Friday night singles group that the Lord wanted people to go an anoint the mountain. For He was going to take the mountain away from the devil. This whole thing was overwhelming for here four years later the Lord performs another miracle ALMOST TO THE HOUR by moving a wrongly drilled door knob hole a 1/4 of an inch. So my new bedroom door wouldn't be ruined. This Lord, this God of ours, never ceases to surprise me. He seems to be miles, miles and miles ahead of me at all times. I still argue with Him. I still love Him. He is still forgiving me. A very merciful God. Yes, very merciful! I guess that's all. (over)
|
649.
Matukio aliyopewa to Raymond Aguilera tarehe 27 Novemba 1990, saa 4:30 za
usiku.
Siku ya kutoa shukrani ya tarehe 28 Novemba, 1990 miaka minne iliyopita na karibu kuwa wakati mmoja na hili tokea la mwaka huu, muujiza mwingine ulinitokea. Usiku wa tarehe 27 Novemba kabla ya siku ya kutoa shukrani ya mwaka 1990, mimi nilikuwa nikisikia kila aina ya sauti, nyingine ikiwa inatoka kwa shetani na ingine ikiwa inatoka kwa Mungu, nami nilikuwa nikibishana kweli na Mungu kuhusu rafiki yangu fulani aliyekuwa maalum kwangu. Mimi nilikuwa nimechanganyikiwa kabisa. Mimi nilikuwa ninajaribu kumweleza Roho Mtakatifu kuwa; mimi siamini chochote kile kinachosemwa. Kwa hiyo mimi nikaendelea kumkasirikia Mungu na kumwambia mimi sitaki kusikia lolote zaidi kutoka Kwake. Na ya kuwa mimi ningelienda kukataa kusikiliza sauti Yeyote. Sauti ikawa inaendelea kuniambia kuwa yule rafiki yangu maalum alikuwa si wa maana yeyote na sauti nyingine ikisema kuwa yule rafiki yangu alikuwa ni safi. Wakati huo katika maisha yangu, kila aina ya jambo unayoweza kufikiria nilikuwa ninaambiwa. Kwa hiyo mimi nikawa nimemkasirikia Mungu. Mimi nilianza kubishana Naye mara pale Uwepo wake ulipokuja kwenye chumba changu jioni ya siku ile ya kutoa shukrani. Wakati wa saa 4:30 ya jioni ya siku ile nakumbuka nilikuwa nimebishana na Roho Mtakatifu na nikawa nimeng’ang’ania kusema, “Hapana!! Kwa kila kitu alichokisema. Roho Mtakatifu alikuwa anaendelea kusema hili na lile, nami nilikuwa nimeng’ang’ania kusema, “Hapana! Hapana! Hapana! Nenda zako.” Mimi sitaenda kusikiliza lolote zaidi. Kwa maana mimi nilidhania kuwa ilikuwa ni pepo mchafu. Mimi nilikuwa nimeling’ang’ania jambo hilo. Mimi nilijaribu kulifunga na kulikemea pepo hilo. Kila kitu unachoweza kulifikiria mimi nililijaribu. Mwishoni Roho Mtakatifu akaacha. Mimi nilidhania kuwa hicho kitu kitakuwa kimekata tamaa mwishoni; wakati huo ilikuwa imekwisha fika saa 9 za alfajiri ya asubuhi ya siku ya shukrani. Kwa hiyo baada ya masaa machache ya usingizi nikawa nimeamka kwenye saa 3:30 za asubuhi. Nikawa nimeingia bafuni na kuoga tayari kwa ajili ya misa ya shukrani. Mimi sikujua misa hiyo ingelianza saa ngapi. Kwa hiyo mimi nikawa nimeweka saa yangu kwenye sinki ya bafuni ili nisije nikaisahau nakuendelea kujitayarisha. Mara nilipomaliza kuoga na kujisafisha, nikawa nimeendoka kwenda kanisani na bado nikiwa nimemkasirikia Mungu. Nikawa niko tayari barabara kwenye safari yangu, baada muda wa dakika ishirini hivi, nikatambua kuwa sikuwa ninaelewa kama nimewahi au nimechelewa misa. Kwahiyo mimi nikatazama saa yangu na kutambua kuwa sikuwa na saa mkononi na yakuwa nilikuwa nimeiacha kule juu ya meza ya bafu yangu. Mimi bado nilikuwa nimeudhika sana na kuamua kuendelea na safari yangu hata kama itakuja kutokea kuwa nimewahi kwa saa nzima na kungoja kwenye gari langu hadi hapo misa itakapoanza. Kwa mshangao wangu, mimi nilikuwa nimewahi kanisani kwa dakika kumi na tano hivi kabla ya kuanza misaa hiyo. Mimi nikaingia kanisani na kukaa chini kwenye viti vya mbele ya kanisa. Wakati wa kuabudi mimi niliona maono ya Yesu mbele ya kanisa nyuma ya mchungaji, lakini mimi bado nilikuwa sielewi ni nini nilichokuwa ninakiona, kilikuwa nini au ni nani nilikuwa ninamwona. Mimi bado nilikuwa na mashaka. Nakumbuka nilimwambia rafiki yangu aliyekuwa amekaa karibu nami kuhusu kile nilichokuwa ninakiona. Yeye alishutushwa sana na kile mimi ninalicho kuwa naweza kukiona. Mchungaji akaanza kutoa mahubiri baada ya kuabudi na wakati wa mahubiri mchungaji akasema ni lazima tumshukuru Bwana kwa ajili ya baraka zote alizotupatia kwa mwaka wote. Mimi bado nilikuwa ninajisikia vibaya kwa sababu bado nilikuwa sielwi ni nini nilichokuwa ninakikaripia. Kwa hiyo nikaaza kutubu. Mimi nikasema, "Bwana unisamehe kama nilikuudhi wewe, lakini kwa kweli mimi sikuwa ninafahamu ni nani aliyekuwa anaongea nami na nimwamini nani na ninaomba radhi unisamehe Bwana kama nimekukosea.” Kisha baada ya sekunde mmoja au mbili hivi baada ya kutubu tu, mara nikaanza kuhisi kuwa kulikuwa kuna kitu mkononi mwangu. Saa yangu ikaonekana juu ya mkono wangu bila kujua imetokea wapi. Ilinishangaza sana. Mimi nilistuka kweli. Mimi nikamwambia rafiki yangu yule ambaye alikuwa amekaa karibu nami. Mimi nikamwambia, "Bwana ameniwekea saa yangu kwenye mkono wangu. Haikuwapo hapo kabla." Yeye akaniambia, "Nini!!” Mimi nikasema, "Bwana aliweka saa kwenye mkono wangu kwa maana mimi nilikuwa nimeiacha nyumbani kwenye meza ya bafu, akini tazama hii hapa saa yangu mkononi mwangu.” Yeye alishangaa sana na kuanza kuchangamka kwa furaha nami pia nilikuwa nimechangamka kwa furaha. Kwa hiyo baada ya misa mimi nikamweleza mchungaji kile kilichotokea na yakuwa nilikuwa na mabishano na Mungu. Na kuwa Bwana alitaka kunionyeshea nguvu zake na uwezo wake. "Hapana," yule mchangaji akasema, "Mimi sidhani kama hayo yanauhusiano wowote na nguvu, bali mimi nadhani inahusiana na wakati. Mimi nadhani haina uhusiano na nguvu," akasema tena. Mimi ninadhani hayo yanauhusiano na wakati. Lakini mimi nikawa simwamini maneno ya huyo Mchungaji. Kisha baada ya siku mmoja nikawa nimemwambia dada fulani katika Bwana kuhusu jambo hilo, naye jibu lake lilikuwa sawasawa na hilo hilo (la mchungaji). Yeye alisema, "Kama Bwana angelitaka kukuonyeshea nguvu zake, Yeye angeweza kukupeleka hadi China. Yeye hana haja ya kuweka saa mkononi mwako." Kwa hakiksho hili la pili, mimi nikaanza kuona kuwa wale watu walikuwa sahihi. Jioni ile Bwana akanitokea tena. Na hiyo ndiyo ile jioni ambako Bwana aliniambia kuwa niende kuweka wakfu Mlima Diablo, siku ya Jumapili ya tarehe 2, 1990 na yakuwa niwaambie kile kikundi cha “The Friday night singles group” kuwa Bwana alikuwa anahitaji watu wa kwenda kuuweka wakfu mlima huo. Kwa maana Yeye anaenda kuuchukua mlima huo kutoka kwa shetani. Jambo hili lote lilikuwa linashangaza kwa maana baada ya miaka minne Bwana tena anafanya muujiza mwingine KWA KARIBIA SAA HIYO HIYO kwa kusogeza shimo la kitasa nililolikosea kuitoboa kwa karibia 1/4 ya inchi zima. Ili ule mlango wa chumba changu hicho usiharibike. Huyu Bwana wetu, Mungu wetu huwa haachi kunishangaza mimi kila wakati. Yeye anaonekana kuwa maili na maili mbele yangu nyakati zote. Mimi bado ninabishana Naye. Mimi bado ninampenda Yeye. Yeye bado ananisamehe mimi. Ni Mungu mwenye huruma sana. Ndiyo, ni mwenye huruma sana! Nadhani haya ni yote. (Mwisho).
|
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )