676. Vision given to Raymond Aguilera on 21 January 1995 at 7:40 PM

During praise and worship at church I had a startling vision. There were about six of us listening to praise tapes and I could sense the Presence of the Lord and it was very STRONG. Within minutes, I was in the spirit seeing all kinds of things. But I saw this one startling vision I had never seen before or read about in the Bible.

During this one worship song all six of us were in the spirit and praising the Lord, when I saw a pair of Hands Clapping. I knew it was the Father Jehovah. I couldn't see a Body, but I could see His Hands Clapping in the spirit.

The next image I saw was of Jesus Christ and He was dancing. He was dancing as the Father was Clapping and we were all singing and praising the Lord all at the same time. A very startling vision and it was so REAL! Christ was just dancing and dancing and dancing. He was moving His Body everywhere as He danced to the worship music. I don't think I will ever forget that..., as long as I live. I guess that's all. (over)

676. Maono aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 21 Januari 1995, saa 1:40 jioni.

Wakati wa kusifu na kuabudu kwenye kanisa; mimi nilipatwa na maono ya kutatanisha. Sisi tulikuwa kama watu sita waliokuwa wakisikiliza nyimbo za kusifu kutoka kwenye mkanda wa kunasia sauti nami nilikuwa ninahisi uwepo wa Bwana na ilikuwa ni ya NGUVU KUBWA. Baada ya dakika chache tu; mara nikajikuta nikiwa kwenye ulimwengu wa kiroho nikiwa naona mambo mengi ya kila aina. Lakini niliona hasa maono haya ambayo yalikuwa ni ya kutatanisha sana ambayo kamwe sijawahi kuyaona au kuyasoma kuhusu jambo la namna hii katika Biblia.

Wakati huo wa nyimbo za kuabudu sisi sote sita tulikuwa katika ulimwengu wa kiroho tukiwa tunamtukuza Bwana, ndipo nikaona Mikono Miwili Yakipiga makofi. Mimi nilijua kuwa alikuwa ni Baba Yehova. Mimi nilikuwa sioni Mwili, lakini nilikuwa ninaona Mikono Yake ikipiga Makofi katika Ulimwengu wa Kiroho.

Maono yaliyofuata kuyaona yalikuwa ni ya Yesu Kristo akiwa anacheza.  Yeye alikuwa anacheza wakati Baba akiwa anapiga makofi na sisi sote tukiwa tunaimba na kumsifu Bwana wakati huo huo. Ilikuwa ni maono ya kushangaza na yalikuwa maono yaliyokuwa HALISI KABISA! Kristo alikuwa anacheza dansi na kucheza na kucheza.  Alikuwa anapeleka Mwili wake kila mahali wakati akiwa anacheza dansi hali nyimbo za kuabudu kwenye kinasa sauti hicho inaendelea kuimba. Nadhani kamwe sitakaa kusahau hayo..., kwa muda wote nitakaoishi. (Mwisho).

 

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.