|
898.
Occurrence and Visions given to Raymond Aguilera on 16 April 1996 at 10:30
PM. During Communion prayer and just before having Communion with a few Christian brothers the Lord showed me a corner of a multi-story apartment building. As I watched it in the spirit, I saw it collapse floor by floor until it was totally destroyed by an earthquake. Occurrence and Vision: Then I saw a White Horse flying through the air. It was impressed on my spirit that it represented an Angel of the Lord, I don't know how I knew but it was an Angel in the figure of a White Horse. Then out of nowhere this enormous hand that looked like a gorilla's hand sneaked up and grabbed this White Horse out of the air like it was a small bird; crushed it, and smacked it to the ground. Then this hand somehow transformed it's five fingers into two and went downward with an incredible force toward the crushed Angel. I don't know if it hit the Angel again, but it had great power in its two newly formed fingers. Immediately my prayer language changed, and I felt like I was going to explode from within and I could feel my body and spirit jump into a warfare mode. I got up from my seat and wanted to stop the Communion prayer and get into the war. But something told me I had to finish Communion and get a brother to anoint me with oil before I went into warfare. I had sensed the urgency to pray for two days, but I didn't know why. So for the next half hour to forty-minutes I wailed and found myself flat on the floor with my arms extended out and with my legs together (in the shape of a cross) with an unusual sounding prayer language that at times was quiet and at other times it was loud and fast. My prayer language was acting crazing during this time and I really lost track of time. This large hairy black gorilla's hand reminded me of the gorilla movie, "King Kong," from the thirties or forties. But what was more interesting was the spiritual war I was seeing. This giant hairy black hand was fighting the Lord's Angelic Forces and was beating them. Then I saw what looked like a hole open up in the side of a mountain, and a tunnel extended out with hundreds upon hundreds of black horses (devils) shooting out, and began to help this large black hand fight the White Horses (Angels). I was surprised by the speed of the battle, there wasn't a wasted movement by either of the parties involved, and I could sense in the spirit the Angels were losing the battle. What was also startling was the gorilla's hand; this creature was enormous compared to the White Horses. I mean, his hand was so large it could place a White Horse in it's palm, and these were life size White Horses or Angels or whatever you would like to call them. Vision: Then I was shown hundreds and hundreds of crucified people on crosses in this dark area with white smoke or fog in the background being ripped off from their crosses, and they began to run past me as I watched them in the spirit. I don't know where they went or how they got pulled off the crosses. Vision: Then I saw this dark place with all of these black creatures that had been slain in this battle with the White Horses looking like White melted Puddles laying on top of these black creatures. They all looked like White Blobs on top of black masses. I believe they were all dead for there was no movement. But as I watched and tried to figure out what was happening I saw the White Blobs on the top of the dead looking creatures begin to move. They somehow reformed themselves into the images of White human looking Angels. They no longer looked like White Horses. I don't know why or how it happened, but they went back up into the battle. Vision: Then the next image was of hundreds upon hundreds of White Horses running from the right toward the left at lighting speeds with their manes blowing in the wind. When they got to the area of the battle they surrounded this large black creature. At this point the black creature looked about 5 or 6 miles high compared to the height of the White Horses, but they surrounded it and the battle immediately stopped. And somehow the small White Horses pounded him from the top as the others stayed around the perimeter and pounded him into this large hole in the ground. It looked like this enormous pit, then this enormous lid came over the large pit and they sealed it shut. Then the vision stopped. What was placed in my spirit was that this large creature was a territorial demon with his demon helpers. Boy, I was amazed at how large and powerful it was. (over) Comments: There is more in the spirit than I ever realized. The spiritual war is for real with demons we don't see, and these battles are happening now; this minute. This is a reality that most people don't even believe, but it is still for real. As I watched the spiritual war I felt very helpless. I have been asking myself these questions: 1. How were the crucified saints sucked off their crosses like a vacuum? 2. Why did they run past me into this empty space? 3. Will they come back to their crosses? 4. Did this territorial Demon get larger because the saints were taken off their crosses? People need to PRAY MORE, for in the spirit, there are some very bad demons out there. These things are beyond what our minds can understand, but yet they are very real. I learned something very startling tonight, we really don't know the extent of the dark forces. (over)
|
898.
Matukio na Maono aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 16 Aprili 1996 saa 4:30
usiku. Wakati wa maombi ya Komunio na kabla tu ya kupokea Komunio, tukiwa na ndugu kadhaa katika Kristo, Bwana alinionyeshea korna ya jumba fulani la ghorofa. Wakati nikiwa ninaiangalia jumba hilo katika ulimwengu wa Kiroho, mimi niliona ghorofa za nyumba hiyo zikianguka ghorofa baada ya ghorofa, hadi jumba hilo lote lilipoangamizwa kabisa na tetemeko hilo la ardhi. Maono na Matukio: Kisha nikaona Farasi fulani Mweupe, akiwa anaruka angani. Nilipewa hisia kwenye roho yangu ya kuwa; huyo alikuwa ni Malaika wa Bwana, mimi sijui jinsi nilivyojua, lakini alikuwa ni Malaika katika sura ya Farasi Mweupe. Kisha Bila ya kutarajia mkono fulani mkubwa ambao ulikuwa unaonekana kama ni wa nyani wa aina wa ya gorilla, ulipitishwa kwa kuvizia na kumnyakua farasi huyo angani utadhania; kama kamchukua ndege mdogo; na kumpigiza ardhini na kumvunja vunja. Kisha vidole vile vitano vya mkono wake huyo gorilla, vikabadilika na kuwa vidole viwili, na kisha akaenda chini kwa nguvu ya ajabu kwa Malaika huyo aliyempigiza chini ardhini. Mimi sielewi kama alimtwanga tena huyo Malaika, lakini alikuwa na nguvu kubwa sana kwenye hivyo vidole vyake viwili ambavyo vimeundwa upya. Mara lugha yangu ya maombi ikabadilika, nami nikajisikia kama mtu anayetaka kulipuka kutoka ndani mwangu, nami nilikuwa naweza kusikia mwili wangu na roho yangu ikiwa inarukia na kujipanga katika hali ya mapambano. Mimi nilinyanyuka kutoka pale nilipokuwa nimekaa na nikataka kuacha maombi ya Komunio na kuingia kwenye mapambano hayo. Lakini kitu fulani kikaniambia kuwa nimalize kushiriki Komunio kwanza na kuwaomba hao ndugu wanipake mafuta kabla ya kuingia kwenye mapambano hayo. Mimi nilikuwa nimeshikwa na hamu na uharaka wa kuomba kwa muda wa siku mbili hapo kabla, lakini sikuwa najua ni kwa sababu gani. Kwa hiyo kwa muda wa nusu saa hadi dakika arobaini iliyofuata mimi nilikuwa nalia na kuomboleza na kujikuta nikiwa nimelala kifudifudi kwenye sakafu na mikono yangu ikiwa imenyooshwa na miguu yangu ikiwa imewekwa pamoja (katika mfano wa msalaba) na huku nikiwa natoa mlio wa ajabu wa lugha ya maombi ambako kuna wakati inakuwa kimya na wakati mwingine inakuwa ni ya sauti kubwa na ya haraka haraka. Lugha yangu ya maombi ilikuwa kwenye maombi mazito ikipayuka kama mwenda wazimu, nami mara nikawa nimepoteza wazo la muda. Nyani huyo wa aina ya gorilla alinikumbusha sinema ile iitwayo, "King Kong," ya miaka ya thelethini au arobaini. Lakini la kuvutia zaidi ilikuwa ni yale mapambano ya kiroho ambayo nilikuwa nayaona. Mkono huo wenye manyoya ulikuwa ukipambana na Majeshi ya Malaika wa Bwana na ulikuwa unaonekana unawashinda Jeshi hilo la Malaika. Kisha kitu kilicho kuwa kinaonekana kama tundu kilifunguka ndani ya mlima fulani, na handani ndefu ilijitokeza na mamiya kwa mamiya ya farasi weusi (mashetani) walijitokeza wakiwa wanarusha mishale na kuanza kuusaidia mkono huo mweusi mkubwa uliokuwa unapigana na hao Mafarasi Weupe (Malaika). Mimi nilishangazwa na kasi ya vita hivyo, kwani hapakuwa na muda uliokuwa unapotezwa na pande hizo mbili, nami nilikuwa naweza kuhisi kuwa hao Malaika wa kiroho walikuwa wanapoteza mapamabano hayo. Cha kushangaza pia ilikuwa ni ule mkono wa yule gorilla; huyo kiumbe alikuwa ni mkubwa sana ukilinganisha na hao farasi weupe. Namaanisha mkono wake ulikuwa ni mkubwa sana kiasi cha kuweza kuweka farasi mweupe kwenye kiganja chake, na hao farasi walikuwa ni wakubwa kama hao tulio nao katika ulimwengu wa mwili ambao ni Malaika au utakavyotaka kuwaita. Maono: Ksiha nikaonyeshewa mamia na mamia ya watu walio kuwa wamesulubishwa misalabani, katika eneo fulani iliyo na giza ikiwa na moshi au ukungu mweupe, wakiwa wananyofolewa kutoka kwenye misalaba yao, nao wakaanza kukimbia kupitia pale nilipo, wakati nikiwa ninawaangalia katika ulimwengu wa kiroho. Mimi sijui walikuwa wanaenda wapi au jinsi walivyo nyofolewa kutoka kule msalabani. Maono: Kisha nikaona sehemu fulani ya giza ikiwa na viumbo hivyo vyeusi ambao wameuawa katika vita hivyo na hao Farasi Weupe wakiwa wanaonekana kama walio yeyushwa na kuwa Vidimbwi Vyeupe na vikiwa vimekaa juu ya viumbe hivyo vyeupe. Wao walikuwa wanaonekana kama Matone Myeupe juu ya rundo la vitu vyeusi. Naamini wao wote walikuwa wamekufa kwa maana hapakuwa na dalili ya uhai au kujitikisa. Lakini wakati nilipokuwa naangalia na kujaribu kujua ni nini kilikuwa kinatokea pale, mimi niliona matone Meupe juu ya viumbe hivyo vilivyo kufa; vikianza kunyanyuka. Wao kwa namna fulani walijigeuza na kuwa Malaika wenye sura Nyeupe ya kibinadamu. Wao walikuwa hawaonekani tena kama Farasi Weupe. Mimi sijui ni kwa nini au ni kwa vipi ilivyotokea, lakini wote walirudi kwenda kwenye mapambano. Maono: Kisha maono yaliyofuata yalikuwa ni ya mamia juu ya mamia ya Mafarasi Weupe wakiwa wanakimbia kutoka kulia kuelekea kushoto kwa mwendo wa kasi sana sana (kasi ya umwanga) na singa za shingo zao zikiwa zinapeperushwa na upepo. Wakati walipofika kwenye eneo la mapigano walimzunguka yule kiumbe mkubwa na mweusi. Wakati huo kiumbe huyo mweusi alikuwa anaonekana kuwa na urefu wa maili 5 hadi 6 ukilinganisha na urefu wa hao Mafarasi Weupe, lakini walimzunguka na mara mapambano hayo yalikoma mara mmoja. Kwa namna fulani hao farasi Weupe walianza kumponda kutoka juu wakati wengine wakiwa wamemzunguka na kumtwanga ili aingie kwenye shimo fulani kubwa sana iliyokuwa hapo ardhini, na kisha kifuniko fulani kikubwa sana cha kufunika shimo hilo likaja juu yake, na likawekea mhuri au lakiri (seal) ili lisifunguliwe. Kisha maono hayo yakakoma. Kile kilicho wekwa kwenye roho yangu ilikuwa ni kuwa huyo mnyama mkubwa alikuwa ni pepo anayetawala eneo fulani akiwa na mapepo waliokuwa wanamsaidia. Ndugu yangu mimi nilishangazwa kuhusu jinsi alivyokuwa mkubwa na mwenye nguvu nyingi sana. (Mwisho). Angalizo: Kuna zaidi katika ulimwengu wa kiroho kuliko tunavyoweza kudhania. Vita vya kiroho ni vya uhakika, tukiwa tunapigana na mapepo tusiowaona, na vita hivyo vinapinganwa sasa hivi dakika hii. Huu ni ukweli ambao watu wala hawaamani, lakini bado ni ukweli mtupu. Wakati nikiwa naangalia mapambano hayo katika ulimwengu wa kiroho mimi nilijisikia kama sina lolote la kufanya. Mimi nimekuwa nikijiuliza maswali haya: 1. Je, hao watakatifu walio sulubishwa walinyofolewaje kutoka kwenye misalaba yao kama ifanyavyo ufagio wa kunyonyea taka wa umeme au smaku? 2. Ni kwa nini walikimbia kupitia pale nilipokuwa mimi kwenda kwenye sehemu ya utupu? 3. Je watarudi kwenye misalaba hiyo? 4. Je, hao Mapepo watawala wa eneo wamekuwa wakubwa kwa sababu watakatifu walikuwa wamechukuliwa kutoka kwenye misalaba? Watu wanahitaji KUOMBA ZAIDI, kwa maana ndani ya ulimwengu wa Kiroho kuna mapepo wabaya sana huko. Mambo haya yako juu ya uwezo wa akili zetu kuweza kutafakari, lakini bado ni mambo ya ukweli mtupu. Mimi nilijifunza kitu fulani ambacho kilinitatiza usiku huu wa leo, nayakuwa kwa uhakika sisi hatujui uhalisi wa pepo wabaya. (Mwisho).
|
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )